Tatizo la wadanganyika wengi ni wivu, chuki, fitina, uroho, upumbavu, ujinga n.k.
Kwani mtu kuwa na pesa zake na kuutaka ubunge ni kosa? Mbona Mzee Ndesa ni bilionea na bado ni mbunge? Mbona mama Lwakatare ni bilionea na bado ni mbunge? Wakili Mkono na wengine wengi ni mamilionea wa kutupwa na bado wanang'ang'ania ubunge sembuse huyo al hadoud? Chuki zenu zinawapeleka pabaya na hasa pale mnapozionyesha hadharani kuhusu mtu fulani au jamii fulani au kikundi fulani.Leo mnalilia maximo mwingine wakati pesa za kumlipa zinatoka ikulu,kwanini msiamue kuchangia wenyewe na kumlipa ili hizo za ikulu zinunue madawati?
Amejitokeza mwanamama shupavu wa kuchangia taifa lake katika michezo mnaanza ooh ushuzi, kajamba mtakufa bure na vijiba vya roho.Acheni ujinga fanyeni kazi na si kufuatilia mambo ya watu,taifa masikini kwa mtaji huo lazima mtaendelea kuwa masikini wa kutupwa na kutawaliwa kila siku. Najua hapo angekuwa anatoa misaada yule ambaye si miongoni mwa mliyetumwa kuwatenga katika mipango yenu basi mngeanza kumsifia yule anafaa sana.
Upumbavu huo hautoisha hadi mbadili yaliyomo katika vifua vyenu. Nimekumbuka mhanga mmoja alisema "La kama mngeyajua yaliyomo vifuati mwao wala msingewafanya hao kuwa marafiki na vipenzi vyenu", sasa chuki zao zimeanza kujionyesha hadharani.
Ukichukia chukia kwasababu huniongezei siku za kuishi hapa duniani,muda wangu ukifika nitajifia na si kuendekeza ujinga na upuuzi wa aina hiyo.
Mungu ibariki Tanzania.
Ndo udhaifu wake huo,
Wanawake jitokezeni mgombee kwenye chaguzi hizi.Akijitokeza Al Kharoos nampa kula yangu.Sijui nimtafute wapi nimfanyie kampeni.!
Ahhhhh bwana kwenye week 2 Mh Rahma Al kharoos al kharoos ametumia Mil 22 kwenye publicity ...10 mil netball na Ridhiwani akiwepo na tena 12 Mil kwa Wazuri (Miss) intercolllege...Hizi pesa zina nunua madawati mangapi.....hawa wanasiasa hawajuai sehemu za kupeleka pesa zao. Mimi hapo ningejenga Dispensary kule anakotekea Balatanda ama kwa kina Manyoya wa Ngoswe
The Following User Says Thank You to Masanilo For This Useful Post:
aah mkulu yupo makini atampatia hata uwaziri baada ya kumteua km mbunge wa kuteuliwa......tanzania inaliwa na wenye meno!!Mkulu kwanini asimpe ukuu wa Mkoa ama wa wilaya naona Ubunge watu weshaanza mambo yao!
Waungwana, mtaniwia radhi kwa kutoonekana ukumbini kwa muda mrefu. Nimekuwa nikisoma alama za nyakati ili niweze kuja hapa na mada iliyosheheni hoja za nguvu, si nguvu za hoja.
Naanza kwa hili la Mke Mdogo wa Mkuu wa Kaya – nadhani wote mnamtambua, sihitaji kumtaja jina lake – ambaye hivi karibuni ameanza kampeni za wazi wazi, ikionekana dhahiri kwamba si kwamba anajinadi ili kuweza kupata umaarufu wa haraka haraka, lakini lengo lake haswa likiwa kuupata Ubunge wa Viti Maalum kupitia Chama Tawala.
Habari za ndani kutoka kwa wadau walio karibu naye zinadai kwamba mwanamama huyu machachari na mkorodi, ambaye inasemekana kwamba "haambiliki" hata kwa Mkuu wa Kaya mwenyewe, amepania naye kuukwaa Ubunge huo ili naye aingie "mjengoni" mwaka 2010, lakini kisichojulikana ni kwa malengo gani haswa yanayomsukuma kufanya hivyo. Licha ya kwamba mwanamama huyu ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kifedha – jambo ambalo amelidhihirisha wazi wazi – haieleweki ni kipi haswa anachokifuata "mjengoni" humo.
