Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Wewe wewe!!!!! Heeeee dada yangu shosti , embu wajaribu kumkamata Lowassa halafu waone. Nakwambia hii nchi haitakalika hata kwa nusu saa.
Na lazima watajuta kwa kufanya huo upumbavu.

Yani wameshindwa kumkamata miaka nane yote waje wamkamate leo??? Nakwambia kama wanataka kufa basi tutakufa wote

Asee kufa peke ako
 
Last edited by a moderator:
Alikua wapi adi aseme leo?..JK Aache unafiki kampeni zmemshinda...alikaa kmya. Muda wote kwakua yeye ndio muhusika mkuu
 
kosa la jinai mmeshaelimishwa mtu anaweza kukamatwa hata baada ya miaka 100. kwani hamjaona manazi wa vita vya pili vya dunia wanakamatwa hadi leo na kushitakiwa. kusema kwa nini akamatwe leo kuna siasa lakini kisheria kama kosa lipo itakua sawa tu.

basi mkuu, tusubiri baada ya miaka 50 ndipo akamatwe. au unasemaje?
 
Ni bora hata hizo za mfukoni FISADI LOWASSA Aligombea na nani huko Chaggadema na alipata kura ngapi.Ratiba ya vikao vya uteuzi ilikuwaje.

Blaza umezoea kudanganywa unadhani ule mchakato wa kinafuki ndio unatoa kiongozi bora? Ule mchakato ni kama KILI music Awards.
 
Baada ya Rais kuweka bayana kuwa mhusika wa Richmond ni Lowassa sasa file linaandaliwa na ushahidi wa kutosha umepatikana na ndio maana rais JK amejitokeza baada ya miaka 8 kulisemea hadharani.

Tahadhari
hatutaki fujo wakati Lowassa atakapokamatwa kujibu tuhuma.

Mahakama sasa ndio itasema nihusika ama la kwa hiyo tuendelee kuitunza amani.

Hata wampeleke the Hegue kama Rais wa KENYA huyo ndiyo RAIS WETU.

Kikwete anamwambia Lissu amtaje wakati Lissu kashamtaja mhusika.Rais wa nchi anaogopa raia wake
 
Wakuu salaam

Yaani ukistaajabu ya Mussa kweli hujakutana na ya Firauni!!

Mtu unaulinzi wa vyombo vyote vya sheria na Maguvu. Kuanzia Polisi,Magereza, Migambo, Wanamaji, Wanaanga, Mizinga na kila aina ya chombo cha Ulinzi. Unaweza kuamrisha fulani akamatwe, aswekwe korokoroni, Lupango, Mahabusu, na hata Kizuizini na hilo likafanyika haraka sana bila mpewa amri kujiuliza mara mbili.!! Kama hiyo haitoshi umewekewa Ulinzi wa kisheria na Katiba ya Nchi kwamba Kwa lolote utakalofanya ukiwa Madarakani ni marufuku kukamatwa wala kushitakiwa..!!!

Lakini bado mtu ili kumtaja Mwizi, Fisadi aliyelisababishia Taifa hasara ya Mabilioni ya shilingi unapata kigugumizi kumtaja, Badala yake unazungukazunguka huku na huku kutafuta namna ya kum-address mbele ya halaiki ya wananchi wenye imani na wewe, waliopanga foleni na jua kali kukupigia kura, unawayawaya kutaja jina la Fisadi..Whyyyyyyyyyyyyyyyyy!! Eti ni yule anayezunguka na fulani.... hivi hana jina au humjui? Ananguvu kukuzidi au. ana nini hasa mpaka ukwepe kutaja jina lake?

Umepungukiwa nini mtu kama wewe? Wananchi wanasababu ya kuendelea kukuamini wewe pamoja na chama chako.? Hebu jifikilieni mara mbili..!! Mnahadhi ya kupata kura yangu na za Wananchi wengine??

BACK TANGANYIKA
 
Hizi zinaitwa ni za uso!!! Safi sana Kamanda Esther Bulaya.

Mbona aliyetajwa na Lowassa kuwa ndio mwenye deal ya Richmond hajitokezi hadharani kukanusha?
Hii inanifanya nione wazi kuwa Lowassa alitengenezewa zengwe na walihakikisha wanatuaminisha sie wananchi kuwa Lowassa ni fisadi ilhali wao ndio wanaoendelea kufaidia na deal la Richmond na kampuni zilizofuatia baadae!!
 
Mnatishiwa nanyi mnaamini.mnajua sheris za uchaguzi.Endeleenu na jitihada za kijenga ukombozi.Ni Lowasa pekee.
 
Anaona jahazi linazama anataka kuwadanganya watu. Kwa nini miaka yote asiseme haya kama sio yeye ndio mmiliki mkuu. Imekula kwao watu hawabadiliki.... Lowassa awe fisadi, alikuwa fisadi watu ni lowasaaaaaa.

Kikwete anathubutu kunyosha mkono kuwa Lowasa ni fisadi?ashukuru kiapo alichoapa Lowasa na sumaye.,uhuni uliopo serikalini ungeanikwa vizuri.
 
Wataweweseka sana. Hakuna namna MABADILIKO ni LAZIMA 2015 CHAGUA LOWASSA.
 
Kweli hawa jamaa ni wajinga kwani LISU ni mwanasheria wa serikali hata wamtake amtaje? Jakaya ndiye haswaaa anayetakiwa kumtaja lakini inashangaza kuona miaka mingi sasa mmiliki wa richmond hafahamiki. Jakaya usitutie ujinga.
 
Baada ya Rais kuweka bayana kuwa mhusika wa Richmond ni Lowassa sasa file linaandaliwa na ushahidi wa kutosha umepatikana na ndio maana rais JK amejitokeza baada ya miaka 8 kulisemea hadharani.

Tahadhari
hatutaki fujo wakati Lowassa atakapokamatwa kujibu tuhuma.

Mahakama sasa ndio itasema nihusika ama la kwa hiyo tuendelee kuitunza amani.

Habari zako ambazo hazina Source of information. Mdogo wangu utafungwa acha propaganda za kupachikwa.
 
Una kila kitu Baba mbona unatuchanganya? au kuna Mtu juu zaidi yako anakuzuia kutoa maamuzi?
 
mhusika mkuu wa wizi wa richmond ni EDWARD NGOYAI LOWASSA - GAZETI MWANANCHI LA LEO AS PER J.K's statement
 
Hapa ni lowasa tu mpaka kieleweke wengine watapiga kelele lakini hatutobadilika sisi na familia zetu, hapa ndani kwangu tu tayari dada wa kazi amejiandikisha na kura ni kwa lowasa, mke wangu the same na mdogo wangu the same hapo ni kura nne ndani ya kaya moja
ushawishi wangu kazini na kwa wateja wangu pia ni mkubwa so nyuma yangu kuna kura c chini ya 500 hapo hujakutana na wapenda mabadiliko wenzangu tuliopo kwenye mfumo hapo kimkakati ccm washaanguka
 
Back
Top Bottom