VIETNAM WAR UNSUNG HEROES: Kutana na komando wa Marekani aliyenusurika kuzikwa akiwa hai. Alimtemea daktari mate usoni akiwa ndani ya begi la maiti

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
VIETNAM WAR UNSUNG HEROES: Kutana na Komando wa Marekani aliyenusurika kuzikwa akiwa hai. Alimtemea daktari mate usoni akiwa ndani ya begi la kubebea maiti.

images (3).jpeg


Roy Benavidez pia anajulikana kwa jina la Raul Perez Benavidez alizaliwa mnamo tarehe 5 Agosti mwaka wa 1935 katika mji mdogo wa Texan. Baba yake, mkulima wa huko Mexico, alikufa kutokana na ugonjwa wa kifua kikuu wakati Roy alikuwa bado mtoto mdogo sana wa miaka miwili.

Miaka mitatu baadaye, mama yake mzazi pia alikufa kwa sababu hizo hizo za ugonjwa wa kifua kikuu. Roy na mdogo wake walichukuliwa na ndugu zao upande wa baba. Roy alienda shule mara kwa mara kwa sababu ilibidi afanye kazi kwa bidii sana ili aweze kujisimamia yeye pamoja na mdogo wake. Alipokuwa na umri wa miaka 15, aliamua kuacha shule ili aweze kufanya kazi kwa muda wote.

Mnamo 1952, Roy Benavidez, kijana mdogo mwenye umri wa miaka 17, aliingia kwenye Jeshi la Marekani, na miaka mitatu baadaye akaanza kutumika na kupewa mkataba wa kudumu. Mnamo 1959, baada ya kumaliza mafunzo ya askari wa anga, alipangiwa kituo kipya cha kazi huko Fort Bragg, North Carolina.

Alijiunga na Kikosi Maalum cha Wanajeshi na kuwa sehemu ya Kikosi cha Masomo na Utambuzi (Studies and Observations Group) kilichotambuliwa sana ambacho kiliendesha shughuli za vita ya kimyakimya (covert operation) siku za kabla na wakati wa Vita vya Vietnam.

Mnamo mwaka wa 1965, alipokuwa kwenye kazi pevu huko Vietnam Kusini, kwa bahati mbaya akakanyaga bomu la kutegwa ardini, kisha kulipuka na kujeruhiwa vibaya sana. Madaktari wake walihitimisha ya kwamba hatatembea tena. Kinyume na matarajio ya watu - na maagizo ya madaktari - Roy aliamua kutokukata tamaa.

Kila usiku, alikuwa akitoka kitandani mwake, na kutumia kidevu na viwiko vyake na kutambaa mpaka kwenye ukuta wa karibu, na kuanza kunyoosha vidole vyake kujaribu na kuinuka.

Alirudia mchezo huu kwa zaidi ya mwaka mmoja, akiungwa mkono na kupewa msaada na wagonjwa wenzake. Usiku wa jasho na machozi ulimalizika naye akitoka hospitalini mnamo mwezi Julai mwaka 1966. Hakuna mtu ambaye angeweza kudhania ya kuwa haya ni mafanikio ya mwanzoni tu kwa upande wa bwana Benavidez.

Miezi sita baadaye alikuwa amerudi Vietnam ya Kusini. Mnamo mwezi Mei mwaka 1968, Roy alikuwa katika uwanja wake wa vita huko Loc Ninh, karibu na mpaka wa Cambodia. Ilipofika saa 1:30 usiku walipokea simu ya dharura.

Doria ya Vikosi Maalum ya askari 12 ilionekana na kundi la askari wa miguu (Infantry Battalion) wa Jeshi la Watu wa Vietnam. Baadae ikaja kugundulika walikuwa karibu elfu moja. Helikopta tatu zilijaribu kuwaokoa, lakini zilirudishwa nyuma na wanajeshi wa adui zikiwa zimeharibiwa pamoja na watu kubeba watu waliojeruhiwa.

Sergeant Benavidez alijitolea kushiriki katika jaribio lingine. Kama Rais Ronald Reagan alivyotoa maoni yake kwa kusema, ikiwa kile kilichotokea kingeweza kupigwa picha kamwe hakuna mtu ambaye angeweza kuamini macho yake.

Yaaani Helikopta ilikuwa ikiruka kwenye msitu mnene na wakati ilipokuwa ikizunguka kwa umbali wa kama futi 10 kutoka ardhini, Benavidez akaruka nje ya helicopter, akiwa amebeba begi la dawa na kisu tu. Kudadadeki.

images (6).jpeg


Alikimbia umbali wa kama yadi 75 kuelekea kwa wenzake waliojeruhiwa na kwa kufanya hivyo alipigwa na risasi ya AK-47 na kisha tena na kupigwa na vipande vipande kutoka kwenye grenade (bomu la mkono). Alipofika kule alikokwenda, uso wake, kichwa pamoja na mguu wa kulia vilikuwa vimejeruhiwa. Jamaa zake wanne walikuwa wamekufa, wakati wale 8 waliobaki walijeruhiwa na hawakuweza kusonga mbele.

Licha ya maumivu makali, aliwavuta karibia na helikopta ya uokoaji. Mission karibia kukamilika, alikimbia mara ya mwisho kuchukua mwili wa kiongozi wa timu aliyekufa pamoja na hati kadhaa za siri sana (Classified Documents)

Wanajeshi wa Vietnam (NVA) walizidisha sana mashambulizi na hatimaye akapigwa risasi ya tumbo, na mara nyingine tena akapigwa na vipande vipande vya mabomu. Wakati huo huo, rubani wa ndege ya helicopter aliuawa na helikopta yenyewe ikaanguka. Balaaaaa

images (5).jpeg


Wakati utumbo wake ukiwa nje, Benavidez alichukua hati hizo na akarudi nyuma kwenye mabaki ya helicopter ili kuwasaidia waliojeruhiwa na kujaribu kuwapanga katika eneo la kujihami. Hatimaye alifanikiwa kwa juhudi zake. Alifanikiwa kuita mashambulizi ya fighter jets pamoja na helikopta nyingine ya uokoaji kutumwa.

Wakati wa kutoa msaada wa huduma ya kwanza kwa mmoja wa askari wenzake, alipigwa risasi tena. Aliendelea kusonga mbele. Helikopta ya uokoaji ilifika na alianza kupeleka askari eneo salama.

images (7).jpeg


Katikati ya yote hayo, wakati alikuwa amembeba askari aliyejeruhiwa vibaya sana, alichomwa na kitu chenye ncha kali (Bayonet/Singe) kutokea kwa nyuma na askari aliyeonekana kuwa amekufa wa NVA.

Taya ikiwa imevunjika, alikuwa anakaribia kufa na kuchomwa na bayonet ya adui. Haraka akashika kisu kikali, akamvuta yule askari wa NVA na kumpiga na kisu shingoni. Lakini, hiyo ni baada ya bayonet kutikiswa kulia kupitia mkono wake wa kushoto.

Na kila mtu akiwa kwenye helicopter, alichukua AK-47 na kuwaua askari wengine wawili wa NVA kabla ya mwishowe kuwaruhusu washiriki wa kikundi chake kumvuta ndani ya helikopta. Mapigano ya masaa sita yalikuwa yamekwisha. Wakati walipofika kwenye ngome, mwili wa Benavidez haukuweza kutembea.

Walisema amekufa na kuwekwa kwenye begi la plastiki. Kwa bahati nzuri, mmoja wa marafiki zake alimtambua na mara moja akapiga simu kwa daktari. Begi lilikuwa likijaa damu haraka sana aisee. Na risasi 37, vipande vipande vya mabomu pamoja na majeraha ya bayonet, macho yaliyotapakaa damu, na hakukuwa na dalili ya mapigo ya moyo, daktari alihitimisha kuwa Benavidez amekufa kweli.

Lakini hakuwa amekufa. Hakuweza kusonga au kuongea, ila alifanikiwa kufanya kitu kimoja tu - akatema mate kwenye uso wa daktari.

Mara moja alihamishwa kurudi katika Kituo chake cha matibabu ambapo alipona. Kwa ushujaa wake mkubwa, alipewa nishani ya juu sana.

Ninauza Vitabu Vya Kujifunzia Lugha Ya Kijerumani. Ich komme aus der Stadt Dar Es Salaam und verkaufe diese Deutsch-Lernbücher

KUMBUKA: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
When you have

nothing to do
Nothing to worry about
Maumivu huyasikii tena
Macho yamezibwa na damu
Mapafu yamejazwa hewa chafu iliyochanganyikana na vumbi na moshi
just hopes and faith. Kongole masoja mliopitia hali kama hizo
images (10).jpg
 
Ila wamarekani wanajikuza sana kwenye vita ya vetnam kwa story zisizo na ushahidi.. ila hawaelezi sababu kwa nini walikimbia uwanja wa vita huku vita ndio kwanza ilikuwa imenoga.


Wanadanganya maandamano ya wananchi marekani ndio sababu waondoke vitani.. ila hii sababu weak sana.. yaani upo vitani na adui bado hujamshinda unakimbia uwanja wa vita kisa maandamano kweli.

Inasemekana walikimbia baada ya kugundua wa vetnam hawaishi hata uuwe wengi kiasi gani
 
Story za Majeshi ya Marekani zina uwongo mwingi .

Osama Bin Laden wamemzika maharini
Shambulio lake wamelitengenezea Makumbusho.
 
Ila wamarekani wanajikuza sana kwenye vita ya vetnam kwa story zisizo na ushahidi.. ila hawaelezi sababu kwa nini walikimbia uwanja wa vita huku vita ndio kwanza ilikuwa imenoga.


Wanadanganya maandamano ya wananchi marekani ndio sababu waondoke vitani.. ila hii sababu weak sana.. yaani upo vitani na adui bado hujamshinda unakimbia uwanja wa vita kisa maandamano kweli.

Inasemekana walikimbia baada ya kugundua wa vetnam hawaishi hata uuwe wengi kiasi gani
nikajua una full fact kuhusu Vietnam war..
baadae unatia neno"" INASEMEKANA"..
kumbe na wewe huna uhakika na unachotaka kukisema hapa.

Bored

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom