Sala ya Jummah Msikiti wa Bwejuu

Shabani Ajaha

Member
Aug 18, 2021
78
60
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka Waumini wa Dini ya Kiislamu kuhimizana kujitokeza kwa wingi Agosti 23 kwa ajili ya kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ili isaidie kutekeleza mipango ya maendeleo ya nchi.

Amesema hayo leo baada ya Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Bwejuu uliopo Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja kabla ya mapumziko mafupi ya ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ya Mkoa huo ambayo imeanza 16 Julai.

IMG-20220722-WA0177.jpg
IMG-20220722-WA0152.jpg
 
Back
Top Bottom