Rahma Al Kharoos anatafuta Ubunge?

hamuongei chochote hapa, mnafichaficha nini kama mambo mnayoongea ni ya kweli? ongeeni openly kama kitu ni cha kweli, sisi wengine hata hatujajua mnaongelea nini haswa.
 
............Kumbe huyu mama ni mke mdogo wa rais mhhh mbona kazi. Kama ni kweli basi kazi ipo.
 
Sasa kila Mtu akitaka ainngie mjengoni, kwa staili hii nani tena atakuwa pembeni??

26870_116830848335861_100000268407034_219550_6693419_n.jpg






HAWA WATU WAPO VERE VERE STRATEGIC...





shy+2.jpg
Ngoswe picha ya juu kabisa mmh inakuwaje? wapi hapo? mbona vivazi vinaacha sehemu za kulishia watoto nje? (huyo haonekani sura ila....) wapi hapo? tukio lipi? valentine? mbona maua?
 
nadhani tumesahau kuwa uzuri wa nyumba kwa nje si usafi wa ndani
heheee hata hivyo kuna haja ya kuwa makini,

ni nani aupandaye mdizi? tena asile matundaye?
 

Toka kushoto ni balozi wa Palestina nchini, Mh Yusuf Habab,
Balozi wa Saudi Arabia nchini mh Al-Jarbuo Ali,Mwenyekiti wa kampuni ya mafuta ya Noor Oil-Industrial technology,Mama Rahma Al kharoos al kharoos, Najey Al Haram pamoja na Bw.Ali


Source: Michuzijr

Is she Tanzanian?
 
Wakubwa, mnaongea kwa mafumbo hivi mwadhani ni wote tunaishi Tz na hizi kampeni twazishuhudia? Twambieni ni nani huyo kumbukeni "where we dare talk openly" sasa mafumbo ya nini? Hivi huyu binti wa Bhanji si ameolewa na Msanii mmoja hapo Bongo?
 
............Kumbe huyu mama ni mke mdogo wa rais mhhh mbona kazi. Kama ni kweli basi kazi ipo.


Kumbe sikuwa peke yangu!! Hata mimi nilikuwa najiuliza alikotokea huyo mrembo na kuanza kumwaga mafweza kama hana akili!! Sasa dot zangu zimesogea kidogo!

Ila mkulu ni hatari sana wa kutafuta vimwana, ...sifa ya kwanza ni ile inayowatesa wasukuma!! Angekuwa anatokea Nasa angekomba mazizi yake yoote...

Mhhhhh, ....Mombo ngafu!!!
 
Twiga Stars yachangiwa mil. 37
18 Dec 2007
By Somoe Ng\'itu
Jumla ya Sh. Milioni 37 juzi usiku ziliahidiwa kutolewa na watu mbalimbali kwa ajili ya kuipatia timu ya soka ya taifa ya wanawake, Twiga Stars ambayo imefanikiwa kusonga mbele katika mashindano ya kutafuta nafasi ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake.

Twiga Stars imefuzu hatua ya pili baada ya kuifunga Eritrea kwa jumla ya mabao 4-2 katika mashindano hayo.

Akitangaza ahadi hizo, mlezi wa timu hiyo ambaye ni mwenyekiti wa kampuni ya Noor Oil & Industrial Technology (T) Ltd, Madame Rahma Al Kharoos aliwataka wachezaji wa timu hiyo kuendeleza juhudi walizozianza na kusema kuwa mafanikio yao yatathaminiwa.

Madame Rahma alisema kuwa wote wanafahamu ugumu wa kuiandaa timu na yeye amekubali kuwa mlezi wa timu hiyo ili kuweza kusaidiana na viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, kutafuta fedha zaidi.

Aliwataja walioahidi kutoa fedha hizo kuwa ni pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba aliyeahidi Sh. Milioni 20, Superdol Sh. Milioni 3, Scandinavia Sh. Milioni 2, hoteli ya Paradise Sh. Milioni 2, familia ya Kapinga Sh. Milioni 1.5 na Mkurugenzi wa Masoko na Udhamini wa Vodacom Sh. 300,000.

Pia mlezi huyo ameahidi kuanzisha mfuko wa kuiandaa timu hiyo utakaoanza na kiasi cha Sh. Milioni 100 kabla ya kwenda katika mechi ya hatua ya pili dhidi ya Cameroon.

Mechi hiyo ya pili itachezwa mapema mwezi Februari mwakani na Twiga Stars wataanzia hapa nyumbani.

Rais wa TFF, Leodegar Tenga aliwapongeza wachezaji hao kwa ushindi huo na kuongeza kuwa walichokifanya ni wazi kuwa walikuwa wamefuata maelekezo ya walimu wao.

Wengine waliohudhuria sherehe hiyo ni pamoja na Kiongozi wa mabalozi wote, Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Juma Mpango na katibu mkuu wa Shirikisho la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye.
* SOURCE: Nipashe
Mnamuonea huyu dada. Kumbe alianza zamani kuchangia soka la wakina mama!

Amandla....
 
Tatizo si kugombea...bali namna atakayotumia kugombea ili apate uongozi naona inamatatizo...ameshaanza kumwaga fedha na hatari yote ipo hapa, kama atagombea on her own merit, mi sina tatizo kabisa...yatakayobakia ni majungu tu.
 
Back
Top Bottom