Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Ccm watoke tu ndo watajitafakari. La sivyo nchi hii msitegemee maendeleo. Ahadi zitakuwa zile zile miaka inaenda. Wakae pembeni wakajipange . nchi za africa bila mabadiliko nchi haipati maendeleo. Tujifunze kwa kenya.
 
Kashachelewa,jipu lishapasuka kilichobaki ni kulifuta tu hamna namna nyingine,jk umetuonyesha kuwa lowassa kisiasa kakupita sana,
 
Kwi kwi kwi kwi kwi, tehe tehe tehe tehe, mama weee mbavu zanguuuuuuuuuu1
 
Raisi wa nchi na amri jeshi mkuu anashindwa kumtaja waziwazi muhusika wa Richmond nae anaishia kutoa vijembe, hahahaha acha na mimi nicheke tena kwa sauti. Kweli Mnyika hakukosea alipomuita dhaifu
 
Yote haya yanafanyika ili neno litimie - Mabadiliko 2015 - Machozi ya wengi mwenyezi Mungu kayasikia.

kwa hiyo ndugu zangu hata hizi kauli ni mipango ya Mwenyezi Mungu, nyie subirini muone hiyo 25th jinsi kimbunga cha mabadiliko kitakavyovuma.
 
Raisi wa nchi na amri jeshi mkuu anashindwa kumtaja waziwazi muhusika wa Richmond nae anaishia kutoa vijembe, hahahaha acha na mimi nicheke tena kwa sauti. Kweli Mnyika hakukosea alipomuita dhaifu
JK ni mwerevu sana, kashapima upepo kashagundua merikebu yao inazama - keptain kashaachia usukani anavaa boya tayari kurukia MELI ya UHAKIKA - UKAWA
 
taasisi ya Urais imekuwa rahisi munoooo... yaani Mh Rais na institutions zote zilizo chini yake anashindwa kutoa hata evidence unachosema hata ka-bank account kinachoonesha transaction ya fedha za Richmond kwenda kwa EL miaka saba iliyopita? Enough with this lip service kura ccm haipati ng'o! maana mi ni lofa!
 
nimeandika jinsi kikwete alivyoisafisha njia ya lowasa...lakini mmechomekea ujumbe huu juu ya ule wa kikwete amtaja muhusika wa richond..kwa mfumo huu hata nyie mnashindwa kuaminika...na ni mara nyingi topiki zinageuzwa jamani wanaofanya hivi wanaishushia heshima jamii forum..chombo ambacho kimekubalika sana
 
JK ni kawaida yake kusema bila kutaja..
1. Akiwa Mbinga kwenye sherehe za jimbo alisema wauza madawa anayo list... HAKUMTAJA HATA MMOJA
2. JK alisema wezi wa banadri anawajuwa... HAKUMTAJA HATA MMOJA
3. JK waliosamehewa kwenye wizi wa EPA anawajuwa, hakumtaja hata mmoja na tena waziri mkuu Pinda alisema wakitajwa nchi itatetemeka

KWA HIYO HATA LEO HAWEZI KUMTAJA MTU KWA JINA KWAMBA NDIYE MUHUSIKA WA RICHMOND

Mkuu,atawataja vipi wakati main character katika hizi MOVIE ZOTE NI YEYE MWENYEWE?
 
Huyu jk ndo mlisema aliandaliwa na chama kuja kuliongoza taifa hili?na jk lazima chama limfie,sijui amejiandaaje maana baada ya uchaguzi ccm inafutika kwenye ramani,
 
ahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,kaka hii forumn imeshakuwa hacked by watu wa rangi ya kijani,hilo am the victim wa unachokisema mwenyewe,so nimeamua nitakuwa nachangia tu bila kupost any topic humu ndani
pole kaka
 
Rais Jakaya Kikwete amesema anashangazwa na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati mwenye Richmond yupo na anatembea naye mikoani.

Kikwete aliyasema hayo jana wakati akiwaaga wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika na kumtaka Lissu amtaje mwenye Richmond.
“Endapo Tundu Lissu atashindwa kumtaja mwenye Richmond, nitatoka hadharani na kumtaja mwenyewe,” alisema Kikwete.
Kabla ya mkutano huo, Rais Kikwete alifungua jengo la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF) ambalo limejengwa kwa Sh7 bilioni.
Akifungua jengo hilo, aliwaomba wawekezaji na mifuko ya kijamii kuiga mfano wa NSSF kwa kuwekeza katika sekta ya majengo kwa kuwa yanapendezesha mji.

Kadhalika, Rais Kikwete alizindua jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na nyumba 36 za bei nafuu zilizopo katika eneo la Mlole, Kigoma Mjini.

Richmond
Suala la Richmond imekuwa moja ya ajenda za CCM katika kampeni za urais hasa baada ya Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa aliyejiuzulu wadhifa huyo kwa kashfa hiyo kuhamia upinzani.

Kila sehemu ambako mgombea urais wa CCM anakwenda, suala hilo limekuwa likiibuliwa, huku Lowassa akisema yeye hakuhusika, bali alijiuzulu kuiokoa Serikali isianguke kwa kuwa ulikuwa uamuzi wa wakubwa.

Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amekuwa akienda mbali zaidi akisema akichaguliwa ataanzisha mahakama maalumu ya kushughulikia mafisadi wanaosababisha umaskini nchini.

Bashe ataka mahakama ya mafisadi mapema
Wakati Magufuli akiahidi mahakama hiyo, mgombea ubunge Jimbo la Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe alimtaka mgombea huyo jana kuiwahisha mapema iwezekanavyo akiingia Ikulu la sivyo atakuwa akihoji bungeni kila mara.

Bashe alisema akipatiwa ridhaa na wakazi wa jimbo hilo kuingia bungeni hatakuwa mbunge wa “ndiyo mzee” badala yake atakuwa akiisumbua Serikali mara kwa mara likiwamo suala la kudhibiti ufisadi nchini.

“Umesema utafungua mahakama ya mafisadi na majizi... nikuhakikishie waziri wako wa sheria utakayemteua ajue atakutana na mtu anaitwa Bashe, kila akiingia bungeni nitakuwa namuuliza kila mara upo wapi muswada wa sheria ya kuanzisha mahakama maalumu ya mafisadi na majizi,” alisema Bashe na kushangiliwa.

“Ni lazima tufike mahali Taifa hili tuache kuwa watu wa porojo....Taifa hili siyo maskini kuna wezi wapo bandarini. Najua saa hizi wanatafuta biashara nyingine.”

Mgombea huyo alisema wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea wa urais, kulikuwa na makundi ndani ya chama akiwamo na yeye lakini baada ya kumpata, Dk Magufuli tofauti zimekwisha.

Bashe alikuwa miongoni mwa vinara wa kumuunga mkono mgombea wa urais wa mwamvuli wa Ukawa kupitia Chadema, Edward Lowassa wakati akiomba ridhaa ya kuteuliwa na CCM kabla ya kuhamia upinzani.

Hata hivyo, jana alisema hataihama CCM kwa kuwa yeye na chama hicho hawakukutana barabarani na kwamba ni muumini wa mabadiliko ndani ya chama hicho.

Huku akigusia tuhuma zilizowahi kuvuma za yeye kuwaambia wananchi wamchague yeye halafu urais wampigie Lowassa, Bashe alisema wanaNzega watampigia kura Dk Magufuli asilimia zote na zikipungua hazitazidi asilimia tano.

Bulembo amvaa Sumaye
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo amemvaa Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye na kumtaka aache kuchukua mshahara na kurudisha walinzi wanaomlinda iwapo ataendelea kukitusi chama hicho kwamba hakijafanya chochote tangu uhuru.

Akiwahutubia wakazi wa Nzega jana, Bulembo alisema maisha yote ya kiongozi huyo na familia yake yametengenezwa na CCM lakini anashangaa kuona sasa anasimama kwenye majukwaa na kuwaeleza wananchi kuwa CCM haijafanya kitu.

“...Analipwa asilimia 80 ya mshahara wa Waziri Mkuu aliyepo madarakani, Mizengo Pinda. Mpaka leo bado ana ulinzi na anahudumiwa na Serikali hii. Kwa kupitia jukwaa hili la Nzega hebu Sumaye aache mshahara huo, arudishe walinzi awe raia kama sisi,” alisema Bulembo.
Aliendelea kurusha vijembe kwa kiongozi huyo akidai kuwa alinyang’anya ardhi ya wana ushirika wa Mvomero mkoani Morogoro baada ya kutetereka.

Magufuli na michango ya shule
Dk Magufuli jana aliendelea na kampeni zake mkoani Tabora na kuahidi kuwa akiingia madarakani atafuta michango yote shuleni inayosababisha baadhi ya wazazi washindwe kuwapeleka watoto shule.

Alisema anatambua kuwa baada ya sera yake ya elimu bure kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne kuanza kutekelezwa iwapo atachaguliwa, kuna baadhi watu wataanzisha michango isiyo na maana na kwamba atawashughulikia.

“Kuna mambo ya kuwaambia wazazi peleka dawati, peleka dawati na hata kama mtoto wa kwanza akishamaliza shule, ukimpeleka mwingine lile dawati hulikuti. Ninafahamu haya yote nitayashughulikia lakini pia, hakuna sababu shule kukosa madawati au viti wakati ipo karibu na miti, mbao zipo, haya yote tutaangalia tukizingatia masilahi ya walimu wetu,” alisema Dk Magufuli.

Akiwa Bukene wilayani Nzega, Dk Magufuli aliwatahadharisha makandarasi wazembe walioshindwa kukamilisha miradi yao kwa wakati akiwataka kufanya hivyo kabla ya Oktoba 25 kwa kuwa yeye ni kiboko yao.

Chanzo:
Mwananchi
Muhusika ni mliki na sio aliyehusika
 
Ila huyu bwana alishasema ana majina ya wauza madawa ya kulevya, waua tembo hadi leo hajayataja, ni kawaida yake, hana la kusema
 
Hili liko wazi...mtu anaweza kujiuliza, iweje mpaka leo (baada ya Lowassa kukimbia CCM) bado ana kigugumizi cha kuzungumzia mmiliki wa Richmond...kwa hali ya kawaida, huu ulipaswa kuwa muda wa kuweka kila kitu hadharani....

Mkuu hawezi kujitaja yeye mwenyewe
 
Back
Top Bottom