Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Wote bureee buree kabisa hao! Empty.Kikwete kama Rais alikuwa wapi mpaka Waziri mkuu afanye maamuzi makubwa hivyo; na alichukua hatua gani kama Rais au HATOSHIIII!!!;

Iweje amsukumie zigo Lissu kazi inayopashwa kufanywa na yeye; JK lianzishe mwanangu; ili tumwage ugali?!!


Wote
Rais Jakaya Kikwete amesema anashangazwa na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati mwenye Richmond yupo na anatembea naye mikoani.

Kikwete aliyasema hayo jana wakati akiwaaga wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika na kumtaka Lissu amtaje mwenye Richmond.
“Endapo Tundu Lissu atashindwa kumtaja mwenye Richmond, nitatoka hadharani na kumtaja mwenyewe,” alisema Kikwete.
Kabla ya mkutano huo, Rais Kikwete alifungua jengo la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF) ambalo limejengwa kwa Sh7 bilioni.
Akifungua jengo hilo, aliwaomba wawekezaji na mifuko ya kijamii kuiga mfano wa NSSF kwa kuwekeza katika sekta ya majengo kwa kuwa yanapendezesha mji.

Kadhalika, Rais Kikwete alizindua jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na nyumba 36 za bei nafuu zilizopo katika eneo la Mlole, Kigoma Mjini.

Richmond
Suala la Richmond imekuwa moja ya ajenda za CCM katika kampeni za urais hasa baada ya Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa aliyejiuzulu wadhifa huyo kwa kashfa hiyo kuhamia upinzani.

Kila sehemu ambako mgombea urais wa CCM anakwenda, suala hilo limekuwa likiibuliwa, huku Lowassa akisema yeye hakuhusika, bali alijiuzulu kuiokoa Serikali isianguke kwa kuwa ulikuwa uamuzi wa wakubwa.

Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amekuwa akienda mbali zaidi akisema akichaguliwa ataanzisha mahakama maalumu ya kushughulikia mafisadi wanaosababisha umaskini nchini.

Bashe ataka mahakama ya mafisadi mapema
Wakati Magufuli akiahidi mahakama hiyo, mgombea ubunge Jimbo la Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe alimtaka mgombea huyo jana kuiwahisha mapema iwezekanavyo akiingia Ikulu la sivyo atakuwa akihoji bungeni kila mara.

Bashe alisema akipatiwa ridhaa na wakazi wa jimbo hilo kuingia bungeni hatakuwa mbunge wa “ndiyo mzee” badala yake atakuwa akiisumbua Serikali mara kwa mara likiwamo suala la kudhibiti ufisadi nchini.

“Umesema utafungua mahakama ya mafisadi na majizi... nikuhakikishie waziri wako wa sheria utakayemteua ajue atakutana na mtu anaitwa Bashe, kila akiingia bungeni nitakuwa namuuliza kila mara upo wapi muswada wa sheria ya kuanzisha mahakama maalumu ya mafisadi na majizi,” alisema Bashe na kushangiliwa.

“Ni lazima tufike mahali Taifa hili tuache kuwa watu wa porojo....Taifa hili siyo maskini kuna wezi wapo bandarini. Najua saa hizi wanatafuta biashara nyingine.”

Mgombea huyo alisema wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea wa urais, kulikuwa na makundi ndani ya chama akiwamo na yeye lakini baada ya kumpata, Dk Magufuli tofauti zimekwisha.

Bashe alikuwa miongoni mwa vinara wa kumuunga mkono mgombea wa urais wa mwamvuli wa Ukawa kupitia Chadema, Edward Lowassa wakati akiomba ridhaa ya kuteuliwa na CCM kabla ya kuhamia upinzani.

Hata hivyo, jana alisema hataihama CCM kwa kuwa yeye na chama hicho hawakukutana barabarani na kwamba ni muumini wa mabadiliko ndani ya chama hicho.

Huku akigusia tuhuma zilizowahi kuvuma za yeye kuwaambia wananchi wamchague yeye halafu urais wampigie Lowassa, Bashe alisema wanaNzega watampigia kura Dk Magufuli asilimia zote na zikipungua hazitazidi asilimia tano.

Bulembo amvaa Sumaye
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo amemvaa Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye na kumtaka aache kuchukua mshahara na kurudisha walinzi wanaomlinda iwapo ataendelea kukitusi chama hicho kwamba hakijafanya chochote tangu uhuru.

Akiwahutubia wakazi wa Nzega jana, Bulembo alisema maisha yote ya kiongozi huyo na familia yake yametengenezwa na CCM lakini anashangaa kuona sasa anasimama kwenye majukwaa na kuwaeleza wananchi kuwa CCM haijafanya kitu.

