Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Wengine mnaropoka tu humu.wanofahamu haya mambo ndio wametujuza hivyo.unataka nini zaidi?
 
Atuondolee shobo hapa.....

Amekuwa Rais wa Nchi hii kwa miaka 10 , nini kilimfanya asimkamate? (hapa anamaanisha mhusika wa richmond)
Kajisamehe wizi wake wa EPA.

Ana majina ya wauza madawa ya kulevya lakini hawakamati.
Alisema fedha za escrow siyo za umma ilihali CAG na bunge walisema ni za umma.
Twiga wamepandishwa ndege Rais akiwa yeye.

Tembo wetu wanamalizwa na Majangili na sisi ndiyo tunaoongoza kuexport meno ya Tembo, wanafanya chochote.

Atuondolee udhaifu wake hapa ,alitaka Wananchi ndiyo wamkamate muhusika wa Richmond?
Nchi ya Wananchi wanalalamika, Rais analalamika.

Watanzania muda wa Mabadiliko umefika wa kutuletea kiongozi ambaye atafanya maamuzi hata yale magumu badala ya kulalamika.
 
Raisi wangu kikwete kwa sasa naona umechanganyikiwa na harakati za mabadiliko za vijana rais wangu

Hivi kweli wewe wa kusimama na kusema lowasa anahusika na Richimondi
Kweli??? Nina hakika ulitukataa ukasema lowasa hahusiki na Richimondi ukaenda ukamshika mkono monduli kwa wananchi wake
Sasa ninahakika ipo siku hata kama mda wako umeisha utakuja kutuambia
Aliekuwa mwanasheria mkuu nae kaiba
Chenge nae kaiba
Tibaijuka nae kaiba
Ngeleja nae kaiba
Majizi yote yaliokula hela zetu utakuja kusema yameiba nayo halia ya kuwa rais wetu ulisema hawajahusika kuiba kama ulivyotuambia kwa lowasa
Ningekuwa na uwezo rais wangu ningekufwata lamda ungenisaidia kuhusu huyu lowasa na nisimpigie kura na ungenifurahisha sana kama ungemkamata ukafungulia mashitaka kuwa alipiga richimond sasa kwa hali hii ya majukwaani tutaamini kweli????


Siku wewe utagombea urais tutakubana urudishe hata zile za yatima ulizohepa nazo
 
Hahahahahahah unambwela mbwela tu ngoma nito hiyo wala hiyo riport huwezi iona na wakimpeleka Lowassa mahakamani hakuna anebaki wataenda wote nchi itasimama

Atuambie pia IPTL ni ya nani ???
 
Walioujumu uchumi wote wakamatwe, yaani Kuanzia rada, Richmond, Eskrow na ufisadi mwingine. Yaani hawa watu

wasingepewa nafasi kabisa ya kugombea nafasi yoyote. Siyo watu wa kukaa na kucheka nao, ni watu wabaya sana. Watu

ambao ni wabinafsi wasiokuwa na hata chembe ya uzalendo kwa taifa hili. Ni watu ambao amejilimbikizia mali nyingi sana

ndani hadi nje ya nchi.

Tena kibaya baadhi yao leo hii bado wanauroho wa madaraka ili waendelee kutunyonya kabisa. Hawafai hawa watu.

Tuwakatae kabisa.
 
CCM ikubali kuwa isipokufa mwaka 2015 itakufa 2020 WITH OR WITHOUT Lowassa
 
Wadau,kiongozi alikuwa nyerere labda na Lowassa akiwa rais,mkuu wa nchi ni wakutoa kauli kama hiyo.hatuna kiongozi hapo
 
Lowassa anatafuta sasa huruma aseme ameonewa. Swahiba wake JK hakuweza kumfunga lakini Magufuli hacheki na mtu. Ngojeni muone! Mnaosema mbona hajapelekwa mahakamani msiingie humu kulialia akipelekwa mahakamani!

Fisiem inatawala masikini kama ww ila matajiri hata haina nguvu nao hata kidgo hayo wawazo yako unawaza ukiwa ndotoni
 
Hili liko wazi...mtu anaweza kujiuliza, iweje mpaka leo (baada ya Lowassa kukimbia CCM) bado ana kigugumizi cha kuzungumzia mmiliki wa Richmond...kwa hali ya kawaida, huu ulipaswa kuwa muda wa kuweka kila kitu hadharani....

Wenzio hatuelewi sisi tunafuata mkumbo tu, hatuchukui hata muda wa kutafakari/ Tunaangalia wapi kuna watu wengi na

sisi hao tunaenda tu.
 
Ulipo tupo. Ninaichukia ccm kuliko shetani wabunge wake wanatukana bungeni wanatunga sheria za kunajisi taifa kwa mfano ya mafuta na gas sio kwa faida yetu ni kwa wageni viongozi wetu wamekua madalali mpaka ninajisikia aibu mbele ya wageni wanaokuja hapa nchini wengine wanapewa nafasi serikalini lakini si tu kwamba awatimizi wajibu wao bali wala hata awajui wajibu wao nini
 
Uhuru na Ruto bado wanakesi ICC lakini wanakenya wamewaingiza Ikulu na WAtanzania tutafanya hivyohivyo kwa Lowassa.Umma hautishiwi mnyau.
 
Back
Top Bottom