Bangi ni tiba kama zilivyo tiba nyingine za mitishamba,matibabu yake yangewekwa wazi na wataalamu wa tiba.
Matumizi ya bange kwa uvutaji kama sigara yanaweza yakawa ni sababu mojawapo inayoficha matumizi mengine makubwa ya mmea huo.
Asilimia kubwa ya nguvukazi hasa katika uvuvi ,migodini, mashambani na kazi zozote ngumu,vijana wengi wanatumia bange.
Kuhalalisha matumizi ya bange si tu kunahitaji haraka, bali umakini mkubwa na pengine tuwahusishe viongozi wetu wa dini walau watoe ushauri wao.
Matumizi ya gongo kwa Tanzania sio kitu cha ajabu Sana kwani karibu vijiji vyote na maeneo ya watu wa hali ya chini mijini watu wanatumia gongo kama ambavyo tunavyowaona wenzetu wazungu wanavyotumia pombe kali, wine n.k
Kama formula ni ile ile inayotumika kutengeneza vileo vikali tofauti labda ni purification na kuondoka harufu kali,basi ufanyike utaratibu mahsusi wa kuwatambua watengenezaji wote ili wapewe elimu juu ya namna ya kuboresha kinywaji hicho ili kitumike kuinua uchumi wa familia zao na Taifa.
Yawezekana kabisa kuwa hizi pombe zinazotengenezwa kienyeji zikawa ni nzuri zaidi kiafya kuliko pombe zinazotambulika sokoni.