Rais Karume Akagua Gwaride la Idd - Imekaaje?

Hili swala la Kiingereza naona umelishikia bango kinoma! Anyway I'll write in english when is needed! So far threads zote ninazo changia zipo kwa kiswahili..:D

Wewe sema ukweli tu. Lugha haipandi. Huwezi kuandika zaidi ya aya tatu kwa kiingereza tu. Unabisha? Na ndio maana mada zote unazochangia ni za kiswahili....heheheheheeee
 
Wewe sema ukweli tu. Lugha haipandi. Huwezi kuandika zaidi ya aya tatu kwa kiingereza tu. Unabisha? Na ndio maana mada zote unazochangia ni za kiswahili....heheheheheeee
Tembelea blog yangu...zipo mada kadhaa kwa kiingereza...Usisahau kuwa na dictionary :D
 
Last edited:
Asalamu alaykum.

Kwanza naomba kuwafahamisha watu waliouliza swali hili kuhusu gwaride lilofanyika kwenye sherehe za Eid El Fitri kwanza naomba mfahamu kuwa Rais Karume hakukagua gharide ila gharide lilikuwepo na amepokea gharide mtangazaji ama amekosea au ufahamu wake ni mdogo katika maswali haya ya kipolisi.

pili zanzibar ni kweli asilimia 99 ya wakaazi wake ni waislamu kwa hivyo licha ya kuwa katiba ya zanzibar na ya tanzania kusema kuwa nchi hizi haziongozwi kwa dini lakini kwa zanzibar huwezi kutenganisha dini ya uislamu na shughuli za kiserikali iadha iwepo au isiwepo kisheria kama ilivyo marekani sio nchi ya kikristo lakini huwezi kutenganisha taifa hilo na ukiristo nadhani utakuwa umefahamu maana mambo mengine huja automatical.

kilichofanyika jana ni gharide la heshima ambalo halijaanza kwa Rais Karume huyu tu tokea miaka ya nyuma kabla ya Rais wa kwanza Abeid Karume mwenyewe na hilo hata Mwalimu Nyerere ameshawahi kuhudhuria sherehe za Eid mara kadhaa na kupokea gharide la heshima kama alivyopokea Rais Karume jana infact sio kitu cha ajabu kwa zanzibar wala sio kitu cha kushangaza ni jambo la kawaida kutokana na mazingira ya hapa kwetu.

kuhusu sherehe za krismas na gharide kwanza gharide litapigwa wapi katika shughuli ipi kwenye misa au wakati watu wanatoka nje kwa sababu sherehe za krismass hufanyika kanisani. sherehe za Eid hazifanyi msikitini ila watu huenda asubuhi kusali na baadae saa nne ndio huenda katika holi na huko hutolewa hutuba na wanaokwenda huko sio waislamu peke yao kuna mbalozi ambazo idadi kubwa sio waislamu, kuna viongozi wa kidini ambayo hualikwa kulingana na kadhehebu yao mapadri wetu hapa zanzibar huhudhuria sherehe hizo tena mara zote wanahudhuria kikamilifu hata sherehe za kwenda kwenye makaburi ya Mzee Karume mapadri hapa zanzibar huenda kuomba dua kwa hivyo hapa zanzibar mfahamu uislamu sio dini tu bali uislamu pia ni cuture yetu kwa hivyo inakuwa ni vigumu sana kutengua vitu viwili hivi.

kuhusu mwezi mtukufu wa ramadhan kuna mtu amesema kuwa hakuuzwi chakula ni kweli ila mtu hajakatazwa kula ila kula hadharani ndio kosa na hilo tokea wakati wa utawala wa kikoloni na wananchi wote huwa wanaustahi mwezi huo sio kwa kulazimishwa na ikifika ramadhani siku mbili kabla wananachi hutolewa matangazao katika vyombo vya habari kupitia kamisheni ya utalii na kuambiwa watu kuwa mwezi mtukufu umefika na wanaombwa kuuheshimu na hata kama wanataka kula basi wasiwabughudhi waliofunga.

lakini jengine wenyewe waislamu hawawezi kuuza vyakula walati wao wamefunga dini yao inawakataza kuwalisha watu wenye uwezo wa kufunga ila wenye dharura ya ugonjwa na watoto wadogo na wasiokuwa waislamu wanaweza kula hawajakatazwa wala sheria haiwabani lakini wananchi wa zanzibar hao waliokuwa sio waislamu wamezowea kuuheshimu mwezi wa ramadhan jinsi wasilamu na wakristo zanzibar walivyo ndugu wanaheshimiana na kustahiana na ndio maana unakuta hata wakristo wa zanzibar mavazi yao ni tofauti na wakaristo wa sehemu nyengine na hilo sio kwa kuwa wanalazimishwa au wanachaguliwa nguo za kuvaa la hasha ni utamaduni uliozoweleka tokea miaka ya nyuma.

zanzibar usishangae kwenda mazikoni ukakuta nusu ya waislamu na nusu iliobaki ni wakristo tena utakuwa ndugu wanne wawili wakristo na wawili waislamu na ndio kama mnafahamu hata marehemu Doglas Toto aliyekuwa baba Askofu Mjomba wake amabye ni ndugu ya mama yake alikuwa sheikh mkubwa tu hapa Tanzania.

udugu wa waislamu na wakristo hapa zanzibar ni wa kupigiwa mfano na unaweza usimfahamu mtu kama ni muislamu au mkristo mimi binafsi nimesoma na wakaristo shule ya primary lakini sikuwa nafahamu kama wao ni wakristo hadi naingia nao sekondari kutokana na kutokuwepo na tofauti yoyote kati yangu na wao kila kitu tulikuwa ni sawa kwetu wala sijawahi hata siku moja kufukuzwa kwao wala yeye hajawahi kufukuzwa kwetu mimi nilikuwa naambiwa ni dada yangu na yeye alikuwa akinitambulisha mimi ni ndugu yake kila tunapokwenda hadi tumekuwa watu wazima tumeshikamana ikifika krismas nakwenda kwao na ikifika sherehe za Eid anakuja kwetu tunasherehekea pamoja.
 
Mmeanza kutukanana kwa lugha tena kwani kujua kiingereza ndio issue? mbona watanzania tunatakiwa kujivunie lugha yaetua adhimu ya kiswahili mimi naona kutokujua kusema kiingereza sio sababu ya mtu kuwa mjinga na bora zaidi ukafahamu lugha yako ya kuzaliwa kuliko kuiga lugha za watu mwenye kujivunia chake ndio bora katika dunia hii mimi nafurahi mtu akinambia sijui kiingereza wala sikasiriki kwa sababu sio lugha yangu lugha yangu ni kiswahili.
 
Asalamu alaykum.

kilichofanyika jana ni gharide la heshima ambalo halijaanza kwa Rais Karume huyu tu tokea miaka ya nyuma kabla ya Rais wa kwanza Abeid Karume mwenyewe na hilo hata Mwalimu Nyerere ameshawahi kuhudhuria sherehe za Eid mara kadhaa na kupokea gharide la heshima kama alivyopokea Rais Karume jana infact sio kitu cha ajabu kwa zanzibar wala sio kitu cha kushangaza ni jambo la kawaida kutokana na mazingira ya hapa kwetu.

Aleykhum Salam Stone Town!

Habri ya Zenji Mkuu?

Asante sana kwa ufafanuzi wako wa kina katika hili. Naanza kupata Mwanga ingawa Mantiki yake bado sijaiona zaidi ya "Mazoea na Heshima" katika Sikukuu ya Idd.

Pamoja na kuwa hili ni suala la kimazoea kwa Zanzibar kama ulivyosema, je unao mfano wowote wa nchi za kiislamu au kikristu ambao hufanya gwaride la heshima wakati wa sikukuu za kidini?
 
