Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Rais Dhaifu sana kama anajuwa kwanini Wasimkamate miaka yote hiyo? kazi kucheka cheka tu
 
Ulipo tupo. Ninaichukia ccm kuliko shetani wabunge wake wanatukana bungeni wanatunga sheria za kunajisi taifa kwa mfano ya mafuta na gas sio kwa faida yetu ni kwa wageni viongozi wetu wamekua madalali mpaka ninajisikia aibu mbele ya wageni wanaokuja hapa nchini wengine wanapewa nafasi serikalini lakini si tu kwamba awatimizi wajibu wao bali wala hata awajui wajibu wao nini

Tuna kazi moja tu ya kuindoa CCM madarakani
 
Tunaomba atutajie na waliobeba hela kwenye rumbesa ESROW, ututajie majina ya wauza madawa coz ulisema una list, ututajie wauaji wa tembo wetu, ututajie wahusika wa ESROW .....ukishamaliza labda tutakuelewa

Raichi wechu alikuwa na jazba
 
kikwete hakumtaja mhusika. badala yake amemtaka tundu lissu ndie amtaje akidai anazunguuka nae.ameshindwaje kutamka jina lake? kama anamlenga lowassa itakuwa ni undumila kuwili maana wakati anajiuzulu uwaziri mkuu huyu huyu kikwete alimtetea akisema "alikumbwa tu na ajali ya kisiasa".

Tusubirie majibu ya LISU maana ni kama wamechokoza!
 
Rais Jakaya Kikwete amesema anashangazwa na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati mwenye Richmond yupo na anatembea naye mikoani.

Kikwete aliyasema hayo jana wakati akiwaaga wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika na kumtaka Lissu amtaje mwenye Richmond.
“Endapo Tundu Lissu atashindwa kumtaja mwenye Richmond, nitatoka hadharani na kumtaja mwenyewe,” alisema Kikwete.
Kabla ya mkutano huo, Rais Kikwete alifungua jengo la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF) ambalo limejengwa kwa Sh7 bilioni.
Akifungua jengo hilo, aliwaomba wawekezaji na mifuko ya kijamii kuiga mfano wa NSSF kwa kuwekeza katika sekta ya majengo kwa kuwa yanapendezesha mji.

Kadhalika, Rais Kikwete alizindua jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na nyumba 36 za bei nafuu zilizopo katika eneo la Mlole, Kigoma Mjini.

Richmond
Suala la Richmond imekuwa moja ya ajenda za CCM katika kampeni za urais hasa baada ya Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa aliyejiuzulu wadhifa huyo kwa kashfa hiyo kuhamia upinzani.

Kila sehemu ambako mgombea urais wa CCM anakwenda, suala hilo limekuwa likiibuliwa, huku Lowassa akisema yeye hakuhusika, bali alijiuzulu kuiokoa Serikali isianguke kwa kuwa ulikuwa uamuzi wa wakubwa.

Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amekuwa akienda mbali zaidi akisema akichaguliwa ataanzisha mahakama maalumu ya kushughulikia mafisadi wanaosababisha umaskini nchini.

Bashe ataka mahakama ya mafisadi mapema
Wakati Magufuli akiahidi mahakama hiyo, mgombea ubunge Jimbo la Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe alimtaka mgombea huyo jana kuiwahisha mapema iwezekanavyo akiingia Ikulu la sivyo atakuwa akihoji bungeni kila mara.

Bashe alisema akipatiwa ridhaa na wakazi wa jimbo hilo kuingia bungeni hatakuwa mbunge wa “ndiyo mzee” badala yake atakuwa akiisumbua Serikali mara kwa mara likiwamo suala la kudhibiti ufisadi nchini.

“Umesema utafungua mahakama ya mafisadi na majizi... nikuhakikishie waziri wako wa sheria utakayemteua ajue atakutana na mtu anaitwa Bashe, kila akiingia bungeni nitakuwa namuuliza kila mara upo wapi muswada wa sheria ya kuanzisha mahakama maalumu ya mafisadi na majizi,” alisema Bashe na kushangiliwa.

“Ni lazima tufike mahali Taifa hili tuache kuwa watu wa porojo....Taifa hili siyo maskini kuna wezi wapo bandarini. Najua saa hizi wanatafuta biashara nyingine.”

Mgombea huyo alisema wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea wa urais, kulikuwa na makundi ndani ya chama akiwamo na yeye lakini baada ya kumpata, Dk Magufuli tofauti zimekwisha.

Bashe alikuwa miongoni mwa vinara wa kumuunga mkono mgombea wa urais wa mwamvuli wa Ukawa kupitia Chadema, Edward Lowassa wakati akiomba ridhaa ya kuteuliwa na CCM kabla ya kuhamia upinzani.

Hata hivyo, jana alisema hataihama CCM kwa kuwa yeye na chama hicho hawakukutana barabarani na kwamba ni muumini wa mabadiliko ndani ya chama hicho.

Huku akigusia tuhuma zilizowahi kuvuma za yeye kuwaambia wananchi wamchague yeye halafu urais wampigie Lowassa, Bashe alisema wanaNzega watampigia kura Dk Magufuli asilimia zote na zikipungua hazitazidi asilimia tano.

