EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
Pichani Rais Kikwete akitembelea msikiti wa Sultani Qaboos Grand na pia akitia saini kwenye kitabu cha wageni.
Rais Kikwete ameendelea na ziara yake nchini Oman ambapo jana alitembelea msikiti wa Sultani Qaboos Grand ulioko Bausher, nchini Oman. Katika ziara hiyo, Rais Kikwete alipewa historia ya msikiti huo ambao unajumuisha chuo cha masomo ya Kiislamu, sehemu ya kufanyia mihadhara na sehemu nyinginezo.
Aidha Rais Kikwete alijionea mwenyewe usanifu wa jengo la msikiti wa Sultani Qaboos Grand uliojengwa kwa usanifu mzuri wa Kiarabu na Kiislamu.
Taarifa inaendelea kusema kuwa Rais Kikwete alijionea mwenyewe majukumu ya msikiti huo katika jamii na katika kufikisha ujumbe wa kuvumiliana kwa mujibu wa dini ya Kiislamu (President Kikwete familiarized himself with the role of the mosque in the society and in conveying the tolerant message of Islam).