Duh...! Yaani hizo nchi nyingine haziwezi kuiga ZNZ!? Ila ZNZ ndo wanapaswa kuiga hizo nchi zingine!?
 
Duh...! Yaani hizo nchi nyingine haziwezi kuiga ZNZ!? Ila ZNZ ndo wanapaswa kuiga hizo nchi zingine!?

Inawezekana X-PASTER;

Je waweza kutuelimisha mantiki yake ni nini? Naona swali sijibiwi au sijawaelewa?
 
Kiongozi;

CIA World Fact Book ya 2008 ina facts hizi juu ya Tanzania:

Population: 40,213,160

Religions:

mainland - Christian 30%, Muslim 35%, indigenous beliefs 35%; Zanzibar - more than 99% Muslim.

Mimi sina uhakika na Souces za Data hizo.

Hata hivyo bado napata tabu ya kujua mantiki ya Gwaride katika sherehe za kidini.

Source ya data hizi za CIA nadhani ni satelite survailence, wanajua wamarekani walikozipata. Lakini inafurahisha sana kusikia Gwaride la Idd, sijui ni jeshi lipi lililocheza kwata hizo za idd, we have to explore possibilities za Gwaride kwa ajili ya waumini wa dini nyingine. Tanzania kila kitu kinawezekana.
 
Khe yaani nyinyi huyo Mtangazaji Bom ndiyo anakushughulisheni katika mjadala. Hakuna Gwaride la Idd. Kuna Gwaride la|Heshima (guard of honour) This can mounted by the gallant forces to their Comander in chief ( his representatives) any where any time inapoonekana inafaa kutolewa heshima hiyo.
 
Je waweza kutuelimisha mantiki yake ni nini? Naona swali sijibiwi au sijawaelewa?
Soma hapa chini maneno ya Sabri...

Khe yaani nyinyi huyo Mtangazaji Bom ndiyo anakushughulisheni katika mjadala. Hakuna Gwaride la Idd. Kuna Gwaride la|Heshima (guard of honour) This can mounted by the gallant forces to their Comander in chief ( his representatives) any where any time inapoonekana inafaa kutolewa heshima hiyo.
Mara nyingi gwaride hili hufanywa na kikosi cha FFU wakiwa kwenye zile kofia zao kama wachungaji wa ng'ombe
 
Asalaam Aleykhum Viongozi;

Nimesikia na kuona katika Taarifa ya Habari ya ITV (very briefly) leo usiku Rais Karume amekagua gwaride la Idd. Niliona gadi moja ya vijana wetu wa kazi FFU.

Hii imekaaje?

Naomba mnisaidie kujua mantiki ya Gwaride katika sherehe za kidini.

Raisi Karume hana kazi za kutosha ndio maana anao muda wa kukagua hata magwaride yasiyoeleweka yasiyo na kichwa wala miguu.

Pia hao askari nao waliopiga hilo gwaride nadhani nao hawana kazi za kutosha za kufanya au hawakuwa na hela za kutosha kusherehekea iddi wakaona waende kupiga gwaride lisilokuwa na kichwa wala miguu angalau wapate pilau ya bure baada ya gwaride.

Na wanajeshi nao mnapoambiwa muwe na utii si maana yake kuwa mtumiwe kupiga gwaride kwenye pilau za Iddi za watu ili kujikomba kwa waliopika pilau.That is beyond military norms.Bunge labda lihoji maana ya gwaride kwenye eneo la usawa wa gudulia la pilau siku ya Idd.
 
You are pathetic....
 
Wewe sema ukweli tu. Lugha haipandi. Huwezi kuandika zaidi ya aya tatu kwa kiingereza tu. Unabisha? Na ndio maana mada zote unazochangia ni za kiswahili....heheheheheeee

Uchokozi tu, muone vile! mbona unanisema sasa!!
 
Back
Top Bottom