Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Magufuli mwenyewe anajinadi kupitia udhaifu wa Ikulu..KILA siku anapanda kulinda kilichokuwa kinaendelea kwa SEREKALI ambayo naye ALIKUWA ndani YAKE laminillas mfumo haukumsapoti...tunamwelewa ila hatuwezi kumpa nafasi kwanini mfumo ni uleule...lowasa kwanza..
 
Kikwete siku aliita wazee wa dar diamond jublee alisema hammjui mmiliki wa Richmond leo hii baada ya miaka saba anasema anamjua?
 
IKUMBUKWE KWAMBA KIKWETE KAMA NI KWELI ALITAMKA HAYO HAJATAMKA JINA LA LOWASSA POPOTE, KWANI KTK KAMPENI LISSU YUKO NA LOWASAA PEKEE!!!!? Raisi ana kigugumizi gani kutaja jina wakati Lissu anamtaja yy laivu ????? hakuna kudanganyana hapa mabadiliko na ukombozi wa pili ni sasa na ni lazima!! Lowasaa is my next pressdent!! NO MATTER WAT!!
 
Tusubirie JK akimtaja mhusika maana kasema asipomtaja Lissu atamtaja yeye
 
Hili suala lilimalizika kwa Lowassa kujiuzulu ili kuiokoa serikali mwaka 2008. Wanajaribu kuliibua ili kuharibu mood ya kampeni tunaomba Lowassa alijibu akiwa Ikulu ila kwa sasa elekeza nguvu kwenye kupata kura nyiiiiingi sisi tutakujibia kwa sababu tuna some data
 
Kweli kweli sasa nimeelewa kwanini wale wazee wetu waliweka hii methali..."Mjinga akierevuka,Mwerevu yu MASHAKANI"

Poleniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii Bravo Prof wa ki Beijing :A S 41::A S 41::A S 41:
 
Naona sasa hali mbaya lumumba, baada ya kuona mambo yamekuwa ndivyosivyoo!!

Leo hii kikwete anasema anayehusika na richmond ni yule anayetembea na lissu kwenye kampeni?

Maswali ya kujiuliza ni nani? lowassa, sumaye, masha, au mgeja?

Mpango uliosukwa ni kwamba, jamaa akijibu lolote kwenye hili, au hata wenzake wakijibu kwamba nani huyo aliyehusika au kwanini wasimkamate, ndio wapate mwanya wa kumkamata ili asiendelee na kampeni na kumfungulia kesi mahakamani. Kesi hiyo itafanya akose rufaa na asiendelee na kampeni.

Hivyo naomba ukawa msiingie kwenye mtegoo huo, hawa jamaa wamekalia pabayaa.

Mh Rais Kikwete hakutaja. Kaelekeza tu kidole. Angetaja au akitaja ni jambo jema. Jema kwani atakuwa ameanza kufungua mdomo kututajia walobeba viroba vya stanbic, escrow, mihadarati na meno ya tembo.
Karibu Mh Rais Kikwete ututajie ili kusafisha jkna lako na Ikulu kuwa si sehemu ya walanguzi.
 
Alipangalo mungu mwanadamu hawezi kulipangu kamwe,Nasema hivi nikikumbuka yaliyotokea na hili lilijitokeza sasa juu ya Jakaya na Richmond.
1.Profesa lipumba alimsafisha lowassa kwa nafsi yake na watanzania tukasikia.Baada ya week akatudi na kutuambia nafsi tena umemstuta."Hakueleweka"
2.Dr slaa akafanya mikakati ya kumsajili Lowassa ukawa,Baada ya kugundua kamati kuu imempendekeza EL agombee urais na si yeye akaibuka baada ya mwezi na kutueleza lowassa ni fisadi akiwa na documents za ikulu."Hatukumwelewa"
3.Rais Jakaya toka sakata la richmond litokee ni miaka 8 sasa chini ya utawala wake na kumekuwa na sintofahamu nyingi sana juu ya sakata hili.Leo anatuambia kimafumbo muhusika ni Lowassa baada ya Ccm kuzidiwa na lowassa huyo huyo na kuungwa mkono na wananchi wengi.Nasema naye amechelewa na hatutamwelewa pia.
Richmond imegeuzwa ajenda ya kupumbaza watz juu ya lowassa ambaye ameonyesha kukubalika na wengi.Huyu mtu ni mpango wa mungu ndio maana kila njama huvurugika au hufanyika kwa kukurupuka.
#Mabadiliko2015 Twende na lowassa mungu kashasema"Ndio"Hamna wa kusema"Hapana"Isipokuwa yeye pekee.
 
Hilo lipo wazi lowasa mwizi sana mahakama ya mafisadi ikija ataisoma namba fisadi huyu.

Hiyo mahakama itaanzishwa kwa Sheria itakayotungwa na Bunge. Sasa kukusaidia wewe na vihiyo wenzako mkiongozwa na Magufuli ni kuwa Sheria huwa Hazifanyi kazi kwa makosa yaliyopita, bali huanza kung'ata pale ilipoanzia, unless, pawe na provision inayoonesha itafanya kazi kwa yaliyopita, kitu hicho ni kigumu sana, hilo huwezekana kwenye gross violation of Human Rights tu, tena na Umma wa Kimataifa! Endeleeni kujitekenya na kujichekesha Wenyewe!
 
Hilo lipo wazi lowasa mwizi sana mahakama ya mafisadi ikija ataisoma namba fisadi huyu.

Hakuna kitu kama hicho cha mahakama ya mafisadi kuanzishwa,hiyo ni danganya toto ya kuombea kura.
Kwani hizi mahakama zilizopo sasa ni kwa ajili ya nini?Zinafanya kazi gani?
Hao mahakimu ya hiyo nyingine ya fiksi za kuombea kura watatoka nchi gani?

CCM mnawafanya watanzania mabwege, waacheni wananchi waamue wenyewe. Lakini siyo kwa hizi ahadi uchwara.
 
Laowassa hafai jamani tuache ushabiki

Ni kweli EL hafai hilo halina ubishi ila atapata kura zetu kwani tumechoshwa na ccm haswa na wabunge wake wasiojua wajibu wa mmbunge. Hivi ule upuuzi uliokuwa ukifanywa na wabunge wa ccm bungeni mlidhani leo hii kuna mtu atawasikiliza? Tumewachoka na tuko bora kuchagua wachafu zaidi ili nyie ccm mkapate wakati wa kuoga na hatimaye mrudi mkitambua wajibu wenu na wapi mlikosea.
 
Rais Jakaya Kikwete amesema anashangazwa na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati mwenye Richmond yupo na anatembea naye mikoani.

Kikwete aliyasema hayo jana wakati akiwaaga wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika na kumtaka Lissu amtaje mwenye Richmond.
“Endapo Tundu Lissu atashindwa kumtaja mwenye Richmond, nitatoka hadharani na kumtaja mwenyewe,” alisema Kikwete.
Kabla ya mkutano huo, Rais Kikwete alifungua jengo la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF) ambalo limejengwa kwa Sh7 bilioni.
Akifungua jengo hilo, aliwaomba wawekezaji na mifuko ya kijamii kuiga mfano wa NSSF kwa kuwekeza katika sekta ya majengo kwa kuwa yanapendezesha mji.

Kadhalika, Rais Kikwete alizindua jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na nyumba 36 za bei nafuu zilizopo katika eneo la Mlole, Kigoma Mjini.

Richmond
Suala la Richmond imekuwa moja ya ajenda za CCM katika kampeni za urais hasa baada ya Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa aliyejiuzulu wadhifa huyo kwa kashfa hiyo kuhamia upinzani.

Kila sehemu ambako mgombea urais wa CCM anakwenda, suala hilo limekuwa likiibuliwa, huku Lowassa akisema yeye hakuhusika, bali alijiuzulu kuiokoa Serikali isianguke kwa kuwa ulikuwa uamuzi wa wakubwa.

Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amekuwa akienda mbali zaidi akisema akichaguliwa ataanzisha mahakama maalumu ya kushughulikia mafisadi wanaosababisha umaskini nchini.

Bashe ataka mahakama ya mafisadi mapema
Wakati Magufuli akiahidi mahakama hiyo, mgombea ubunge Jimbo la Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe alimtaka mgombea huyo jana kuiwahisha mapema iwezekanavyo akiingia Ikulu la sivyo atakuwa akihoji bungeni kila mara.

Bashe alisema akipatiwa ridhaa na wakazi wa jimbo hilo kuingia bungeni hatakuwa mbunge wa “ndiyo mzee” badala yake atakuwa akiisumbua Serikali mara kwa mara likiwamo suala la kudhibiti ufisadi nchini.

“Umesema utafungua mahakama ya mafisadi na majizi... nikuhakikishie waziri wako wa sheria utakayemteua ajue atakutana na mtu anaitwa Bashe, kila akiingia bungeni nitakuwa namuuliza kila mara upo wapi muswada wa sheria ya kuanzisha mahakama maalumu ya mafisadi na majizi,” alisema Bashe na kushangiliwa.

“Ni lazima tufike mahali Taifa hili tuache kuwa watu wa porojo....Taifa hili siyo maskini kuna wezi wapo bandarini. Najua saa hizi wanatafuta biashara nyingine.”

Mgombea huyo alisema wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea wa urais, kulikuwa na makundi ndani ya chama akiwamo na yeye lakini baada ya kumpata, Dk Magufuli tofauti zimekwisha.

Bashe alikuwa miongoni mwa vinara wa kumuunga mkono mgombea wa urais wa mwamvuli wa Ukawa kupitia Chadema, Edward Lowassa wakati akiomba ridhaa ya kuteuliwa na CCM kabla ya kuhamia upinzani.

Hata hivyo, jana alisema hataihama CCM kwa kuwa yeye na chama hicho hawakukutana barabarani na kwamba ni muumini wa mabadiliko ndani ya chama hicho.

Huku akigusia tuhuma zilizowahi kuvuma za yeye kuwaambia wananchi wamchague yeye halafu urais wampigie Lowassa, Bashe alisema wanaNzega watampigia kura Dk Magufuli asilimia zote na zikipungua hazitazidi asilimia tano.

Bulembo amvaa Sumaye
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo amemvaa Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye na kumtaka aache kuchukua mshahara na kurudisha walinzi wanaomlinda iwapo ataendelea kukitusi chama hicho kwamba hakijafanya chochote tangu uhuru.

Akiwahutubia wakazi wa Nzega jana, Bulembo alisema maisha yote ya kiongozi huyo na familia yake yametengenezwa na CCM lakini anashangaa kuona sasa anasimama kwenye majukwaa na kuwaeleza wananchi kuwa CCM haijafanya kitu.

“...Analipwa asilimia 80 ya mshahara wa Waziri Mkuu aliyepo madarakani, Mizengo Pinda. Mpaka leo bado ana ulinzi na anahudumiwa na Serikali hii. Kwa kupitia jukwaa hili la Nzega hebu Sumaye aache mshahara huo, arudishe walinzi awe raia kama sisi,” alisema Bulembo.
Aliendelea kurusha vijembe kwa kiongozi huyo akidai kuwa alinyang’anya ardhi ya wana ushirika wa Mvomero mkoani Morogoro baada ya kutetereka.

Magufuli na michango ya shule
Dk Magufuli jana aliendelea na kampeni zake mkoani Tabora na kuahidi kuwa akiingia madarakani atafuta michango yote shuleni inayosababisha baadhi ya wazazi washindwe kuwapeleka watoto shule.

Alisema anatambua kuwa baada ya sera yake ya elimu bure kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne kuanza kutekelezwa iwapo atachaguliwa, kuna baadhi watu wataanzisha michango isiyo na maana na kwamba atawashughulikia.

“Kuna mambo ya kuwaambia wazazi peleka dawati, peleka dawati na hata kama mtoto wa kwanza akishamaliza shule, ukimpeleka mwingine lile dawati hulikuti. Ninafahamu haya yote nitayashughulikia lakini pia, hakuna sababu shule kukosa madawati au viti wakati ipo karibu na miti, mbao zipo, haya yote tutaangalia tukizingatia masilahi ya walimu wetu,” alisema Dk Magufuli.

Akiwa Bukene wilayani Nzega, Dk Magufuli aliwatahadharisha makandarasi wazembe walioshindwa kukamilisha miradi yao kwa wakati akiwataka kufanya hivyo kabla ya Oktoba 25 kwa kuwa yeye ni kiboko yao.

Chanzo:
Mwananchi

Huyu prezdnt ni shida,Lissu anatembea na wengi kwenye majukwaa
 
Wamemchokonoa JK mpaka kaanza kusema, wamchokonoe tena atutajie na wezi wa escrow! Mwaka huu tutawajua wezi wetu wote.
 
IKUMBUKWE KWAMBA KIKWETE KAMA NI KWELI ALITAMKA HAYO HAJATAMKA JINA LA LOWASSA POPOTE, KWANI KTK KAMPENI LISSU YUKO NA LOWASAA PEKEE!!!!? Raisi ana kigugumizi gani kutaja jina wakati Lissu anamtaja yy laivu ????? hakuna kudanganyana hapa mabadiliko na ukombozi wa pili ni sasa na ni lazima!! Lowasaa is my next pressdent!! NO MATTER WAT!!

Hajitambui preznt
 
Rais analalamika, makamu analalamika, waziri mbunge diwani pia, ahh ahh ahhh
 
Back
Top Bottom