Rais Kikwete awaombe radhi Wanyarwanda

Status
Not open for further replies.
Watu kama nyie ndiyo huwa mnawafumania wake zenu kisha unamwambia vaa twende nyumbani, unamwambia nimekusamehe lakini usirudie hata ajakuomba msamaha.

Ritz nimependa ulivyo andika pamja na kuwa huwa tunatofautiana mda mwingi kimtazamo ila kwa hili la Rais wa Tanzania kuomba radhi kwa Kagame siungi mkono hata ukiniwekea AK47 shingoni kwani itakuwa imetuzalilisha watanzania wote na si Rais kama yeye.
 
Fashisti Nduli Kagame ananuka damu .... Mtu huyu ni mshenzi, ameua watu wengi! Na sasa tutampiga. Uwezo wa kumpiga tunao, sababu za kumpiga tunazo, na sasa tumepata nia ya kumpiga. Sasa tutampiga!
 
KUNA msuguano wa waziwazi unaoendelea kati ya Tanzania na Rwanda kufuatia ushauri wa Rais Jakaya Kikwete kwa mwenzake Paul Kagame, kumtaka akae na kuzungumza na waasi wa FDLR.


Msuguano huo ulianza muda mfupi tu baada ya kumalizika kwa kikao cha viongozi wa nchi za Maziwa Makuu kilichofanyika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) na kuhudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, chini ya uenyekiti wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.


Rais Kikwete alimtaarifu Rais Museveni kile walichojadili baada ya yeye kuchelewa kufika. Alisema ni vema serikali za Rwanda na Uganda zikakaa na kuzungumza na makundi ya waasi wa nchi zao, na kulitolea mfano kundi la waasi wa Rwanda la FDLR.


Inasemekana ushauri huo uliungwa mkono na Rais Museveni, lakini ulipingwa vikali na Serikali ya Kigali, na tangu wakati huo hadi sasa yamesikika matamshi ya ubabe kutoka kila upande.


Alhamisi wiki hii, Tanzania kupitia kwa Ofisa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mkumbwa Ally, imetoa onyo kwa Kigali kuwa wasithubutu kuanzisha vita dhidi ya Tanzania kwa kuwa kitendo hicho kitajibiwa vikali.


Onyo hilo la Dar es Salaam limekuja kutokana na kauli ya vitisho inayodaiwa kutolewa na Rais Kagame hivi karibuni mjini Kigali kwamba: “Sitapoteza muda wangu kumjibu Kikwete, inajulikana maana kuna mahali hataweza kuvuka…haiwezekani.”


Kwanza lazima nikiri kuwa ushauri huo wa Rais Kikwete ni mzuri kutokana na dhamira njema iliyobeba ushauri huo. Dhamira inayolenga kuyapatia ufumbuzi wa kudumu matatizo ya kiusalama yanayozikabili nchi za Rwanda, Uganda na DRC kwa miongo kadhaa sasa.


Hata hivyo, ushauri huu haukuwa sahihi na haukutolewa mahali sahihi. Haukuwa sahihi kwa sababu haukuzingatia ukweli na mtazamo wa Kigali juu ya kundi la waasi la FDLR.


Kundi la FDLR linaundwa na wanamgambo wa Interahamwe na wanajeshi wa zamani wa jeshi la nchi hiyo chini ya aliyekuwa Rais wa Rwanda hayati Juvenal Habyarimana anayedaiwa kuuawa na vikosi vya Rwandese Patriotic Front vya Rais Kagame mwaka 1994 wakati akitokea Tanzania kwenye mazungumzo ya amani kati ya serikali yake na Kagame.


Interahamwe na lililokuwa jeshi la Habyarimana ndio waliotekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani wa Rwanda mwaka 1994. Waliposhindwa vita mwaka 1994 dhidi ya vikosi vya Rais Kagame, walikimbilia katika misitu ya DRC iliyo mashariki mwa nchi hiyo na kuunda kundi hilo la FDLR.


