Rais Biden amtunuku nishani ya heshima askari aliyekaidi amri katika uwanja wa vita Vietnam

Juma Wage

Member
Sep 8, 2023
60
201
USIKU wa June 18, 1968 Karibu na Kijiji cha "Go Cong" kusini mwa Vietnam, Luteni Usu wa jeshi la Marekani akiendesha helikopta ya Mashambulizi aina ya G- Cobra yenye mruko namba AH1 alipokea taarifa ya kuombwa msaada kupitia simu ya upepo (Radio call).

"Tumezungukwa.....tumezungukwa....tunashambuliwa....tunaomba msaada" ilisikika sauti kutoka kwa wanajeshi wenzie waliokuwa wakishambuliwa na wapiganaji wa Vietnam.

walikuwa askari wanne wa kimarekani waliozungukwa na wapiganaji zaidi ya 100 wa kivietnam.

Giza totoro lililotanda angani lilimfanya Taylor ashindwe kung'amua eneo sahihi walipo askari wenzake waliokuwa wakiomba msaada.

Aliwajibu kupitia simu ya upepo "Fyatueni fataki hewani ili nifahamu eneo sahihi mlipo."

Taylor akiwa na msaidizi wake waliruka umbali mrefu katika eneo hatari lililosheheni vikundi vya wapiganaji vyenye uchu dhidi ya askari wa kimarekani mithili ya fisi aviziaye mkono wa binaadamu.

Walisafiri kwa mruko wa chini, lengo kubaini mahali walipo wenzao wakati huo helikopta ikiwa imesalia kiwango kidogo cha mafuta.

Kwa mujibu wa wataalamu wa Medani za kivita wanasema "Uwezekano wa Taylor kuwaokoa askari wenzake ulikuwa mdogo kama ngamia kupenya kwenye tundu la sindano."

Taylor aliamini hawezi kuwaacha wapiganaji wenzake wakiangamia.

Wakiwa angani, risasi za maadui ziliigonga helikopta na kumlazimu Taylor kubadili mbinu za kimedani kwa kuwasha taa kuwatamanisha maadui wajikite kuishambulia helikopta ili waache kuwashambulia askari wenzake.

wakiwa kwenye Mashambulizi makali, Taylor alipata ushujaa wa kuishusha helikopta hadi eneo waliokuwepo askari wenzake wanne.

Askari wale waliidandia miguu ya helikopta kwa haraka, Taylor aliirusha helikopta hadi eneo salama.

Wakati yote akiyafanya, Taylor alikwisha pokea ujumbe kupitia simu ya upepo ukimtaka airejeshe helikopta kambini na asithubutu kuwaokoa wenzake kwa sababu helikopta hiyo haijatengenezwa kufanya oparesheni za Maokozi.

Septemba 05, Mwaka huu baada ya kupita miaka 55 tangu kutokea tukio hilo, Rais wa Marekani Joe Biden amemtunuku Taylor (81) Nishani ya juu ya kijeshi kutambua mchango wake katika vita ya Vietnam.

Ndimi Juma Wage
Dodoma
September 09, 2023.

IMG-20230908-WA0057.jpg
IMG-20230908-WA0044(1).jpg
 
USIKU wa June 18, 1968 Karibu na Kijiji cha "Go Cong" kusini mwa Vietnam, Luteni Usu wa jeshi la Marekani akiendesha helikopta ya Mashambulizi aina ya G- Cobra yenye mruko namba AH1 alipokea taarifa ya kuombwa msaada kupitia simu ya upepo (Radio call).

"Tumezungukwa.....tumezungukwa....tunashambuliwa....tunaomba msaada"ilisikika sauti kutoka kwa wanajeshi wenzie waliokuwa wakishambuliwa na wapiganaji wa Vietnam.

walikuwa askari wanne wa kimarekani waliozungukwa na wapiganaji zaidi ya 100 wa kivietnam.

Giza totoro lililotanda angani lilimfanya Taylor ashindwe kung'amua eneo sahihi walipo askari wenzake waliokuwa wakiomba msaada.

Aliwajibu kupitia simu ya upepo "Fyatueni fataki hewani ili nifahamu eneo sahihi mlipo."

Taylor akiwa na msaidizi wake waliruka umbali mrefu katika eneo hatari lililosheheni vikundi vya wapiganaji vyenye uchu dhidi ya askari wa kimarekani mithili ya fisi aviziaye mkono wa binaadamu.

Walisafiri kwa mruko wa chini, lengo kubaini mahali walipo wenzao wakati huo helikopta ikiwa imesalia kiwango kidogo cha mafuta.

Kwa mujibu wa wataalamu wa Medani za kivita wanasema "Uwezekano wa Taylor kuwaokoa askari wenzake ulikuwa mdogo kama ngamia kupenya kwenye tundu la sindano."

Taylor aliamini hawezi kuwaacha wapiganaji wenzake wakiangamia.

Wakiwa angani, risasi za maadui ziliigonga helikopta na kumlazimu Taylor kubadili mbinu za kimedani kwa kuwasha taa kuwatamanisha maadui wajikite kuishambulia helikopta ili waache kuwashambulia askari wenzake.

wakiwa kwenye Mashambulizi makali, Taylor alipata ushujaa wa kuishusha helikopta hadi eneo waliokuwepo askari wenzake wanne.

Askari wale waliidandia miguu ya helikopta kwa haraka, Taylor aliirusha helikopta hadi eneo salama.

Wakati yote akiyafanya, Taylor alikwisha pokea ujumbe kupitia simu ya upepo ukimtaka airejeshe helikopta kambini na asithubutu kuwaokoa wenzake kwa sababu helikopta hiyo haijatengenezwa kufanya oparesheni za Maokozi.

Septemba 05, Mwaka huu baada ya kupita miaka 55 tangu kutokea tukio hilo, Rais wa Marekani Joe Biden amemtunuku Taylor (81) Nishani ya juu ya kijeshi kutambua mchango wake katika vita ya Vietnam.

Ndimi Juma Wage
Dodoma
September 09, 2023.

View attachment 2744148View attachment 2744149
Safi sana hii....
 
Gold Citizen
 
Back
Top Bottom