Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 85,970
- 146,269
Sijui kwanini unawaamini viongozi wa Tanzania hadi uhalalishe matamshi yao kwa kutumia quotes zao. Wakati hao hao ni mabingwa wa kuchakachua hizo quote zenyewe na kutumia msemo maarufu 'Sikumaanisha hivyo, mmenielewa vibaya"
Bongo tambarare bwana...unasema mwenyewe afu unageuza habari. Hivyo ndivyo walivyosema, nasi baadhi yetu tuliwasikia.
Sasa kama kwetu viongozi ni wepesi wa kugeuza kauli, hili linaongeza kabisa umuhimu wa kuzinasa hizi kauli neno kwa neno, ili kesho wakitaka kuturuka tuweze kusema kauli yako hii hapa, umesema hivi na vile.
Tukizungumza kwa maneno jumla jumla bila direct quotes ndo hapo mtu anapokuja kuruka.
Kwa kutokutoa direct quote mnampa nafasi Tendwa aweze kujitetea "Mimi sikupiga marufuku maandamano na mikutano ya CHADEMA kwani hiyo ni haki yao ya kikatiba, ila nilikuwa nawahimiza kuhakikisha usalama wa wananchi unazingatiwa katika mikutano yao"
Kama hamtaki kumpa loopholes kama hizi inawabidi mrekodi vilivyo neno baada ya neno ili kesho akija kukanusha mmuonyeshe maneno halisi aliyosema.
Point yako inaongeza umuhimu wa kuwa na direct quotes, haipunguzi.