“...Analipwa asilimia 80 ya mshahara wa Waziri Mkuu aliyepo madarakani, Mizengo Pinda. Mpaka leo bado ana ulinzi na anahudumiwa na Serikali hii. Kwa kupitia jukwaa hili la Nzega hebu Sumaye aache mshahara huo, arudishe walinzi awe raia kama sisi,” alisema Bulembo.
Aliendelea kurusha vijembe kwa kiongozi huyo akidai kuwa alinyang’anya ardhi ya wana ushirika wa Mvomero mkoani Morogoro baada ya kutetereka.

Magufuli na michango ya shule
Dk Magufuli jana aliendelea na kampeni zake mkoani Tabora na kuahidi kuwa akiingia madarakani atafuta michango yote shuleni inayosababisha baadhi ya wazazi washindwe kuwapeleka watoto shule.

Alisema anatambua kuwa baada ya sera yake ya elimu bure kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne kuanza kutekelezwa iwapo atachaguliwa, kuna baadhi watu wataanzisha michango isiyo na maana na kwamba atawashughulikia.

“Kuna mambo ya kuwaambia wazazi peleka dawati, peleka dawati na hata kama mtoto wa kwanza akishamaliza shule, ukimpeleka mwingine lile dawati hulikuti. Ninafahamu haya yote nitayashughulikia lakini pia, hakuna sababu shule kukosa madawati au viti wakati ipo karibu na miti, mbao zipo, haya yote tutaangalia tukizingatia masilahi ya walimu wetu,” alisema Dk Magufuli.

Akiwa Bukene wilayani Nzega, Dk Magufuli aliwatahadharisha makandarasi wazembe walioshindwa kukamilisha miradi yao kwa wakati akiwataka kufanya hivyo kabla ya Oktoba 25 kwa kuwa yeye ni kiboko yao.

Chanzo:
Mwananchi
 
Mkuu nisaidieni mie nimechanganyikiwa kiukweli.Hivi hawa watu wanaopigana vikumbo kutafuta madaraka,wanatafuta madaraka ili wafanye nini?Jk amewahi kutueleza kuwa anajua majina ya wauza sembe ila kama Amri jeshi mkuu hakufanya lolote sasa sijui nani achukue hatua,Leo tunamkata Lowasa ndiye ataje mmiliki wa RICHmond while mtu tuliyeingia nae mkataba yupo na JK nae anaishia kupoint fingures-Sasa nimechanganyikiwa hawa watu wanatafuta madaraka ya nini kama hawana uwezo?

Lowasa anapaswa kulaumiwa kwa kila jambo lililotokea ndani ya utawala wa JK kwasasabu yeye ndiye aliyekuwa mshawishi mkuu wa kumpeleke jk ikulu. Hivyo basi inamuwia vigumu JK kumsulubu swahiba wake wa miaka lukuki.
 
Lowasa ni mboni ya jicho la mabadiliko,ole ole ole,wake atakayejaribu kumgusa atatamani asingezaliwa,
mwacheni lowasa wetu kama alivyo enyi magamba ccm.
naona sasa hali mbaya lumumba, baada ya kuona mambo yamekuwa ndivyosivyoo!!

Leo hii kikwete anasema anayehusika na richmond ni yule anayetembea na lissu kwenye kampeni?

Maswali ya kujiuliza ni nani? Lowassa, sumaye, masha, au mgeja?

Mpango uliosukwa ni kwamba, jamaa akijibu lolote kwenye hili, au hata wenzake wakijibu kwamba nani huyo aliyehusika au kwanini wasimkamate, ndio wapate mwanya wa kumkamata ili asiendelee na kampeni na kumfungulia kesi mahakamani. Kesi hiyo itafanya akose rufaa na asiendelee na kampeni.

Hivyo naomba ukawa msiingie kwenye mtegoo huo, hawa jamaa wamekalia pabayaa.
 
Jakaya jembe haogopi atawataja tu mwaka huu, kaenda kujipanga tena akija anawataja wote kuanzia EPA, ESCROW, WASAFIRISHA SEMBE tena hawa alishasema anawajua kitambo, atawataja wote tu msijali mpaka waliopakia twiga kwenda uarabuni. Subirini tu muda bado upo.

Haahaa teh teh .ubarikiwe .nimeipenda hii .Kikwete hoyeeeeee
 
Inasikitisha sana kama miaka yote zaid ya nane aliyokaa madarakan baada ya kashfa ya richmond kama Raisi alishindwa kuchukua hatua yoyote ya kumwadhibu muhusika huku akijua kuwa ni nani,leo hii ndo anatamka hadharani kuwa ni nani? kuna uwalakin katika hili...toka hadharan basi uzungumze kama wewe ni mkweli......!!
 
Rais Jakaya Kikwete
amesema anashangazwa na
Mwanasheria wa Chadema, Tundu
Lissu kumtaka amtaje mhusika wa
Richmond wakati mwenye Richmond
yupo na anatembea naye mikoani.
Kikwete aliyasema hayo jana wakati
akiwaaga wananchi wa Kigoma katika
Uwanja wa Lake Tanganyika na
kumtaka Lissu amtaje mwenye
Richmond.
“Endapo Tundu Lissu atashindwa
kumtaja mwenye Richmond, nitatoka
hadharani na kumtaja mwenyewe,”
alisema Kikwete.
Kabla ya mkutano huo, Rais Kikwete
alifungua jengo la Mfuko wa Taifa wa
Hifadhi ya Jamii, (NSSF) ambalo
limejengwa kwa Sh7 bilioni.
Akifungua jengo hilo, aliwaomba
wawekezaji na mifuko ya kijamii kuiga
mfano wa NSSF kwa kuwekeza katika
sekta ya majengo kwa kuwa
yanapendezesha mji.
Kadhalika, Rais Kikwete alizindua
jengo la Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC) pamoja na nyumba 36 za bei
nafuu zilizopo katika eneo la Mlole,
Kigoma Mjini.
Richmond
Suala la Richmond imekuwa moja ya
ajenda za CCM katika kampeni za urais
hasa baada ya Waziri mkuu wa zamani
Edward Lowassa aliyejiuzulu wadhifa
huyo kwa kashfa hiyo kuhamia
upinzani.
Kila sehemu ambako mgombea urais
wa CCM anakwenda, suala hilo
limekuwa likiibuliwa, huku Lowassa
akisema yeye hakuhusika, bali
alijiuzulu kuiokoa Serikali isianguke
kwa kuwa ulikuwa uamuzi wa
wakubwa.
Mgombea urais wa CCM, Dk John
Magufuli amekuwa akienda mbali zaidi
akisema akichaguliwa ataanzisha
mahakama maalumu ya kushughulikia
mafisadi wanaosababisha umaskini
nchini.
Bashe ataka mahakama ya mafisadi
mapema
Wakati Magufuli akiahidi mahakama
hiyo, mgombea ubunge Jimbo la Nzega
Mjini (CCM), Hussein Bashe alimtaka
mgombea huyo jana kuiwahisha
mapema iwezekanavyo akiingia Ikulu
la sivyo atakuwa akihoji bungeni kila
mara.
Bashe alisema akipatiwa ridhaa na
wakazi wa jimbo hilo kuingia bungeni
hatakuwa mbunge wa “ndiyo mzee”
badala yake atakuwa akiisumbua
Serikali mara kwa mara likiwamo
suala la kudhibiti ufisadi nchini.
“Umesema utafungua mahakama ya
mafisadi na majizi... nikuhakikishie
waziri wako wa sheria utakayemteua
ajue atakutana na mtu anaitwa Bashe,
kila akiingia bungeni nitakuwa
namuuliza kila mara upo wapi
muswada wa sheria ya kuanzisha
mahakama maalumu ya mafisadi na
majizi,” alisema Bashe na
kushangiliwa.
“Ni lazima tufike mahali Taifa hili
tuache kuwa watu wa porojo....Taifa
hili siyo maskini kuna wezi wapo
bandarini. Najua saa hizi wanatafuta
biashara nyingine.”
Mgombea huyo alisema wakati wa
mchakato wa kumtafuta mgombea wa
urais, kulikuwa na makundi ndani ya
chama akiwamo na yeye lakini baada
ya kumpata, Dk Magufuli tofauti
zimekwisha.
Bashe alikuwa miongoni mwa vinara
wa kumuunga mkono mgombea wa
urais wa mwamvuli wa Ukawa kupitia
Chadema, Edward Lowassa wakati
akiomba ridhaa ya kuteuliwa na CCM
kabla ya kuhamia upinzani.
Hata hivyo, jana alisema hataihama
CCM kwa kuwa yeye na chama hicho
hawakukutana barabarani na kwamba
ni muumini wa mabadiliko ndani ya
chama hicho.
Huku akigusia tuhuma zilizowahi
kuvuma za yeye kuwaambia wananchi
wamchague yeye halafu urais
wampigie Lowassa, Bashe alisema
wanaNzega watampigia kura Dk
Magufuli asilimia zote na zikipungua
hazitazidi asilimia tano.
Bulembo amvaa Sumaye
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya
CCM, Abdallah Bulembo amemvaa
Waziri Mkuu wa zamani, Frederick
Sumaye na kumtaka aache kuchukua
mshahara na kurudisha walinzi
wanaomlinda iwapo ataendelea
kukitusi chama hicho kwamba
hakijafanya chochote tangu uhuru.
Akiwahutubia wakazi wa Nzega jana,
Bulembo alisema maisha yote ya
kiongozi huyo na familia yake
yametengenezwa na CCM lakini
anashangaa kuona sasa anasimama
kwenye majukwaa na kuwaeleza
wananchi kuwa CCM haijafanya kitu.
“...Analipwa asilimia 80 ya mshahara
wa Waziri Mkuu aliyepo madarakani,
Mizengo Pinda. Mpaka leo bado ana
ulinzi na anahudumiwa na Serikali
hii. Kwa kupitia jukwaa hili la Nzega
hebu Sumaye aache mshahara huo,
arudishe walinzi awe raia kama sisi,”
alisema Bulembo.
Aliendelea kurusha vijembe kwa
kiongozi huyo akidai kuwa
alinyang’anya ardhi ya wana ushirika
wa Mvomero mkoani Morogoro baada
ya kutetereka.
Magufuli na michango ya shule
Dk Magufuli jana aliendelea na
kampeni zake mkoani Tabora na
kuahidi kuwa akiingia madarakani
atafuta michango yote shuleni
inayosababisha baadhi ya wazazi
washindwe kuwapeleka watoto shule.
Alisema anatambua kuwa baada ya
sera yake ya elimu bure kutoka darasa
la kwanza hadi kidato cha nne kuanza
kutekelezwa iwapo atachaguliwa, kuna
baadhi watu wataanzisha michango
isiyo na maana na kwamba
atawashughulikia.
“Kuna mambo ya kuwaambia wazazi
peleka dawati, peleka dawati na hata
kama mtoto wa kwanza akishamaliza
shule, ukimpeleka mwingine lile dawati
hulikuti. Ninafahamu haya yote
nitayashughulikia lakini pia, hakuna
sababu shule kukosa madawati au viti
wakati ipo karibu na miti, mbao zipo,
haya yote tutaangalia tukizingatia
masilahi ya walimu wetu,” alisema Dk
Magufuli.
Akiwa Bukene wilayani Nzega, Dk
Magufuli aliwatahadharisha
makandarasi wazembe walioshindwa
kukamilisha miradi yao kwa wakati
akiwataka kufanya hivyo kabla ya
Oktoba 25 kwa kuwa yeye ni kiboko
yao.
 
Hii nchi kila mtu analalamika hata yule aliyepaswa kuchukua hatua !! Tutapona kweli. Hata kama Lowasa ni Fisadi kweli, ni nani kamlea mpaka kufikia hatua FISADI PAPA, kwa nini hakuchukuliwa hatua mapema angali FISADI DAGAA. Ndio maana watu wanahitaji mtu wa kuchukua hatua za papo kwa hapo.
 
CCM ni ileeeee ileeeeeeee na Kikwete ni yule yuleeeeeee mwaka huu CCM wataisoma nambaaaaaaaa..!!! Kikwete anatumia kila njia chama kisifie mikononi mwake. Mbaya zaidi huku anakoelekea ndio anazidi kujifunua nguo. Richmond isn't a big deal kwa sasa. It's too late.. kwani hata mkuu mwenyewe ni mtu wa issues tu.
 
Richmond si ndiyo imezaa Dowans - na bado inafanya kazi nchini. Hapo kama una akili timamu utajua Dowans (Richmond) kwa nini haijakimbizwa nchini?? bado inakula mabillion ya hela za watanzania hadi wa leo.
Richmond (Babu) akazaa Dowans (baba) naye akamzaa Symbion (mjukuu). Malofa na wapumbavu mwendo mbele kwa mbele, na mkuu wa malofa (lodilofa) anatuletea taarab za Khadija Kopa!
 
Rais naye anamuogopa waziri mkuu wake,huu ndio udhaifu ulio wazi wazi
 
Sasa huu ujinga sasa, Rais anaogopaje kutaja jina na ni amiri jeshi mkuu anaogopa nini? Watanzania tuamke la sivyo tutapelekwa pabaya
Kikwete baba mdogo wa Taifa.ataki kuvunja katiba ya ccm.ngoja Lowasa awe raisi na amiri jeshi mkuu.akisha kuwa RAIA atawasema wote Richmond.epa.escrow anawajuwa wote .hivyo subiri awe RAIA ndio utujua alivyo shujaa.Kikwete hoyeeee.
 
Sasa lisu amtaje mhusika kama nani ? Yeye rais ndio anatakiwa atoke hadharani na kutuambia nini kilijiri
 
Sasa ukijua lowassa anahusika na wizi kwenye deal ya richmond, kwanini ulishindwa kumuadabisha? Kwani ulishindwa kumuadabisha chenge. Kifupi ni kusema kwamba chama chenu kina operate kama gangsters, genge la
 
Kama anamjua haina haja ya kumtaja,apeleke ushahidi polisi sheria ichukue mkondo wake
 
Back
Top Bottom