Rais Kikwete atembelea msikiti wa Sultani Qaboos Grand Oman

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
1350503365044013000.jpg
1350503345024010900.jpg

Pichani Rais Kikwete akitembelea msikiti wa Sultani Qaboos Grand na pia akitia saini kwenye kitabu cha wageni.

Rais Kikwete ameendelea na ziara yake nchini Oman ambapo jana alitembelea msikiti wa Sultani Qaboos Grand ulioko Bausher, nchini Oman. Katika ziara hiyo, Rais Kikwete alipewa historia ya msikiti huo ambao unajumuisha chuo cha masomo ya Kiislamu, sehemu ya kufanyia mihadhara na sehemu nyinginezo.

Aidha Rais Kikwete alijionea mwenyewe usanifu wa jengo la msikiti wa Sultani Qaboos Grand uliojengwa kwa usanifu mzuri wa Kiarabu na Kiislamu.

Taarifa inaendelea kusema kuwa Rais Kikwete alijionea mwenyewe majukumu ya msikiti huo katika jamii na katika kufikisha ujumbe wa kuvumiliana kwa mujibu wa dini ya Kiislamu (President Kikwete familiarized himself with the role of the mosque in the society and in conveying the tolerant message of Islam).
 
Ukiondoa kujionyesha wakati wa sikukuu hivi kweli Kikwete huswali au ni funga kamba? Namuona kama mjanja mjanja anayeutumia uislam kupata sympathy anapokuwa amezidiwa.

Nilipokuwa nasoma comment yako hii, nilimaliza then nikahisi kama sijakuelewa, nikairudia mara ya pili kuisoma. Nilipomaliza nikajikuta nacheka sanaaaaa kisha nikaamua kukupa LIKE
 
Jamaa wana misikiti misafi! hakuna mikeka! Halafu wenzenu wanaingia na viatu misikiti! safi sana! Sheikh ponda na kundi lake wapelekwe wakajifunze uislam wa kisasa! JK yuko msikitini akiwa amepiga suti kali! mjeshi wake nae kaingia msikitini.
Huu ndio uislam! Haya ndio mambo ya kuiga! very interesting!
 
Mzee huo msikiti sio kama wanaingia na viatu hapo ni lango kuu la kuingilia tu, ila ndani ya msikiti lazima kuvua viatu, huu msikiti sana umewekwa kwa maonyesho zaidi maana muda mwingi ukienda utakuta watalii nje wanapiga mapicha na ni mkubwa sana sehem ya kuswalia ipo ndani sana, ila hapa chakujifunza pamoja na watalii wengi kuja kupiga picha lakini waislam hawawadhuru
 
Nipo sehemu ambapo inshu siyo dini, inshu kubwa ni utaifa! ukienda mskitini utakutana na wanafunzi na wananchi wengi wanaotembelea msikitini kwa nia ya kujifunza na wanaruhusiwa kuingia hadi ndani kuangalia watu wanavyoswali. Hakuna vurugu za kibongo bongo, hivyo hivyo ukienda kanisani watu wanatembelea na kuuliza nini kinchoendelea. Pamoja na hayo, kuna baadhi ya makanisa yanawagawia hadi pesa waumini kuwashawishi. But all in all, watu wanaheshimiana na suala kubwa ni utaifa, fanya mambo yako yoote lakini linapokuja suala la utaifa hakuna kuoneana aya.
 
Huyu jamaa kaenda kutalii kama kawaida badala ya kushughulikia matatiizo ya nchi yake. Huu ni ujinga

Huu ndio upuuzi tunao ukataa' sasa ulitaka kikwete huko alipo atembee analia ndio utajua anawajali wa tz? Ina maana huko tz nchi imestop kwa kila kitu kisa makanisa kuchomwa? Hizo chuki zingine hazina maana kabisa
 
Mzee huo msikiti sio kama wanaingia na viatu hapo ni lango kuu la kuingilia tu, ila ndani ya msikiti lazima kuvua viatu, huu msikiti sana umewekwa kwa maonyesho zaidi maana muda mwingi ukienda utakuta watalii nje wanapiga mapicha na ni mkubwa sana sehem ya kuswalia ipo ndani sana, ila hapa chakujifunza pamoja na watalii wengi kuja kupiga picha lakini waislam hawawadhuru
Hapa kwetu ukijaribu kupiga picha Msikiti wowote wakikukuta lazima makanisa matatu yateketee Kama sio kukuchinja na jambia
 
Hapa kwetu ukijaribu kupiga picha Msikiti wowote wakikukuta lazima makanisa matatu yateketee Kama sio kukuchinja na jambia

Wewe badala ya kutumia JF kama shule unatumia JF kama uwanja wa mapambano dhini ya Uislam.
 
Haya JK.. hongera kwa kazi uliyofanya ya kutembelea msikiti huo. Ni muhimu sana kwa maendeleo yetu ...
 
Back
Top Bottom