Duru za kisiasa zinasema harakati za mwanamama huyu zinaweza kuleta athari hasi kwa Mkuu wa Kaya, kwani zitasomeka kuwa harakati za kuigeuza hali ya kisiasa nchini hapa kuwa ya "kisultani", kwani, minong'ono inasikikika kwamba mwana wa Mkuu wa Kaya, ambaye ni Mjumbe wa NEC kupitia Wilaya ya Bagamoyo, naye pia yumo mbioni kujiandaa kugombea kuingia "mjengoni", ingawa hajatangaza rasmi nia yake hiyo.
Mwanamama huyu alianza kishindo cha kampeni zake siku chache zilizopita baada ya kumwaga kitita cha fedha taslim shilingi milioni 10, ambazo alihakikisha zinaonekana kwenye taarifa ya habari ya kituo cha luninga cha Channel Ten, ambacho ndicho kimekuwa karibu naye kwa wakati wote huu. Kitita hicho kilimwagwa kama "msaada" kwa timu ya soka ya wanawake, Twiga Stars, RK akitambulishwa kama "mdau wa soka ya wanawake", na kutambulishwa kwamba amekuwa akiichangia timu hiyo mara kwa mara. Jambo la kushangaza ni kwamba, ni zaidi ya mara moja timu hiyo imekuwa ikitembeza bakuli kwa wafadhili mbalimbali, lakini haikuwahi kusikika hata mara moja kwa mwanamama huyo – ambaye anaishi nchini Oman – kujitokeza kuisaidia, licha ya uwezo wake mkubwa wa kifedha.
Jitihada za mwanamama huyu kujinadi wazi wazi hazikuishia hapo, kwani, ni Jumapili ya wiki iliyoisha, alijitokeza kufadhili kinyanganyiro cha kuwasaka walimbwende wanaoshiriki kupitia shindano la Miss Inter College, ambao washindi wake watapata nafasi ya kuingia moja kwa moja kwenye shindano la Miss Tanzania 2010. Safari hii, dau la mwanamama huyu limeongezeka kufikia Shilingi milioni 12, akijinadi kupitia kampuni ya RBS Oil and Technology.
Tathmini yangu ni kama ifuatavyo.
Iwapo mwanamama huyu ataachwa kuendelea kufanya ayatakayo, huenda kambi ya Mkuu wa Kaya ikapata athari hasi, kwani harakati hizi zitaweza kuwa "mtaji wa kisiasa" (political capital) kwa kambi ya upinzani, wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010, jambo ambalo linaweza kuathiri vibaya matokeo ya kura zitakazovunwa na Mkuu wa Kaya
Duru za kisiasa zimezidi kudodosa na kusema kwamba, harakati za mwanamama huyu zinaweza kutafsiriwa kuwa ukandamizaji kwa wanawake kutokana na nafasi kubwa aliyonayo kama Mke Mdogo wa Mkuu wa Kaya, nafasi ambayo anaweza kuitumia ipasavyo kwani hakuna atakayeweza kumpinga wakati wa kinyang'anyiro hicho cha Ubunge kupitia Viti Maalum. Kampeni ya kusaka umaarufu kwa kutoa michango lukuki inasadikiwa kuwa ni kutaka kumwiga Mke wa Rais, ambaye tayari amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na mchango wake mkubwa kwa maendeleo ya wanawake na watoto, japokuwa Mke huyo hajaonesha nia ya kutaka kugombea nafasi ya kuingia "mjengoni"
Wadau wa masuala ya kisiasa wamemshauri Mkuu wa Kaya kumwita mwanamama huyo na kumkalisha, kasha kumpa karipio kali na amri ya kusitisha mara moja harakati zake hizo, kwani harakati hizo za kuutaka umaarufu zinaelekea kumwaga "mtama" na kuweka wazi mambo ya ndani ya "familia" yasiyopaswa kujulikana, jambo ambalo litaweza kuiweka kambi ya Mkuu wa Kaya kwenye wakati mgumu mara tu kipenga cha kampeni za Uchaguzi Mkuu kitakapopulizwa rasmi.
