Rais Kikwete awaombe radhi Wanyarwanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete awaombe radhi Wanyarwanda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Jul 31, 2013.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2013
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,239
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  KUNA msuguano wa waziwazi unaoendelea kati ya Tanzania na Rwanda kufuatia ushauri wa Rais Jakaya Kikwete kwa mwenzake Paul Kagame, kumtaka akae na kuzungumza na waasi wa FDLR.


  Msuguano huo ulianza muda mfupi tu baada ya kumalizika kwa kikao cha viongozi wa nchi za Maziwa Makuu kilichofanyika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) na kuhudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, chini ya uenyekiti wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.


  Rais Kikwete alimtaarifu Rais Museveni kile walichojadili baada ya yeye kuchelewa kufika. Alisema ni vema serikali za Rwanda na Uganda zikakaa na kuzungumza na makundi ya waasi wa nchi zao, na kulitolea mfano kundi la waasi wa Rwanda la FDLR.


  Inasemekana ushauri huo uliungwa mkono na Rais Museveni, lakini ulipingwa vikali na Serikali ya Kigali, na tangu wakati huo hadi sasa yamesikika matamshi ya ubabe kutoka kila upande.


  Alhamisi wiki hii, Tanzania kupitia kwa Ofisa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mkumbwa Ally, imetoa onyo kwa Kigali kuwa wasithubutu kuanzisha vita dhidi ya Tanzania kwa kuwa kitendo hicho kitajibiwa vikali.


  Onyo hilo la Dar es Salaam limekuja kutokana na kauli ya vitisho inayodaiwa kutolewa na Rais Kagame hivi karibuni mjini Kigali kwamba: “Sitapoteza muda wangu kumjibu Kikwete, inajulikana maana kuna mahali hataweza kuvuka…haiwezekani.”


  Kwanza lazima nikiri kuwa ushauri huo wa Rais Kikwete ni mzuri kutokana na dhamira njema iliyobeba ushauri huo. Dhamira inayolenga kuyapatia ufumbuzi wa kudumu matatizo ya kiusalama yanayozikabili nchi za Rwanda, Uganda na DRC kwa miongo kadhaa sasa.


  Hata hivyo, ushauri huu haukuwa sahihi na haukutolewa mahali sahihi. Haukuwa sahihi kwa sababu haukuzingatia ukweli na mtazamo wa Kigali juu ya kundi la waasi la FDLR.


  Kundi la FDLR linaundwa na wanamgambo wa Interahamwe na wanajeshi wa zamani wa jeshi la nchi hiyo chini ya aliyekuwa Rais wa Rwanda hayati Juvenal Habyarimana anayedaiwa kuuawa na vikosi vya Rwandese Patriotic Front vya Rais Kagame mwaka 1994 wakati akitokea Tanzania kwenye mazungumzo ya amani kati ya serikali yake na Kagame.


  Interahamwe na lililokuwa jeshi la Habyarimana ndio waliotekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani wa Rwanda mwaka 1994. Waliposhindwa vita mwaka 1994 dhidi ya vikosi vya Rais Kagame, walikimbilia katika misitu ya DRC iliyo mashariki mwa nchi hiyo na kuunda kundi hilo la FDLR.


  Rais Kagame na mamilioni ya wananchi wa Rwanda wa kabila la Watutsi na Wahutu wachache wenye msimamo wa wastani, ni waathirika wakubwa wa ukatili na unyama uliofanywa na FDLR, na bila shaka hawajasahau wala kusamehe.


  Rais Kikwete alipaswa kuzingatia ukweli huu kabla ya kuamua kutoa ushauri wake. Kama angezingatia ukweli huu kabla, bila shaka asingethubutu kumshauri Rais Kagame kukaa meza moja na kundi ambalo halijawahi kuomba msamaha kwa Wanyarwanda wala kuonyesha kujutia uovu wao.


  Halafu Rais Kikwete alikosea kutoa ushauri huo mbele ya mkutano ule. Hapakuwa mahali sahihi kwa jambo zito kama hilo. Angetafuta nafasi nyingine, na kwa maoni yangu angezungumza na marais wenzake kwa faragha, ama wote kwa pamoja au mmoja mmoja.


  Angepata nafasi nzuri zaidi ya kufafanua dhamira ya ushauri wake, na pia angeweza kuona mwitikio wa Rais Kagame juu ya ushauri huo. Ninaamini msuguano wa sasa usingekuwepo kwa sababu wangejadiliana kwa kina na kuyamaliza mambo yote katika chumba kilichofungwa milango.


  Sasa ushauri unataka kuzaa vita ya majirani wawili wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Bila shaka madhara yake ni makubwa. Mbali na kusababisha kuharibika kwa mahusiano kati ya nchi hizi, pia zitapoteza maisha ya watu wake na rasilimali, na hivyo kuteteresha uchumi wa kila moja.


  Ni imani yangu Watanzania wengi hawataki na hawawezi kuunga mkono uamuzi wa kuingia vitani na Rwanda. Watanzania hawapo tayari kwa vita vingine, baada ya vile vya Uganda vya mwaka 1978. Tunataka kujenga nchi yetu kiuchumi, kisiasa na kijamii kukimbizana na wakati kwa sababu tupo nyuma sana.


  Namshauri Rais Kikwete awaombe radhi Wanyarwanda, amuombe radhi Rais Kagame. Ampigie simu amwambie yaishe kwa kuwa hakukusudia kumuudhi wala kumkumbusha machungu ya unyama wa Interahamwe, amwalike Dar es Salaam wanywe chai na mnyinyo.


  Na George Maziku
  0659985064
   
 2. N

  Nyabhurebheka Member

  #2
  Jul 31, 2013
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Umejitahidi kuandika kiswahili kizuri, sidhani kama kuna mnyarwadi anayeweza kuandika kiswahili kizuri namna hii au ndo matunda ya elimu yetu uliyofaidi bure toka sekondari hadi chuo kikuu wakati wewe ni mnyarwanda? Usimfundishe Rais wa Tanzania nani amuombe msamaha.
   
 3. M

  Manyerere Jackton Verified User

  #3
  Jul 31, 2013
  Joined: Dec 11, 2012
  Messages: 2,354
  Likes Received: 661
  Trophy Points: 280
  Hata kama hammpendi Rais Kikwete, nasema kwa hili hana sababu ya kuomba radhi. Aombe ili iweje? JK watuachie sisi wenyewe tutofautiane naye huku, linapokuja suala la nchi, msimamo wetu ni mmoja-kuungana! Tusikubali kwa namna yoyote kuruhusu nguvu za nje kutuvuruga hata kama Rais wetu wengine humu ndani hawampendi.
   
 4. bwafo

  bwafo Senior Member

  #4
  Jul 31, 2013
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Mwambie Kagame aongee na FDLR. Hataki aache, Period!
   
 5. Prishaz

  Prishaz JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2013
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,889
  Likes Received: 1,376
  Trophy Points: 280
  Kagame aombwe msamaha kwa lipi! Kuambiwa uweli?
   
 6. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2013
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,556
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  umeongea kidiplomasia saana, mi naona kuna logic, ukimwambia mtu kitu asipopendezwa nacho, huna budi kumuomba ladhi, i can see the logic behind, manaake ninachoona ni mpambano usio na tija kwa pande zote mbili!
   
 7. M

  Master plan JF-Expert Member

  #7
  Jul 31, 2013
  Joined: Dec 24, 2012
  Messages: 2,859
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Msimuhukumu mleta uzi hii habari nimeisoma tangu sa 11 asbh kwenye gazeti la Tanzania daima
   
 8. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #8
  Jul 31, 2013
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,896
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Vita haina macho, mi sitopigana vita! Huu ni upuuzi. Mpelekeni Ridhwan. JK kayataka mwenyewe
   
 9. R

  Rapture Man JF-Expert Member

  #9
  Jul 31, 2013
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  George, nashindwa kuamini kwamba JK aliongea hilo jambo mbele ya Mkutano ule kabla ya kuongea na P Kagame faragha. Kuna uwezekano mkubwa sana kwamba JK na Mamlaka za Tanzania walishaongea sana faraghani na mamlaka za Rwanda kuhusu hilo na mamlaka za Rwanda zikakataa pendekezo hilo huko huko faraghani ndio maana JK kaamua kulibwaga pendekezo hilo mkutanoni.

  JK na mamlaka za TZ hawawezi kukosa ustaarabu kama huu. Haiwezekani. Dhahabu na Urani za DRC ni tamu sana kwa Kagame!
   
 10. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #10
  Jul 31, 2013
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,109
  Likes Received: 3,567
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha EasyFit Kikwete aombe msamaha kwa kipi ?.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. M

  Mwananchi JF-Expert Member

  #11
  Jul 31, 2013
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 2,097
  Likes Received: 771
  Trophy Points: 280
  Japo kumejitahidi kuandika na kutueleza kuwa Kagame na RPF wake walihusika kumwua Rais Habyarimana, umekosea kusema kuwa Rais Kikwete anapaswa kuomba radhi kwa Kagame.
  Aombe radhi kwa kosa gani, kushauri rafiki yako apatane na adui wake ni kosa? Unaopaswa kuelewa kuwa pamoja na Rais Kagame (RPF) kuhusika kumwua Habyarimana mpaka leo hajawahi kuomba radhi au kushitakiwa kwa kosa ambalo ndilo lilikuwa chanzo cha mauaji ya kimbali. Maana mauaji hayo yalikuwa triggered na kifo cha Habyarimana ndio visa vya kulipiza kisasi vilianza.
  Kilichofanyika katika Mahakama ya ICTR ilikuwa ni kukamata wahusika wakuu na kuwahukumu kwa kutumia sheria ya kimataifa ya Command responsibility, kwa maana anafungwa kiongozi aliyehusika kutoa amri na si jeshi zima la watu wadogo wenye kufuata amri tu. Mpango mzima wa Carla de Ponte ulikuwa baada ya Wahutu na Watsu waliohusika kwenye mauaji washitakiwe, lakini Kagame kama kipenzi cha Marekani walishinikiza mpaka yule mama akaondolewa kwenye madaraka ya Mwendesha Mashitaka. Tango hapo Watsi wamepita bila kushitakiwa japo nao ni wahusika.
  Kikwete kama mmoja wa wahusika wakuu katika ukanda wa maziwa alikuwa sahihi kutoa ushauri huo na sioni kwa nini Kagame awakatae Wanyarwanda wenzie na kuwafanya waishie kukaa Congo ukimbinzini hali yeye alipigana kurudi Rwanda kwa mtutu wa bunduki na hapa anashauriwa kupatana kwa njia ya manai na si mtutu? Ebu Maziku funguka acha kutumia kalamu kukwepa wajibu wa kuelimisha jamii kwa sababu za itikadi zako za kupendelea Watsi. FDLR nao wana haki ya kusihi nyumbani kwao, na unapaswa kujua kwamba demokrasi ya kweli inatakiwa nchini Rwanda na siyio kukamata maadui wako kisa wanataka haki sawa kwa kisingizio cha Genocide.
  Mpaka sasa nashangaa Watsi bado kila mwaka wanakumbuka mauaji ya Kimbari badala ya kusika tofauti yao na kusahau. Kama ni hivyo sasa Gacaca yaani mahakama ya reconciliation ilikuwa ya nini kama siyo kuzika tofauti?
   
 12. t

  thatha JF-Expert Member

  #12
  Jul 31, 2013
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 177
  Trophy Points: 160
  warwanda wajinga sana mnataka kuombwa radhi kwa kipi kaeni na ujinga wenu tena mda siyo mrefu mtapgwa na umoja wa mataifa .
   
 13. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #13
  Jul 31, 2013
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,001
  Likes Received: 1,212
  Trophy Points: 280
  We jamaa mweupeeE,
  Nenda wakakufundishe tena kuandika.
   
 14. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #14
  Jul 31, 2013
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,001
  Likes Received: 1,212
  Trophy Points: 280
  Tusi wewe? Au M23 ?
   
 15. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #15
  Jul 31, 2013
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Ningeshauri wewe uiombe radhi JF kwa bandiko hili linalomdhalilisha rais wetu.

  Ushauri wa JK aliuweka wazi kwenye mkutano uliokuwa wazi. Ushauri wake ulizingatia maslahi ya Tz kwani mapigano ndani ya DRC yana athiri amani mipakani mwa Tz. Sasa wewe ulitaka JK amwite Kagame falagha ili akamwambie madhara ya vita Tz? Kwa kuhofia nini?

  Kwenye post yako unajichanganya: kwanza unasema ushauri ulikuwa sahihi lakini unakuwa mnafiki kwa kutomshauri Kagame aufuate ushauri huo. Kinachosababisha vita DRC sasa sio ushauri wa JK na mahala alipoutolea bali ni kushindwa kwa Kagame kuwatambua maadui wake. Oops sio kushindwa kuwatambua bali nikukataa kuwatambua ili vita iendelee na m23 waendelee kupora almasi kwa manufaa ya Kagame.

  Mgogoro na vita vinaisha kwa makundi hasimu kukutana na kutambuana uwapo wao. Miaka 16 ya vita imepita kati ya Kagame na FDLR na hakuna mshindi. Ni lini Kagame atakubali njia nyingine ya kumaliza vita hii na nikwanini umoja wa mataifa wasijiridhishe kwamba vita hii inanufaisha Rwanda na ndio maana aiishi?

  All in all, labda ni Rwanda tu ambako mtoa ushauri uliosahihi anapaswa kuomba radhi. Mods muwe mnaziyeyusha mada kama hizi, mana zinaweza zitufanye members wengine tupige below the belt!!
   
 16. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #16
  Jul 31, 2013
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Muanzisha mada inabidi uiombe radhi JF kwa kuturudisha nyuma mambo ambayo tulishajadili hapa kwa undani, unataka kutupotezea muda kuyarudia. Kagame kapigana na FDLR kawashindwa, sasa ni lazima aongee nao! Katumia kisingizio cha FDLR kuiba mali za Congo na kuua raia, sasa kisingizio hicho sasa basi.
   
 17. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #17
  Jul 31, 2013
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,232
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Watu kama nyie ndiyo huwa mnawafumania wake zenu kisha unamwambia vaa twende nyumbani, unamwambia nimekusamehe lakini usirudie hata ajakuomba msamaha.
   
 18. nkasoukumu

  nkasoukumu JF-Expert Member

  #18
  Jul 31, 2013
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 676
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  kikwete ameongea mahala panapostahili, ile vita haipiganwi faragha kwa hiyo siyo kitu cha siri na sio siri kwamba kagame ni muhusika kikwete usimuombe radhi huyo mtu anaye ongoza mkoa, asdhanii mziki wetu ata uweza tuta wapiga, mpaka watafuniwe uji
   
 19. kbosho

  kbosho JF-Expert Member

  #19
  Jul 31, 2013
  Joined: Jun 4, 2012
  Messages: 12,489
  Likes Received: 3,268
  Trophy Points: 280
  rais wetu anamadhaifu mengi..ila kwa hilo hakukosea na wala awezi kuomba radhi kwa gaidi kagame.
   
 20. S

  Song Member

  #20
  Jul 31, 2013
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ukingalia kwa makini huo mtiririko wa matukio utakuja kuona hakukua na sababu ya Msingi kwa Raisi Kikwete kuongelea suala hili kwenye ule mkutano kama kweli nia yake ya dhati ni uondoaji wa tofauti ya serikali ya Rwanda na FDRL kwa njia ya mazungumzo! Mie naona angetumia principle hiyo hiyo anayo idvocate kuwasaidia ndugu zetu na majirani zetu Rwanda....ya kumuita Kagame kukaa naye chini na kuongea nae kirafiki kabisa...kwa sababu mwisho wa siku jukumu linabakia upande wa Kagame kufanya uamuzi wa kukubali kuongea na FDRL au la....najua lisingezaa matunda kwa kikao kimoja au viwili lakini huko mbeleni lingeweza kupewa nafasi ndani ya moyo wa Kagame....anyway halijaharibika kitu coz ata washauri wa Raisi wetu ni binadam wanakosea sometimes....kilichobaki ni Kikwete kujifanya -------- amwite Kagame au hata kama ni kuomba radhi ( which to me is the last option ) wakae, waondoe kwanza hili gape lililopo now la kutunishiana misuli, thn waangalie possibility nyingine ya kukaa na hawa ndugu zet FDRL kutatua migogoro yao! Hili jambo linawezekana ila lina garama kwa njia yoyote utakayotumia! Linaweza likatugarimu

  1.vita kati yetu na Rwanda na muendelezo wa vita kati ya Rwanda na FDRL ambapo hata ndugu zetu ( Watanzania na Warwanda wataathirika kwa kumwaga dam zao au hata athari za kisaikolojia na kiuchumi...kwa sababu vita inagarama kubwa ndugu zangu)

  2. Au kuonekana wajinga kwa kuomba msamaha na kukaa meza moja kirafiki na kutatua hili tatizo...kitu kitakachowasaidia Warwanda na Sisi pia

  I stand to be corrected ila katika maisha yangu mafupi niliyoishi nimeona option ya 2 inakuaga na mafanikio from individual level to the nation al large! Thnx guyz

  Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...