Rais Kikwete arejea, Selasini na Hamad Rashid wampokea

Rais Kikwete arejea, Selasini na Hamad Rashid wampokea

only83

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Posts
5,342
Reaction score
2,528
Taarifa zinasema kuwa JK amereje muda si mrefu sana kutokea Marekani alikokuwa na ziara ndefu sana ya takribani wiki mbili..Maswali mengi kwa watanzania, nini hatima ya mswada wa marekebisho ya sheria ya katiba, na Je, CIVIL DISOBEDIENCE DAY itakuwaje?



attachment.php


Picha, JK akisalimiana na Mizengo Kayanza Peter Pinda na Ghalib Bilali leo uwanja wa ndege baada ya kurejea nyumbani.

attachment.php


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Rombo Mhe Joseph Selasini wakati alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2013 akitokea Marekani katika ziara ya kikazi. Wanaofuatia ni Mbunge wa Nkenge Mhe. Asumpta Mshama na Mbunge wa Wawi Mhe Hamad Rashid Mohamed
 

Attachments

  • jk.jpg
    jk.jpg
    32.7 KB · Views: 5,215
  • Kikwete-Airport.jpg
    Kikwete-Airport.jpg
    63 KB · Views: 5,847
kuna mtu kaota kwamba eti jk ameonekana akiongea na ' wazee ' wa Dar es salaam !
 
Mimi huu ujinga mpaka leo bado sijaulewa. Hivi kwa nini rais anaposafiri na kurejea nchini anasindikizwa na viongozi kibao wa serikali? Je, ni nidhamu ya uwoga au ni ujinga tu?
 
JK, CCM sio mama yako wala baba yako. Tanzania ni mama yako na baba yako pia. Tumia busara yako kuinusuru Tanzania. Mungu akupe busara na hekima katika kuchagua lililo jema kwa Tanzania. Na watu wote wenye mapenzi mema na Tanzania waseme Amina.
 
karibu home fastjet after long vasco dagamia.YOUR WARMLY WELCOME.
 
Salasini na Hamadi ni wabunge upande wa upinzani makini. Nadhani wanaelewa kuwa wenzao wanapotea njia. Na mburula humu ndani ambao hawakosi ila ni kula kulala hawajajua kuwa vyama vyao vimekosa mwelekeo na vimeanza kumeguka. Pumba nyie
 
Salasini na Hamadi ni wabunge upande wa upinzani makini. Nadhani wanaelewa kuwa wenzao wanapotea njia. Na mburula humu ndani ambao hawakosi ila ni kula kulala hawajajua kuwa vyama vyao vimekosa mwelekeo na vimeanza kumeguka. Pumba nyie

Hawana kazi za kufanya.

Ni jambo la ajabu Mbunge kuacha kazi zake na kwenda kufanya ujinga huu.Labda kama walikua Airport Muda huo lakini kwa mtu anayejali Muda hilo ni suala la kipuuzi
 
Baba karudi katoka kuhemea vibaba vya unga wakati nyumbani kwake kuna ardhi yenye rutuba, mito isiyokauka, misitu, madini - mpaka gesi! bandari.
Kuombaomba na uvivu ni tabia mbaya sana ya makabila ya pwani waliyodanganywa na waarabu.
Anatia aibu!
 
Napendekeza Ikulu ingengwe pale uwanja wandege ili asiwe anapata tabu kusafiri..
Wewe na wenzako endeleeni kupiga porojo.

Mbunge wa Rombo kupitia Chadema, Joseph Selasini anajua umuhimu wa Rais Kikwete.

Hongera Joseph Selasini kwa kuacha kazi zako na kwenda kumpokea Rais.
 
hawa wengine labda walikuwa wanasafiri ndo wakakutana airpot inamaana serikali iliwaomba akina rashid wakampokee raisi?
 
Uone watu walivyo wanafiki humu, mada ni JK apokelewa na HAMAD rashid na SELASINI, lakini angalia sasa wambea wanachokiandika humu, Hata hivyo kuna Tatizo gani Rais akipokelewa na hawa watu , si ni rais wao? tuache unafiki.
 
hawa wengine labda walikuwa wanasafiri ndo wakakutana airpot inamaana serikali iliwaomba akina rashid wakampokee raisi?

Hao ni watu makini katika siasa, Ningeshangaa kumuona SLAA, SUGU, MBOWE na LEMA.
 
lipi kati ya haya Ben ni jambo la kipuuzi kwenda kumpokea raisi wa nchi au kwenda kuwawekea wenzio sumu?

Teh teh teh teh teheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee. haa haa haaaa
 
Back
Top Bottom