Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Nashauri tumuongezee jk miaka mingine kama 15 ili aweze kutimiza ndoto na ahadi zake kwa Watanzania.
Hii ni kwa sababu imemchukua miaka zaidi ya saba pale aliposema hamjui mmiliki wa RICHMOND mpaka jana aliposema amemjua na hapo hajatutajia jina. Kwa maana hiyo akipata kama miaka 20 zaidi naamini anaweza kutimiza hata ahadi nyingine kama kutuletea meli Ziwa Victoria. Viva JK
 
Richmond=Richard Monduli.Walifanya wizi wa kimkakati(Strategic theft) jinsi ya kupata ushahidi beyond no doubt ni ngumu.Na sheria zilivyo najua huzijui ila Fisadi EL baada ya kukaa kwa muda inaonekana wamemshauri kwamba ukitaka kulikwepa sema "Wakupeleke mahakamani" wakati kama ni kweli yeye siyo MWIZI kwanini HAUMIZWI NA UFISADI na RUSHWA KABISA,Kwanini anagawa sana PESA na Kwanini UHALALI WA UTAJIRI WAKE NI SIRI KUBWA.Aseme jinsi alivyopata ili na sisi tunaotafuta tufuate nyayo zake.NI MWIZI TU.....
Mkuu nisaidie nchi hii tulimkabidhi nani?na je huyo mtu tuliyemkabidhi nchi kututajia jina la mwizi wa mali zetu anataka tufanyeje?tuchukue hatua mkononi?au anatuambia kuwa tulikosea kumkabidhi nchi kwa kuwa yeye na chama chake ni dhaifu na hawezi kuchukua hatua siyo?
 
Waliochota pesa za escrow ndio Richmond.
fwatilieni scandal ya Richmond, symbion, dowans, IPTL,PAP na hatimaye inazaliwa account ya escrow alafu watu kugawana pesa za kubeba kwa lumbesa.

Hii dili niya mda mrefu na mitambo ni hiyohiyo inabadilishwa tu majina ili kufikia itimisho la kuiba pesa za umma.
Kikwete anataka kututhibitishia yale yaliyosemwa na Mnyika. Yaani Rais mzima upige mipasho na taarabu kwenye jambo nyeti kama hili! Urais ni taasisi kubwa - kama anamjua kwa nini serikali yake isitaje waziwazi ikiwa ni pamoja na kuonesha ushahidi wa nyaraka badala ya Rais kutumia mipasho? EL alijiuzulu kwa kuwajibika kama msimamizi mkuu wa serikali (political responsibility) kama Rais Mwinyi alivyowahi kufanya alipokuwa waziri wa mambo ya ndani. Mwinyi alipojiuzulu, haikuwa na maana kuwa ndiye aliyeua wale mahabusu huko Shinyanga bali ilikuwa kuwajibika kisiasa. Sasa JK anataka kuchezea akili za malofa na wapumbavu kwa ktuimbia taarabu!
 
Kwanini hayuko jela au hata mahakamani huyo mhusika, anatajwa kimajungu majungu tu ndio maana raia wameamua kupuuza tu.

Uswahiba wa JK na fisadi Lowassa ndio umemfanya fisadi Lowassa aendelee kudunda, lakini JK anamaliza muda wake na tumeambiwa kesi ya fisadi Lowassa haina mwisho siku yoyote itaunguruma! Kwahiyo raia tukae mkao wa kula, Magufuli akiingia Ikulu lazima tuanze Lowassa.
 
Ccm mnaweweseka tu maana sisi tushamjuaga kwamba kikwete ndo muhusika kwahio hasitufanye wajinga wananchi tuna akili labda hao maccm ndo hawajui maana kama raisi anashindwaje kumfikisha mahakam huyo muhusika wakati babu seya tu alivotembea na mchepuko wake kikwete hadi leo anaoza jela hahaha watu tunajua na tunasema mwisho wa wakoloni weusi ni oct 25 viva lowassa viva ✌✌✌✌✌
 
ukisikia utamu kolea ndio sasa tumefikia patamu mzee wa richmond wakati wowote hadharani ukawa mtaumbukaje?
maana babu yenu ndio mwenye richmond halafu anatuiaminisha eti msafi kwa lipi?
 
Kabla hujatoka mapovu kuandika usiyoyajua ni busara ukajiuliza mbona huyo unayemtetea kwa mdomo wake hajawahi kumtaja muhusika wa Richmond?
Mkuu nisaidieni mie nimechanganyikiwa kiukweli.Hivi hawa watu wanaopigana vikumbo kutafuta madaraka,wanatafuta madaraka ili wafanye nini?Jk amewahi kutueleza kuwa anajua majina ya wauza sembe ila kama Amri jeshi mkuu hakufanya lolote sasa sijui nani achukue hatua,Leo tunamkata Lowasa ndiye ataje mmiliki wa RICHmond while mtu tuliyeingia nae mkataba yupo na JK nae anaishia kupoint fingures-Sasa nimechanganyikiwa hawa watu wanatafuta madaraka ya nini kama hawana uwezo?
 
Anaona jahazi linazama anataka kuwadanganya watu. Kwa nini miaka yote asiseme haya kama sio yeye ndio mmiliki mkuu. Imekula kwao watu hawabadiliki.... Lowassa awe fisadi, alikuwa fisadi watu ni lowasaaaaaa.

Kuna kipindi watu waliokuwa wanajiunga JF walifahamu kuwa hili ni jukwaa la watu wenye kufikiri na kubishana kwa hoja, wanachama wengi wa hivi karibuni badala ya kujibu hoja au kuhoji hoja wanaeleza hisia zao basi angalau hata waseme kwa nini wanahisi hivyo
 
Hivi wenzangu, ajenda ya ccm ni richmond tuuuu.... Mbona hawaongelei escrow, meremeta, mabehewa mabovu, nyumba za serikali kuuzwa, mv dar es salaam, barabara mbovu n.k n.k. Hivi vyote vinawagusa kwa asilimia kubwa lakini hawavioni wanaona richmond tuu....... Mi nafikiri jk hana hoja, na kwa kuwa anaishi jumba la vioo na huku kaazisha vita ya mawe basi ujue wakianza kurudisha mashambulizi akaadhirika.
 
Miaka 9 leo rais wa nchi anaogopa kutaja jina? Haaaahaaaaaa

Aiesee kikwete ni mmoja wa maraisi Bomu kuwahii kutawala Tanzania.taasisi ya raisi kama udaku wa kitaani .duuhh Mungu tunashukuru kutuwezesha kumaliza nae salama nakumuwezesha ataa hayo mazuri kidogo aliyofanya.atukuzwe Mungu juu mbinguni na Amani iwepo Tanzania.duuh raisi msaaniiii
 
Mkuu nisaidieni mie nimechanganyikiwa kiukweli.Hivi hawa watu wanaopigana vikumbo kutafuta madaraka,wanatafuta madaraka ili wafanye nini?Jk amewahi kutueleza kuwa anajua majina ya wauza sembe ila kama Amri jeshi mkuu hakufanya lolote sasa sijui nani achukue hatua,Leo tunamkata Lowasa ndiye ataje mmiliki wa RICHmond while mtu tuliyeingia nae mkataba yupo na JK nae anaishia kupoint fingures-Sasa nimechanganyikiwa hawa watu wanatafuta madaraka ya nini kama hawana uwezo?

Mkuu, mimi siwezi kukusaidia kwasababu kwanza sijakuelewa. Pili umechanganyikiwa! Samahani mkuu...
 
Back
Top Bottom