Bulembo amvaa Sumaye
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo amemvaa Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye na kumtaka aache kuchukua mshahara na kurudisha walinzi wanaomlinda iwapo ataendelea kukitusi chama hicho kwamba hakijafanya chochote tangu uhuru.

Akiwahutubia wakazi wa Nzega jana, Bulembo alisema maisha yote ya kiongozi huyo na familia yake yametengenezwa na CCM lakini anashangaa kuona sasa anasimama kwenye majukwaa na kuwaeleza wananchi kuwa CCM haijafanya kitu.

“...Analipwa asilimia 80 ya mshahara wa Waziri Mkuu aliyepo madarakani, Mizengo Pinda. Mpaka leo bado ana ulinzi na anahudumiwa na Serikali hii. Kwa kupitia jukwaa hili la Nzega hebu Sumaye aache mshahara huo, arudishe walinzi awe raia kama sisi,” alisema Bulembo.
Aliendelea kurusha vijembe kwa kiongozi huyo akidai kuwa alinyang’anya ardhi ya wana ushirika wa Mvomero mkoani Morogoro baada ya kutetereka.

Magufuli na michango ya shule
Dk Magufuli jana aliendelea na kampeni zake mkoani Tabora na kuahidi kuwa akiingia madarakani atafuta michango yote shuleni inayosababisha baadhi ya wazazi washindwe kuwapeleka watoto shule.

Alisema anatambua kuwa baada ya sera yake ya elimu bure kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne kuanza kutekelezwa iwapo atachaguliwa, kuna baadhi watu wataanzisha michango isiyo na maana na kwamba atawashughulikia.

“Kuna mambo ya kuwaambia wazazi peleka dawati, peleka dawati na hata kama mtoto wa kwanza akishamaliza shule, ukimpeleka mwingine lile dawati hulikuti. Ninafahamu haya yote nitayashughulikia lakini pia, hakuna sababu shule kukosa madawati au viti wakati ipo karibu na miti, mbao zipo, haya yote tutaangalia tukizingatia masilahi ya walimu wetu,” alisema Dk Magufuli.

Akiwa Bukene wilayani Nzega, Dk Magufuli aliwatahadharisha makandarasi wazembe walioshindwa kukamilisha miradi yao kwa wakati akiwataka kufanya hivyo kabla ya Oktoba 25 kwa kuwa yeye ni kiboko yao.

Chanzo:
Mwananchi

AKITUTAJIA NA MUHUSIIKA MKUU WA ESCROW TUTAFURAHI ZAIDIi
 
Hivi Lowasa ana compete na nani katika uraisi? anashindana na Kikwete au Magufuli? naona Raisi ana weweseka kila kukicha kwenda majukwaani kupiga kampeni kwa kofia ya uraisi. Kwani hajifunzi kwa nchi nyingine duniani?, yeye ndo fisadi no 1 hivyo anaogopa upinzani wakiingia madarakani watafukunyua madudu yote aliyoyafanya. Yeye akae kimya na asubiri kukabidhi dola kwa amani huo ndo ukomavu wa democracy duniani. Leo utamuona Kikwete na serikali yote iko busy kufanya kampeni, kwani anaogopa nini? tulia ofsini subiri mzee kikwete, lasivyo tutakubogojoa.

Siku ya kufa nyani....Raichi wetu alikuwa na msongo wa mawazo alipokuwa anazungumza habari za RICHMOND
 
Yule aliyesema hilo suala amewaagiza makatibu wakuu waendelee na mchakato?
 
Kuna kiongozi mkubwa nchi hii anajifanya anamfahamu mwenye Richmond!
Aibu!! Amejidhalilisha na kujivunjia heshima na taasisi anayoingoza!!

Ndio akili ya kokosi kazi cha kampeni ccm.akili za watu 32 hizo.
teh teh tehee
 
Hili liko wazi...mtu anaweza kujiuliza, iweje mpaka leo (baada ya Lowassa kukimbia CCM) bado ana kigugumizi cha kuzungumzia mmiliki wa Richmond...kwa hali ya kawaida, huu ulipaswa kuwa muda wa kuweka kila kitu hadharani....

Kuja kwa LOwassa UKAWA tutajua siri nyingi za kifisadi ndani ya Serikali ya CCM
 
serikali ya ccm- kikwete haiwezi kamata mafisadi, serikali ya ccm yakufikirika - magufuri ndo inauwezo wakukamata mafisadi du, mafisadi yenyewe yapo ccm
 
Sasa asiendelee na kampeni c uchaguzi itaharishwa? Sheria za nec zinasemaje?
 
Prezida anatufanya wajinga kweli wananchi, eti atamtaja mhusika wa richmond, basi aanze kujitaja mwenyewe na familia yake halafu aje list ya mafisadi hapo tutamwelewa, vinginevyo atuache na LOWASSA wetu wasimkere
 
Siku si nyingi kila kitu kitakuwa clear hizi chenga chenga zitachujwa vizuri ila tu msije mkalalamika kwani mumeanza ninyi sisi tutamalizia."He who laughs last laughs loudest"
 
Huyu mtu anaitw Simuyu yetu anajitambua kweli mbona haongerei mafisadi ya escrow, hayo mahakama inaundwa kwa ajili ya watu wawili tu.
 
Back
Top Bottom