Mkuu pamoja na hayo mimi nilidhani uwepo wa "wabunge wa viti maalum" ni kutetea maslahi & ustawi wa wanawake & watoto ktk mijadala ya Bunge! Kumbe ni kodi zetu zinaliwa bure tu kwa maslahi ya Vyama vilivyowateua!! Nilitarajia wabunge wote wanawake na hasa wale wa viti maalum wasimame kidete kutaka uchunguzi yakinifu mapema iwezekanavyo!!!
Nakubaliana na wewe kabisa. Kama Viongozi wanawake walio kwenye uongozi wa juu wamegeuka 'jiwe', basi hawa wabunge wanawake walioingia bungeni kwa mgongo wa 'jinsia' wangeonesha wapo bungeni kutetea UTU na haki ya mwanamke.
Takribani 36% ya wabunge ni wanawake, kama sikosei wabunge hawa (bila ya kujali vyama vya siasa) wamejiwekea uongozi. Huyo kiongozi yuko wapi? Na huo umoja wa wabunge wanawake unamsaidia nini huyo binti ambaye anatumikia kifungo cha maisha kinachohusishwa na mbunge mwenzao? Where is justice kwa huyu binti?
Ni vema pia tukaangalia wabunge wanaume. Kapuya atakuwa amedhalilisha wanaume wote na hasa wabunge wote wanaume wa Tanzania. Kuhusishwa na unyama wa aina huu kunaleta sura mbaya sana, na nilitegemea wabunge wanaume walaani unyama huo. Kukaa kimya kunaleta picha kwamba Paedophilia inakubalika. Wabunge wanaume wanatakiwa watoe kauli kwenye hili.
Hatuwezi kuongelea ustawi wa Taifa kama watoto wanageuzwa kuwa sex-slave wa wakubwa, with impunity. Na inaleta hasira kusoma comment zinaelekea kumlaumu huyu binti! Huku ni sawa na kumpa victim hukumu ya kifo kwa mara ya pili.
Jeshi la Polisi nalo ni la kuungalia. Hawa ni law-enforcement agent. Wako wapi? Kwa kifupi, the entire system has failed this young girl!
Kwa kumalizia, maana viongozi wanaonekana kuwa na kigugumuzi kwenye hili, watanzania wote na hasa wazazi (bila ya kuingalia itikadi) wanatakiwa walaani kitendo cha kiongozi kutumia utajiri na nafasi yake kumpokonya binti wa miaka 14 HAKI yake ya msingi ya kuishi bila ya kadhia ya magonjwa yasiyotibika. Alienda kumuona huyo mbunge akitegemea kupata msaada wa kuwekeza kwenye maisha yake, badala yake kaachiwa ukimwi!
Sieweli ni kwanini hadi dakika huyu bado ni mbunge na anazurura babarani? Hivi zile Jumuiya za wazazi zipo? Ukitaka kujua nchi inaelekea wapi, angalia jinsi inavyotunza/wekeza kwa watoto wake. Tanzania tunaelekea wapi?