Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi: Tanzania kuboresha mazingira rafiki ya Biashara nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,675
851
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi: Tanzania kuboresha mazingira rafiki ya Biashara nchini

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Tanzania imechukua hatua mbalimbali kuboresha mazingira rafiki ya Biashara nchini.

Rais Dk. Mwinyi amesema hayo wakati akizungumza na Wafanyabiashara, Wawekezaji wa Tanzania na Wadau wa Bandari za Tanzania jijini Bujumbura nchini Burundi.

Amewakaribisha Wawekezaji kuwekeza Zanzibar katika sekta mbalimbali zikiwemo Rasilimali za Utalii, Mafuta na Gesi, Uvuvi na Kilimo cha Mwani kupitia Sera ya Uchumi wa Buluu.

Rais Dk. Mwinyi amesema hayo wakati akiwa nchini Burundi akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Jamhuri ya Burundi zilizofanyika tarehe: 01 Julai, 2022.

IMG-20220701-WA0021.jpg
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom