Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Hao CCM ndio watakuwa malofana wapumbavu. Wasubiri mtuhumiwa ajibu jukwaani ndo wamkamate?
Kama wana ushahidi kwanin wasimkamate toka mwanzo?
Kikwete asituharibie nchi.
kosa la jinai mmeshaelimishwa mtu anaweza kukamatwa hata baada ya miaka 100. kwani hamjaona manazi wa vita vya pili vya dunia wanakamatwa hadi leo na kushitakiwa. kusema kwa nini akamatwe leo kuna siasa lakini kisheria kama kosa lipo itakua sawa tu.
 
Kila siku mnalalamika jk ataje nani Mwenye Richmond Leo ametaja mnabisha .

Jk na Lowasa ni wanasiasa naamini wanajua wanachokifanya hivyo ni juu yetu wananchi kupepeta pumba na mchele .
 
Vijana munarukaruka na kukanyagana wenyewe mpaka basi, mara oohhh mbona hawamkamati kama yeye…!! Leo mumegeuka munasema mbona hawakumkamata toka mwanzo…!! Kesho mutakuja na jipya lingine lakini Mwakyembe alishaambia kesi ya jinai haina mwisho.
 
attachment.php
 
Waimba mashairi bana chezea jk wewe ana ubavu wa kumpeleka lowasa mahakamani? Yaan mpaka nashindwa kujua kazi ya mahakama mpaka watu waimbeeee na ushahidi wamebebelea makwapani
 
Mgombea Ubunge jimbo la Bunda mjini ndg Esther Bulaya katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika Bunda Stoo Bunda mjini amesema kwamba CCM waache kulalamikia Richmond kwa kumwandama mgombea wa UKAWA ndg EDWARD LOWASSA kua ndiye aliyekua mhusika wa Richmond! Bulaya amesema kua Lowassa alitoa muda mrefu na wa kutosha vyombo husika wafanye uchunguzi lakini mpaka leo wako kimya, tangu kashfa ya Richmond itokee viongozi wote wa CCM walikaa kimya na hawajawahi kusema chochote, wanaCCM ndio wanaijua kwa kina Richmond kwanini hawakisema siku zote?
Aidha Bulaya amesema kuna watu wameishiwa hoja wamebaki na Richmond tu ila hakuna kingine cha kuzungumzia, amesema hakuna mahali popote panamtaja Lowassa kama mhusika wa Richmond ispokua alitakiwa kuwajibika kwa sababu yaliyofanyika yalikua Chini yake.

Chanzo: Mimi mwenyewe.
 
Mh raisi unasikitisha sana
Hii inathibitisha kauli ya Mnyika kuwa CCM in dhaifu, Serikali ya CCM ni dhaifu na Viongozi wakuu wa serikali ni dhaifu!!

Kwa mujibu wa katiba yetu ni rais peke yake mwenye kinga ya kupelekwa mahakamani, sasa huyo mwingine ambaye kwa zaidi ya miaka 8 serikali imeshindwa kumfikisha mahakamani ni nani na ana kinga gani kikatiba?!

Mbona Mramba na Yona wamehukumiwa kwa matumiza mabaya ya madaraka?!

Hakika kiongozi wetu amejidhalilisha!!!
 
Kwa wale ambao sheria hamzijui, na pia kesi na mienendo yake!! Unaambiwa kesi ya jinai ni kama ugonjwa, saa yoyote inaeza kuanza!! Hata kama ilikua dormant for even 50 years, as Farr as muhusika still alive, carry on.

#hapakazitu babangu.
 
Ha hahaaa ni kichekesho lowasa anasema aliagizwa na mamlaka yabjuu yake, leo tunaambiwa yule anayetembea na lisu kaazi kweli kweli. Bora tumchague lowasa mabadiriko tuyaanzie hapo
 
Wewe wewe!!!!! Heeeee dada yangu shosti , embu wajaribu kumkamata Lowassa halafu waone. Nakwambia hii nchi haitakalika hata kwa nusu saa.
Na lazima watajuta kwa kufanya huo upumbavu.

Yani wameshindwa kumkamata miaka nane yote waje wamkamate leo??? Nakwambia kama wanataka kufa basi tutakufa wote

Alikamatwa Sheikh Ponda, na tuoo tuli tunadunda....Lowassa ana nini cha ziada?
 
Last edited by a moderator:
yaani raisi anashindwa kutaja jina la muharifu nchini? kweli hii ni Tanzania
 
Kura yangu itarudi CCM ikiwa atawachukulia hatua za kisheria hao mafisadi sio kuwataja tu. KUWATAJA HAITOSHI
 
Back
Top Bottom