Rais Kikwete awaombe radhi Wanyarwanda

Rais Kikwete awaombe radhi Wanyarwanda

Status
Not open for further replies.
Kwa hili tuko pamoja na rais Kikwete, kama hao FLDR wameendelea na vita vya muda mrefu dhidi ya Wakongo na hata Rwanda yenyewe, Kikwete alikua sahihi kutoa ushauri ule, hapa cha muhimu ni hiki, jaribuni kutekeleza kile rais wenu alicho kisema, tutashughulika na nyie, kwanza ni watu wa ajabu sijapata kuona, hamna shukurani kabisa, tumewahifadhi bure kwa muda mrefu hapa nchini wakati kwenu kukiwa na vita halafu leo eti mnakuja na koropoka, JWTZ ipo tayari kwa kazi, hizi zote mnaleta mara baada ya kubanywa kule Goma na wizi wenu mliokua mkiendelea nao huko ma madini ya Almasi na Dhahabu. Narudia, kwa hili tutabaki kama Watanzania na sio CDM na ccm!
 
Msamaha wa nin? Kwalip hasa? Kwani Rwanda wanatakaje? Eebu wajaribu afu wata isoma # ka c kuiandika looo!!!!!!??????
 
Japo JK ana mapungufu yake nchini kwetu lakini kwa hilo suala la FDLR yupo sahihi kabisa wala hakuna haja ya kuomba msamaha, nipo nasoma na wanyarwanda hapa chuoni kwetu ambao nao ni watusi kwa upande wao wanaona JK alikuwa sahihi kama mm ninavyoona, yeye alitoa ushauri M7 akakubali na Kagame kama hataki alitakiwa akatae basi wala si kuleta visa vyake, Kagame bado analeta chuki yake ya kikwete kumhifadhi Karegeya na ndo maana Kagame hawaivi hata na Zuma kwa sababu ya kumhifadhi Nyamwasa.

Je unajua baadhi ya majenerali wa FDLR Walirudi na wameingizwa kwenye jeshi la Ruanda? Je unajua kuwa mkuu wa magereza wa sasa Rwanda alikuwa FDLR? je kwanini awakubali baadhi then akatae kuongea nao hao wote. kagame ameifanya Rwanda kama mali yake pekee yake na watusi na kuwatenga wahutu anatumia dhana ya genocide kukandamiza wahutu.

JK simamia ukweli tunakuunga mkono katika hili
 
Umejitahidi kuandika kiswahili kizuri, sidhani kama kuna mnyarwadi anayeweza kuandika kiswahili kizuri namna hii au ndo matunda ya elimu yetu uliyofaidi bure toka sekondari hadi chuo kikuu wakati wewe ni mnyarwanda? Usimfundishe Rais wa Tanzania nani amuombe msamaha.

Hahaha...
 
Yatasemwa mengi sana lakini mwisho wa siku either M23 waweke silaha chini na ku-disarm, wacongo wabaki Congo, wanyarwanda warudi kwao; au wasubiri wapate kichapo hadi watimkie Rwanda then tuwafuate hukohuko. Tayari wameshapewa 48 hours waweke silaha chini la sivyo wasubiri kichapo......UN gives DR Congo rebels 48 hours to disarm | Fox News
 
hakuna cha kuomba radhi hapa KAGAME hatoshi hata kwenye kiganja!! na isitoshe kwanza ni jambazi wa madini ya DRC- huko KIVU. Binafsi sioni kabisa kosa la LUTENI KIKWETE.
 
George, nashindwa kuamini kwamba JK aliongea hilo jambo mbele ya Mkutano ule kabla ya kuongea na P Kagame faragha. Kuna uwezekano mkubwa sana kwamba JK na Mamlaka za Tanzania walishaongea sana faraghani na mamlaka za Rwanda kuhusu hilo na mamlaka za Rwanda zikakataa pendekezo hilo huko huko faraghani ndio maana JK kaamua kulibwaga pendekezo hilo mkutanoni.

JK na mamlaka za TZ hawawezi kukosa ustaarabu kama huu. Haiwezekani. Dhahabu na Urani za DRC ni tamu sana kwa Kagame!

wewe unaona dhahabu za congo!!! kama JK ana uchungu na rasilimali za congo inakuwaje zetu ndo anagawa kawa pipi.. in short the man is real an intention seeker that only what i can see on him but even with his weakness never absolve Rwanda from all allegation from international community, the best thing is to handle everything in diplomatic way..
 
Ndugu yangu, kosa la Rais Kikwete ni lipi? Hivi kumwambia Rais Kagame azungumze na wabaya wake ili amani itamalaki Rwanda na ukanda huu wote ni kosa la kumshurutisha Rais wetu aombe raidhi? Aombe radhi kwa lipi?

Fikiria, ni kama wewe leo umwambie Rais Kikwete aketi na Chadema wamalize tofauti zao. Je, ni haki Rais Kikwete au Freeman Mbowe kuudhika? Je, watokee watu humu wakushurutishe uombe radhi kwa kauli yako, utakubali?

ndiyo maana nasema, Rais Kikwete ni rais wetu. Linapokuja suala la nchi na nchi, lazima tusimame upande wa Rais wetu hata kama wapo Watanzania wasiompenda. Suala la nchi lazima ushabiki wenu uwe mmoja. Hivi ninavyoandika majibu haya nasikiliza Redio DW ikitangaza kwamba Rais Obama kawatuma maseneta wawili, akiwamo John McCain (wote wa Republican) kwenda Misri kuhakikisha amani inarejea. Obama kafanya hivyo kwa manufaa ya Marekani. Linapokuja suala la nchi, Chadema, CCM, UDP, TLP na wasio na chama sote tunapaswa kuwa kitu kimoja. Rais wetu hawezi kutukanwa halafu tukashangilia. Tukishangilia, tutaonekana mazuzu mbele ya jumuiya ya kimataifa.

Naandika haya kwa kuwa naamini katika matumizi ya diplomasia ya mazungumzo kuelekea upatanishi wa amani ya kweli. Vita ni njia pekee ya mwisho katika kutafuta ufumbuzi wa mgogoro...kama tulivyofanya kwa Uganda ya Idd Amin.

.....kosa la Rais Kikwete ni lipi?

Nina imani kabisa, mkuu, alikuwa anajua serikali ya Rwanda ilikuwa imeanzisha utaratibu wa maridhiano kati ya wahanga wa mauaji ya kimbari mara tu baada ya hali ya amani kutengemaa kiasi nchini humo. Rejea taarifa hizi hapa chini

Background Information on the Justice and Reconciliation Process in Rwanda - Outreach Programme on the Rwanda Genocide and the United Nations

Rwanda’s Gacaca courts: a mixed legacy -- New Internationalist

Mbali na mapungufu machache kulinganisha na faida nyingi za utaratibu huu wa maridhiano ulioanzishwa na serikali ya Rwanda, bado FDRL hawakuonyesha nia ya dhati kushiriki katika utaratibu huu ili waijenge Rwanda ya wamoja.

Kwa kuzingatia haya, mkuu wetu, angeanza kuishauri serikali ya Rwanda irudishe utaratibu wa maridhiano wa Gacaca ambao iliufunga mwaka jana (2012) pia angewashauri FDRL wajumuhike katika mpango wa maridhiano ulioandaliwa na wanyarwanda kupitia serikali iliyopo madarakani nchini humo huku akiwa amehakikishiwa na Kigali kuwa itarudisha Gacaca. Kupitia ushauri huu nadhani maridhiano yangefikiwa kati ya Kigali na FDRL.

Mkuu wetu kuanza kutoa ushauri "alioutoa" huku akipuuza utaratibu ulikuwa imeanzishwa na Wanyarwanda ili waponyeshe vidonda vya mauaji ya kimbari, kwa maoni yangu, mkuu aliteleza ila hakuangua. Kwa maana hiyo anayonafasi kuangalia namna ya kurekebisha hili.

......Suala la nchi lazima ushabiki wenu uwe mmoja.

...Nakubaliana 100% na wewe katika hili. Hata hivyo, tunapokuwa upande mmoja na rais haimaniishi kuwa haturuhusiwi kutoa ushauri kwake ni upande upi atuongoze tusimame naye. Na ninaimani sote tutakuwa na furaha tutakapo simama upande mmoja na rais mahali ambapo huko mbeleni hatutamlaumu...kuwa alituchagulia upande wenye madhara kwa afya ya nchi yetu. Mwanzisha uzi huu katimiza wajibu wake katika hili. Mwanzisha mada anataka tusimame na rahisi mahali pa salama na majirani zetu. Uungwana ni kujua udhaifu wako ...na hapo unaufanyia kazi kuurekebisha udhaifu huo. Si maanishi kuwa lazima tuiombe radhi Kigali lakini tunaweza kutuma "envoy" Kigali kulizungumzia suala hili...najua tunaweza kuunda envoy ambayo inaweza kusimamia hili kama tunavyounda tume mbalimbali yanapotokea majanga.

...Rais wetu hawezi kutukanwa halafu tukashangilia. Tukishangilia...

Envoy tutakayoituma Kigali inaweza kulishughulikia hili pia...wanyarwanda wanaweza nao wakaona umuhimu wa kufuta kauli zao dhidi ya Rais wetu kwa namna ambayo sisi tutaonyesha kujali juhudi zao za kuleta maridhiano nchini mwao. Binafsi sishangilii kutukanwa Rais....au mtu yeyote mwenye nia njema na mwenzake. Kama nilivyoeleza mwanzo,mkuu wetu, ameteleza ila hajaanguka...hivyo tumshauri namna ya kutembea upande wa utelezi ili asiteleze tena na hatimaye kuanguka nasi tukaanguka pamoja naye.

......mazuzu mbele ya jumuiya ya kimataifa

Ukiona jumuiya yoyote ya kimataifa inakona zuzu wakati wewe unaangaika kuleta maridhiano kati ya wale wanaohasimiana au unaamulia ugomvi kwa wanoupigana. Basi ujue jumuiya hiyo ni "JUMUIYA YA KISHETANI" wala usiisikilize.
 
Wewe George Maziku una akili kweli? Mimi ni mchungaji ila .....,wewe Yuda Iskariot mtoto wa malaya.
Mchungaji punguza hasira ueleweke....

Mimi sioni tatizo la mleta mada, ushauri wa George na ule wa JK hauna tofauti kubwa, Kikwete anashauri Kagame akutane na waasi FDLR George naye anashauri Kikwete akutane na Kagame waombane msamaha yaishe kiutu uzima so what is the difference, kwanini ushauri wa mwingine uonekane mbaya?

Kuomba radhi kwa mtu mzima ni kuonyesha usitaarabu na ukomavu hata kama wewe ndiye uliyekosewa, radhi huepusha shari kinyume chake ni kujenga uhasama.
 
Hata kama hammpendi Rais Kikwete, nasema kwa hili hana sababu ya kuomba radhi. Aombe ili iweje? JK watuachie sisi wenyewe tutofautiane naye huku, linapokuja suala la nchi, msimamo wetu ni mmoja-kuungana! Tusikubali kwa namna yoyote kuruhusu nguvu za nje kutuvuruga hata kama Rais wetu wengine humu ndani hawampendi.

Manyerere, may be you are right in what you have highlighted lakini my question can you from the better part of the bottom of your heart claim that Tanzanians are united? Inanipa tabu kuwa Watanzania tuko united wakati watu au niwe wazi Wanasiasa na Viongozi wa dini mchana kweupe wanasimama wanahubiri udini.

Tumesikia kuwa akiuawa muumini huyu na nyie Karidinali, Askofu, padre, mchungani orodha ni ndefu ni halali yetu. Halafu tukio lililosababisha muungwana huyu-Ilunga kusema hayo was his reaction to the killing of Sheik in Mombasa. Neither police nor any security organs put this Ilunga into gallows. He's walking majestic. Tumesikia mchaana wa jua la utosi wanasiasa wakisema kuwa CDM chama cha Kaskazini, cha Wachagga, kampuni ya familia na ni viongozi waandamizi wa serikali na CCM lakini hatujawahi kusikia watu wanasema tuungane tuwalaani maana wanataka kusababisha machafuko.

Tumesikia watu wanasema CDM ni chama cha kigaidi kama ambavyo waliwahi kufanya kwa CUF. Leo hatujaombwa kama Taifa tuungane kuwalaani. Na cha ajabu zipo taasisi ambazo zimetoa usajiri wa vyama hivi na zinatumia kodi ya wananchi na hazijawahi kukanusha na kusaidia kuleta moyo wa mshikamo japo hitikadi ni tofauti. Twende kwenye socializing bodies kama shule na vyuo ambavyo vilikuwa ni incubators za umoja, mshikamo, udungu na uzalendo.

Hivi leo vimekuwa ndio vyanzo vya mmomonyoko wa nilichokitaja. Kama kuna motto toka chekechea anasafiri kwa basi kwenda shule au ndege na shule zina kila aina ya vitendea kazi na akimaliza kwa kuwa wazazi wako kwenye system au ni wakurugenzi wa makapuni makubwa ile networking inamfanya asisote akitafuta kazi. Je, kuna siku yule wa St.Kayumba na shule za kata, chuo cha kuakariri, kudesa na kujiripua na atoke pale asage rami akitafuta kazi, atweza kukaa meza moja na yule niliyemtaja awali?

Ukisema ndio ni kujidanganya maana tunaishi Tanzania hii na tumeona kuwa hakuna utangamamno hata kidogo. Yesu Kristo aliwa kwenye mateso alisema jililieni nyie na wanenu. Jamani wahamasishe Watanzania walilie haya na mengine yanayopelekea erosion of social fabric kuliko hili la kauli ya Kagame maana huko kwenye periphery hawayajui. Kama tusipofanya hivyo kauli za kina Kagame nyingi zaja maana tutakuwa tunaji expose kwao
 
Huyu Marcopollo Wa tz Aombe Radhi Tu Wanyarwanda Kwa Kuingilia Mambo YasiyoMhusu, Akiendelea Kubisha, Kagame Mfanye Kama Juverinal Habyrimana..... Tungulia Mbali Huko Akafie Huko....shwain!
 
Ushauri wako si wa maana sana...

JK hana sababu yoyote ya kumuomba msamaha PK
 
Uli*ak** unyofol* kucha na meno...naogopa ban tu vinginevyo ningekukuporemeshea maneno ...

Wewe na wapuuzi wenzako endeleeni na upumbavu wenu
 
MWe, si Kagame ashaamua tuzichape? Sasa msamaha wa nini tena?
 
unatakiwa kufaham kwamba FDRL toka 1994 mpaka leo askari wake wengi ni vijana na 90% ya hao wala hawakuwai kushiriki hiyo genocide walikua bado wadogo ni viongozi wao tu kwa iyo acha kupoteza uma kua FDRL wote walishiriki genocide??? mbona huongelei second congo war iliyoua watu wengi kuliko iyo rwanda genocide ambae huyo kagame ni mmoja wa wahalifu pia!!! acha porojo!!!!
 
Hizi jazba za baadhi ya wachangiaji ndio kama zile alizokua nazo PK wakati alipopewa ushauri na JK kuna mtu anajiita pastor lakini amefunguka hadi koromeo lake limekauka anamuita G,maziku sani ofu ebichi duh?
 
I'm sorry to say, asiyewafahamu vizuri Wanyaranda ndiye atakaye weza kununua hili bandiko na kufanya kama mleta bandiko anavyopenda.

Wanyarwanda ni vinyonga na kwa ukinyonga wao, kwa sasa wameishaifanya EAC kuwa talking shop.

Siwezi kushangaa kama mleta mada atakuwa ni wale wale au ameishawezeshwa ili kupata nguvu za spinning kwenye international politics.

Relax, mbona mnatumia nguvu nyingi kujibu sentesi moja ya Rais Kikwete, au ndiyo yale yale ya guilty conscience kuwasumbua.
 
Mleta mada naona haujielewi, hivi mkulu wa kaya aombe radhi kitu gani wakati ule ulikuwa ni ushauri tu tena uliotolewa katika sehemu tunayoweza kusema kuwa ilikuwa ni "neutral arena , yaani kwenye mkutano wa marais wa Afrika, yaani ni kama ukiwa kwenye baraza la UN unaruhusiwa kutoa duku duku lako hata kwa USA, German, France, China au nchi yeyote kama unaona kuna ulazima wa kufanya hivyo , na ndio maana hata babu Mugabe huwa anaenda UN na kushusha nondo zake (msimamo wake ) dhidi ya vikwazo vya marekani na washirika wake dhidi ya nchi yake bila bughdha yoyote licha ya kuwa harusiwi kutia maguumaeneo ya mnene wa dunia "USA". so kikwete alikuwa sahihi kusema alichosema mbele ya wajumbe , labda angeliteta teta pembeni ingekuwa majanga.
 
Umeeleza vizuri sana ingawa umeshindwa kuchanganua ni kwa nini Kagame akasirike wakati ushauri uliotolewa na Kikwete ilikuwa ni taarifa ya walichokuwa wamejadili kabla M7 hajafika. Kwa nini Kagame hakutaka kuona kuwa Kikwete ali-amplify ushauri wa kikao na sio maoni binafsi. Inaelekea Rwanda wana tatizo jingine na Kikwete tofauti na hili waliloamua kukomaa nalo. Hebu tazama andiko kwenye gazeti lao ili uone weakness katika argument zenu na raisi wenu huko Rwanda:Understanding President Kikwete
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom