Rai: Bangi na gongo vihalalishwe

Rai: Bangi na gongo vihalalishwe

na ikishakua binafsi maana yake hawa wamama muuza waliopo kwa mamia mitaani watafaidikaje na hiyo transition ya gongo production kama serikali itaamua kumonopolize hiyo sector ya gongo inayoajiri mamia lakini inateketeza maelfu.
Hapana hawa wote watapata mafunzo na kuajiriwa huko kumbuka kuna kukusanya malighafi kuchakata kuzalisha kuhifadhi kusambaza kuuza kwa jumla na rejareja hivyo ajira zitakuwepo hapo
Hii yangu ni rai tu utekelezaji wake unataka mipango thabiti na umakini
 
Kama una uhakika na madai yako kuhusu Polisi kuhusika na uchukuaji wa "chochote" basi nakushauri uende uonane na Viongozi wao utoe taarifa yako ya kina ili hatua stahiki zichukuliwe vinginevyo itakua ni majungu tu.Pia km unadhani banghi na gongo vihalalishwe je mwanao au wewe mwenyewe ni watumiaji wa hivyo vitu?Isije ikawa Kama baadhi ya Viongozi wa wanatetea ushoga wakati wao wala familia zao hawapendi kabisa wajihusishe na ushoga.
 
Kuendelea kutozitambua hizi bidhaa ni kuendelea kupoteza ajira nyingi na mapato mengi mengi
Tafiti nyingi zimethibitisha kuwa bangi ikitumiwa kwa kiwango cha chini ni tiba kwa magonjwa mengi hata kwenye ushirikina
Vile vile Vinywaji vingi vikali formula zake haitofautiani na gongo kwanini tusiwekeze huku?
Na uchumi ulivyobana bwashee,,. Bia hazinunuliki.
 
Nimeiona tayari.

Ila ujue wakishaiboresha kama unavyoshauri haitakua tena ikiuzwa 100 au 200 kama ilivyosasa bali inaweza kuwa 500 kutokana na gharama za uendeshaji ikiwemo vifungashio tena hapo ndio inaangukia kwenye banana na viroba majanga mapya muonekano tofauti.
Unapoboresha kitu ni lazima thamani yake ipande hilo halina ubishi na kama taifa Tunahitaji kuwa na standards kwenye kila kitu
Vitu vingi tu mbona vinapanda bei na bado watu wananunua? Tulenge kwenye ubora tusihofie gharama
 
Hata mimi nakubaliana na wewe, waruhusu pia Malaya kujiuza ili mradi wawekewe utaratibu wa kupimwa mara kwa mara na kulipa kodi, kwa hili nadhani tutapata uungwaji mkono wa baadhi ya wabunge wa ccm akiwemo msukuma
Si kila kitu ni siasa Ndugu.
 
Kuendelea kutozitambua hizi bidhaa ni kuendelea kupoteza ajira nyingi na mapato mengi mengi
Tafiti nyingi zimethibitisha kuwa bangi ikitumiwa kwa kiwango cha chini ni tiba kwa magonjwa mengi hata kwenye ushirikina
Vile vile Vinywaji vingi vikali formula zake haitofautiani na gongo kwanini tusiwekeze huku?
Ni kweli mkuu kama paraguai wamehalalisha bangi
 
Watanzania hatuendelei sababu ya unafiki na uvivu wa kufikiria hiyo bangi ikiruhusiwa itaoNgeza pato na ajira kwa vjana wengi kuliko mrad wowote ule wa kutoa ajira
 
Tutegemee mazao ya chakula kupungua na kilimo cha bangi kuongezeka kwa kasi kwa vile watuamiaji tupo wengi tu sana
 
Hata serikalini wapo waliouza gongo makwao na wapo waliosomeshwa kwa kipato konachotokana na gongo na bange
 
1474042534148.jpg
1474042538231.jpg
tayari mitaani kuna mitambo mizuri kabisa inayoweza kutengeneza mpaka nembo za mamlaka ya mapato na kuchapisha logo ya brand fulani
Hawa watu wanapaswa tu kuelimishwa ili watengene logo yao
 
kitu cha ara ni poa ila nadhani sio kila mtu ana kiasi, hii kitu inakuaga kama transition to ilicit drugs
 
Bangi ni tiba kama zilivyo tiba nyingine za mitishamba,matibabu yake yangewekwa wazi na wataalamu wa tiba.
Matumizi ya bange kwa uvutaji kama sigara yanaweza yakawa ni sababu mojawapo inayoficha matumizi mengine makubwa ya mmea huo.
Asilimia kubwa ya nguvukazi hasa katika uvuvi ,migodini, mashambani na kazi zozote ngumu,vijana wengi wanatumia bange.
Kuhalalisha matumizi ya bange si tu kunahitaji haraka, bali umakini mkubwa na pengine tuwahusishe viongozi wetu wa dini walau watoe ushauri wao.
Matumizi ya gongo kwa Tanzania sio kitu cha ajabu Sana kwani karibu vijiji vyote na maeneo ya watu wa hali ya chini mijini watu wanatumia gongo kama ambavyo tunavyowaona wenzetu wazungu wanavyotumia pombe kali, wine n.k
Kama formula ni ile ile inayotumika kutengeneza vileo vikali tofauti labda ni purification na kuondoka harufu kali,basi ufanyike utaratibu mahsusi wa kuwatambua watengenezaji wote ili wapewe elimu juu ya namna ya kuboresha kinywaji hicho ili kitumike kuinua uchumi wa familia zao na Taifa.
Yawezekana kabisa kuwa hizi pombe zinazotengenezwa kienyeji zikawa ni nzuri zaidi kiafya kuliko pombe zinazotambulika sokoni.
 
Back
Top Bottom