Rais Kagame na mamilioni ya wananchi wa Rwanda wa kabila la Watutsi na Wahutu wachache wenye msimamo wa wastani, ni waathirika wakubwa wa ukatili na unyama uliofanywa na FDLR, na bila shaka hawajasahau wala kusamehe.


Rais Kikwete alipaswa kuzingatia ukweli huu kabla ya kuamua kutoa ushauri wake. Kama angezingatia ukweli huu kabla, bila shaka asingethubutu kumshauri Rais Kagame kukaa meza moja na kundi ambalo halijawahi kuomba msamaha kwa Wanyarwanda wala kuonyesha kujutia uovu wao.


Halafu Rais Kikwete alikosea kutoa ushauri huo mbele ya mkutano ule. Hapakuwa mahali sahihi kwa jambo zito kama hilo. Angetafuta nafasi nyingine, na kwa maoni yangu angezungumza na marais wenzake kwa faragha, ama wote kwa pamoja au mmoja mmoja.


Angepata nafasi nzuri zaidi ya kufafanua dhamira ya ushauri wake, na pia angeweza kuona mwitikio wa Rais Kagame juu ya ushauri huo. Ninaamini msuguano wa sasa usingekuwepo kwa sababu wangejadiliana kwa kina na kuyamaliza mambo yote katika chumba kilichofungwa milango.


Sasa ushauri unataka kuzaa vita ya majirani wawili wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Bila shaka madhara yake ni makubwa. Mbali na kusababisha kuharibika kwa mahusiano kati ya nchi hizi, pia zitapoteza maisha ya watu wake na rasilimali, na hivyo kuteteresha uchumi wa kila moja.


Ni imani yangu Watanzania wengi hawataki na hawawezi kuunga mkono uamuzi wa kuingia vitani na Rwanda. Watanzania hawapo tayari kwa vita vingine, baada ya vile vya Uganda vya mwaka 1978. Tunataka kujenga nchi yetu kiuchumi, kisiasa na kijamii kukimbizana na wakati kwa sababu tupo nyuma sana.


Namshauri Rais Kikwete awaombe radhi Wanyarwanda, amuombe radhi Rais Kagame. Ampigie simu amwambie yaishe kwa kuwa hakukusudia kumuudhi wala kumkumbusha machungu ya unyama wa Interahamwe, amwalike Dar es Salaam wanywe chai na mnyinyo.


Na George Maziku
0659985064

Sasa wewe ulitaka Mh. Kikwete atoe ule ushauri akiwa wapi habari maelezo? Kama Jews na Germans wamekaa meza moja, why note Wanyarwanda? Raisi wetu alitoa ushauri na its up to Kigali to take it or leave it, why all this fuss niushauri Kikwete hajawalazimisha.
 
Wewe mleta mada kweli unaturudisha nyuma hii mada ilishajadiliwa sana hapa JF ila waambie watusi wenzio kuwa JK hana sababu ya kuomba radhi kwa PK,anachosubiri PK ni kile kilichomtokea CHARLES T.aliyekuwa raisi wa liberia kifungo cha maisha kule ICC,Janja yake ina mwisho.Kwa akili yako unadhani ataishinda vita yake na FDLR???.
 
experience ya kupigana na waasi nadhani ndiyo inayompa kiburi huyu bwana mdogo kagame,haya sijui sisi tuna ipi zaidi ya ile ya nduli amin,au ana DRONES, manake kanajiamini,unaweza kumdharau kumbe ana ngumi za chembe,ila huyu jamaa ni kamanda sana
 
Kimsingi sidhani km huyo ni mtz au anataka kujua zaidi. Pia hana details za kutosha na kiswahili chake cha kubambanya.
 
Khaa!!! wewe bure kabisa! amuombe msamaha kwa lipi? Kumpa ushauri? Ningekuwa JK kwanza ningeanza kumwambia aache kuwasaidia M23 kisha ndiyo akae na ndugu zake waongee wayamalize[/QUOTE

Kwa ulofa wa mawazo kama huu sishangai watawala wa sasa wanaandaa mauaji ya kimbari kupitia dini zetu! Kama unaweza sahau haraka hivi mauaji ya kimbari ya Rwanda,1994,utawezaje kujua kama uchochezi wa kidini unaoendelea nchini ni kiberiti kitakacho ripuka siku moja na kusababisha mauaji mabaya sana nchini kwetu? Kwanini Waafrika tuwasahulifu kama nyumbu?!
 
Ng'wamapalala, with due diligence naomba nitofautiane na wewe katika hili maana conclusion yako is short of both political and spiritual diplomacy. Nitajikita katika spiritual diplomacy ambayo naamini na wewe unayo to some extent as not long time back you stated to have been altar boy. Even though you were at tender age but catechism teaches us to reconcile, confess and self negation. So as ex- altar you should know that sincere penance is complete when you apologise sincerely even to those who have trespassed or done wrong to you.To put myself in the shoes of many, Kagame has done wrong to President Kikwete in all the remarks uttered following Kikwete's advice. However, as a spirit of tolerance and forgiveness Kikwete's apology to Kagame can add value. It's hard for normal human being to do but as a matter of fact, that's how spiritually we are supposed to die a little for a better world. Nawasilisha
Mkuu Bigaraone ,
I really don't understand why you want or you would like Pres. Kikwete to apologise to Pres. Kagame for offering a well deserved peaceful advice.

Even Jesus saw such incidence will one day happen in this world and he decide to give a well thought advice to his disciples by saying on Matthew 5:9
Blessed are the peacemakers, for they will be called the children of God.
He went on to say on Luke 10:5-6,
Whenever you enter a house, first say, 'May peace be on this house!'
And if a peace-loving person is there, your peace will remain on him, but if not, it will return to you.
He finish off by saying on Luke 10:10-11
But whenever you enter a town and the people do not welcome you, go into its streets and say,
Even the dust of your town that clings to our feet we wipe off against you. Nevertheless know this: The kingdom of God has come.'

Pres. Kikwete has done exact the same and wipe off the dust of Rwanda conflict from his deliberating.

It's up to Pres. Kagame to diggest and swallow or vomit.

Sijaona bado kosa la Rais Kikwete na sidhani kama nitaliona. Hizi kelele nyingi kutoka serikali ya Rwanda wala hazina mshindo wowote kwa macho ya wapenda amani wengi.
 
Last edited by a moderator:
Kagame aombwe msamaha kwa lipi! Kuambiwa uweli?

Huyu mwandishi amenikera kweli. Nadhani hajasoma vizuri historia ya Rwanda. Nisiende huko kwa kuwa nina jazba. JK akimuomba msamaha Kagame kwa njia yoyote ile nahama nchi. Kagame aombwe msamaha kwa lipi? yeye ndiye anatakiwa aombe msamaha kwa JK.
 
kwanza mleta mada hana detail za kutosha.anaposema mamilion ya wanyarwanda.pengine anaonekana hajui hata population density ya nchi yao ni watu wachache.
 
George Maziku ni dhaifu kuliko dhaifu original!!! Unafikiri akiomba radhi Kikwete itakuwa kaomba yeye binafsi au Tanzania ndio itakuwa imeomba radhi?

Ukwendeeee alaaaa!!!

Huyo jamaa ni kilaza sana na aojiwe, uwenda ni kibaraka wa Hitler Kagame. Si tunakumbuka lile pandikizi la Israel nchini Syria!?. Achunguzwe mwenendo wake kama ni msaliti wa nchi hii
 
Kimsingi sidhani km huyo ni mtz au anataka kujua zaidi. Pia hana details za kutosha na kiswahili chake cha kubambanya.

