Tetesi: Je ni kwanini Trump alishindwa kumkabidhi rais Biden sanduku la nyuklia.?

Adolph Jr

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
5,558
8,631
Tunaishi ndani ya dunia iliyo ndani ya begi dogo mno ni kiasi cha mistake ndogo tu tunaiacha dunia, twende pamoja....

Fununu kuhusu sanduku hilo...

Sanduku hili ndilo inaloitwa black Box ama 'sanduku la nyuklia', sanduku lililotengenezwa kwa chuma linalomuandama rais wa Marekani kila mahali iwapo anataka kurusha bomu la kinyuklia akiwa nje ya ofisi.

Tangu sanduku hilo lilipoanza kutumika wakati wa utawala wa rais John F Kennedy, ubebaji wa sanduku hilo umekuwa kitu muhimu licha ya kutokuwa miongoni mwa vitu muhimu katika sherehe hiyo ya kumuapisha rais mpya nchini Marekani.

Tukio lilitokeaje?
Hatahivyo , mwaka 2021 U.S.A ilikabiliwa na changamoto kubwa : kwa mara ya kwanza katika zaidi ya karne moja, rais anayeondoka mamlakani hakuwepo katika halfa ya kumuapisha mrithi wake.

Kulingana na itifaki , Trump alipaswa kuwa na sanduku hilo la nyuklia hadi saa sita usiku tarehe 20 jan 2021 .
lakini kufikia wakati huo tayari alikuwa umbali wa kilomita 1500, kusini mwa Florida mbali na rais Biden , ambaye alipaswa kumkaribisha wakati huo.

Hatahivyo kuna masunduku kama hayo kulingana na watalaamu ambayo huwa tayari kutumika katika matukio kama hayo.

Hatahivyo , wataalam kadhaa na wasomi walielezea matukio kadhaa yanayoweza kufanyika iwapo hali hiyo isiyo ya kawaida itafikia hapo katika historia ya Marekani .
Wakati wa hafla ya kituo cha udhibiti wa silaha, Stephen Schwartz, alielezea kwamba tofauti na fikra za wengi kuna masunduku matatu ya aina hiyo.

Moja ni lile linaloandamana na rais , lakini kuna orodha nyingine ya dharura inayopewa makamu wa rais ama mtu aliyepona { waziri ambaye huteuliwa kuchukua mamlaka iwapo kwa sababu fulani viongozi wote wamefariki}

Schwartz alisema kwamba Pentagon inaweza kutumia mojawapo ya masunduku yake - ama kuandaa jipya ili kumkabidhi Biden na kulifanya kuweza kufanya kazi punde Biden atakapoapishwa tarehe 20-01-2021.

Wakati huo , usimamizi wa Trump wa nyuklia na udhibiti unaisha , hivyobasi kadi zake zinazotoa nambari hizo za siri za sanduku hilo la nyuklia huzimwa.

"Iwapo afisa anayebeba sanduku hilo ataandamana na Trump katika ndege ya Airforce One kuelekea Florida , msaidizi huyo ataondoka mahala alipo Trump mwendo wa saa sita kamili na kurudi Washington na sanduku hilo, Schwartz aliambia CNN.

Mchakato halisi
Ni hali hiyo ambayo suala la sanduku hilo limezua maswali mengi na matumizi yake yamewavutia mamilioni ya watu miaka yote.

Hatahivyo kile ambacho watu hawakijui ni kwamba nambari za siri na funguo zake katika sanduku hilo ambazo zinamruhusu rais kuwa na uwezo wa kutoa maagizo ya kutekeleza shambulio hazipo katika sanduku hilo.

Funguo hizo za uwezo wa kutekeleza shambulio la kinyuklia huwa ni kadi ndogo ya plastiki ambayo rais aliye madarakani hubeba mfukoni. Kadi hiyo hujulikana kama ''Code of Gold au Cookie''

Rais hutakiwa kuikata mara mbili ili kuthibitisha utambulisho wake anapowasiliana na kitengo cha vita katika Pentagon , ili kuruhusu shambulio.

Mapema siku ya kuapishwa kwa rais , rais mpya na makamu wake hupokea maagizo ya jinsi ya kutumia sanduku hilo na rais anayechukua mamlaka hupatiwa kadi hiyo.

Sanduku hilo likoje..(kiuhalisia)

Bruce Blair, mwanachama mstaafu wa kundi la timu ya kutekeleza shambulio la nyuklia nchini Marekani , awali alielezea BBC , kwamba tofauti na jinsi watu wanavyoamini,

sanduku hilo la Nyuklia halina kitufe ama nambari za siri zinazomwezesha rais kutekeleza shambulio la nyuklia moja kwa moja , na badala yake itifaki za shambulio hilo ni sharti awasiliane na washauri wa ngazi za juu.

"Katika sanduku hilo pia kuna mchoro wa mpango wa vita , malengo yake pamoja na idadi ya watakaofariki bila kusahau silaha zilizopo.
''Hivyobasi ni rahisi kuelewa hali ilivyo katika sekunde chache'', alisema Blair.

Ndani ya sanduku hilo si nambari za siri pekee za kutekeleza shambuliko hilo la uharibifu , pia kuna vitabu viwili.

Kimoja kina maelezo ya kina kuhusu aina ya shambulio hilo la nyuklia ambalo linaweza kutekelezwa na orodha nyingine ya maeneo salama kwa rais wa Marekani na familia yake kujificha.

Wakati mwingi sanduku hilo huonekana na antena iliojitokeza ambayo hutumika kuimarisha mawasiliano ya moja kwa moja na idara ya ulinzi The Pentagon.

Hitimisho.

Mataifa yanayofahamika kwamba yana vibeg ni.. U.S.A na Russia.

U.S.A kibeg chake kinaweza kuripua hii dunia ndani ya lisaa 🤔🤔, narudia "Only one hour".
 
_116614686_caf030f0-6b59-49e6-967d-0dbfba41ca75.jpg
 
Back
Top Bottom