"Sio kwamba Mkuu wa Kaya anapendwa sana na wananchi wake, la hasha; sio kwamba wananchi wake wote watafurahi akirejea ulingoni, la hasha; itakuwa ni aibu akishindwa kurejea kwa sababu ya kukuru-kakara za mke wake mdogo", alishauri mdau mmoja wa kisiasa.
Nimepewa ujumbe niufikishe kwa Mkuu wa Kaya. Natumai utafika.
>>> Mchokonozi, Shujaa wa Kuchokonoa!
Sasa hii kweli haitazua ugomvi na yule wa Mawasiliano?
Tatizo la wadanganyika wengi ni wivu, chuki, fitina, uroho, upumbavu, ujinga n.k.
Kwani mtu kuwa na pesa zake na kuutaka ubunge ni kosa? Mbona Mzee Ndesa ni bilionea na bado ni mbunge? Mbona mama Lwakatare ni bilionea na bado ni mbunge? Wakili Mkono na wengine wengi ni mamilionea wa kutupwa na bado wanang'ang'ania ubunge sembuse huyo al hadoud? Chuki zenu zinawapeleka pabaya na hasa pale mnapozionyesha hadharani kuhusu mtu fulani au jamii fulani au kikundi fulani.Leo mnalilia maximo mwingine wakati pesa za kumlipa zinatoka ikulu,kwanini msiamue kuchangia wenyewe na kumlipa ili hizo za ikulu zinunue madawati?
Amejitokeza mwanamama shupavu wa kuchangia taifa lake katika michezo mnaanza ooh ushuzi, kajamba mtakufa bure na vijiba vya roho.Acheni ujinga fanyeni kazi na si kufuatilia mambo ya watu,taifa masikini kwa mtaji huo lazima mtaendelea kuwa masikini wa kutupwa na kutawaliwa kila siku. Najua hapo angekuwa anatoa misaada yule ambaye si miongoni mwa mliyetumwa kuwatenga katika mipango yenu basi mngeanza kumsifia yule anafaa sana.
Upumbavu huo hautoisha hadi mbadili yaliyomo katika vifua vyenu. Nimekumbuka mhanga mmoja alisema "La kama mngeyajua yaliyomo vifuati mwao wala msingewafanya hao kuwa marafiki na vipenzi vyenu", sasa chuki zao zimeanza kujionyesha hadharani.
Ukichukia chukia kwasababu huniongezei siku za kuishi hapa duniani,muda wangu ukifika nitajifia na si kuendekeza ujinga na upuuzi wa aina hiyo.
Mungu ibariki Tanzania.
Ahhhhh bwana kwenye week 2 Mh Rahma Al kharoos al kharoos ametumia Mil 22 kwenye publicity ...10 mil netball na Ridhiwani akiwepo na tena 12 Mil kwa Wazuri (Miss) intercolllege...Hizi pesa zina nunua madawati mangapi.....hawa wanasiasa hawajuai sehemu za kupeleka pesa zao. Mimi hapo ningejenga Dispensary kule anakotekea Balatanda ama kwa kina Manyoya wa Ngoswe
The Following User Says Thank You to Masanilo For This Useful Post:
Rais wa kampuni ya RBP OIL & INDUSTRIAL TECHNOLOGY (T) LIMITED,Mama Rahma Al Kharoos akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari waliofika leo katika Hoteli ya Movenpic wakati wa akitangaza udhamini wake wa Mil. 12 kwa ajili ya shindano la Miss Dar Inter College
Rais wa kampuni ya RBP OIL & INDUSTRIAL TECHNOLOGY (T) LIMITED,Mama Rahma Al Kharoos akikabidhi Hundi yenye Thamani ya shilingi Mil. 12
Huyu mwanamama amepewa maelekezo ya kujitangaza through michezo na sanaa.Lengo halikuwa ubunge kama walivyofikiri wengi bali anaandaliwa ulaji sehemu flani.Mkakati huo bado upo lakini unaweza kuathiriwa na uhusiano wake na Kikwete kutajwatajwa waziwazi.