Katika mjadala wa katiba hii tuliangalie kuhusu wasaliti wa nchi hii, kwa kuongwa Pesa au maslai binafsi. Tuweke adhabu ya kifungo kirefu gerezani, ushaidi huwe mambo kama Haya. Tusitake ushaidi mwiiiiiiingi, kama huu tu unatosha wa kumsapoti adui wa nchi hii.
 
tanzania ni nchi isiotishwa na mtu yoyote.kama tumeweza kumchana live mu izrael kwamba mambo anayoyafanya dhidi ya palestina sio.na tulimshuri mbele ya baraza la usalama kwamba arejee mikataba 1969.na hadi leo atujamuomba msamaha itakuwa kagame?.
kwanza mtoa mada ameshindwa kuandika fadhila za tz kwa wanyarwanda kipindi cha vita yao.
kwanza misaada mingi ya kibinadamu ilipita tz.
pili makambi ya wakimbizi yalikua tz
3.baraza la usuluhishi chini mw.nyerere kwa juhudi ya tz.
4.juhudi za yeye kupata uraisi zimetokea hapa.
hapo alipo anatuhuma za udikteta sisi tumenyamazia.
sasa muache ajidanganye mwiba unapoingilia ndipo utapotokea.
 
Mungu wangu weeee! we Albosignathus huna roho ya kibinadamu kabisaaa!!!!!!! Kagame ndo alisababisha waue wanawake, watoto, wehu, etc, eti kwasababu ni watutsi? We vipi? Unajihami kwa kuteketeza kizazi? Mauaji ya kimbari unayatetea kwasababu tu unatumia jina bandia? Kweli we una utu?
Wewe Kalisa kaa kimya wewe Mauaji ya kimbari yalisababishwa na Kagame na jeshi la serikali lilikuwa linajihami.Kagame ndio chanzo ya yote.
 
ndugu mzalendo vita vya kagera, kuna adhabu kubwa kwa wasaliti wotote, soma vitabu vya sharia. Ila usichanganye mjadala wa mambo ya kawaida na usaliti, utakuwa unawatisha watu ili wafikirie kama wewe
Katika mjadala wa katiba hii tuliangalie kuhusu wasaliti wa nchi hii, kwa kuongwa Pesa au maslai binafsi. Tuweke adhabu ya kifungo kirefu gerezani, ushaidi huwe mambo kama Haya. Tusitake ushaidi mwiiiiiiingi, kama huu tu unatosha wa kumsapoti adui wa nchi hii.
 
si nasikia Balangila ni ndugu zao watusi? we vipi Omulangi-la, mbona una jaziba na chuki dhidi ya ndugu zako, au we si omulangila, ni mzana?
Maziiku tayari Kagame amefanya uchokozi wa kutosha na Rais Kikwete Amekuwa mpole kupita kiasi. Wenyeji wa Kagera wanahujumiwa na Rpf sana. Wamejimilikisha kimabavu karibu pori lote linalounga wilaya ya Bk vijijini upande wa Izimbya kuelekea Burigi upande wa Muleba hadi Biharamulo kuzungukia Nyakahura hadi Ngara na kurudi Karagwe. 1. Wameyafanya mapori haya ya akiba mali yao wakihonga watendaji wa kata na madiwani katika vijiji vinavyozunguka mapori. Pesa ya kuhonga watendaji wa serkali wanaipata kwa kuteka na kuua raia na kuwanyang'anya mali zao. Sasa huyu Kagame ataendelea kutambanchini kwetu hadi lini? Hayo maendeleo unayodai yatafanyikia wapi? Bahati nzuri wananchi wa Rukoma- Izimbya juzi waliua askari 2 wa Rwanda waliokuwa na bunduki za kijeshi waliokuwa wamevamia mnada wa ng'ombe. Namuunga mkono rais Kikwete hawa watu warudishwe makwao kwa nguvu, na atakayeleta luneno anyolewe!!
 
JK kwa mara ya kwanza aliongea point kwa Rwanda,awaombe radhi kwa lipi?
stop bluffing and we called your bluff many days ago,.bring it on if you can.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom