Rafu mbaya uchaguzi CCM mkoa wa Morogoro

Ambakucha

JF-Expert Member
Aug 16, 2019
277
445
Mkoa wa Morogoro ulifanya uchaguzi wake wa kumpata Mwenyekiti wa Mkoa ambapo rafu mbaya akichezewa mgombea Nasoro Duduma aliyekuwa mmoja wa wagombea.

Baada ya uchaguzi huo uliyompa ushindi James Masunga, baadhi ya wajumbe walionekana kumwoneshea kidole Mbunge wa Morogoro Vijijini, Inocent Kalogalie na Mwenyekiti aliyekatwa jina, Bi Dorothi.

Inadaiwa, Inocent aliingia eneo la maegesho ya magari akiwa na kofia kibao na kuanza kuzigawa kwa wajumbe wa Morogoro Vijijini kisha ikasambazwa taarifa kuwa, anayegawa kofia hizo ni mgombea, Duduma ambaye alikuwa tayari ukumbini, hivyo baadhi ya wajumbe kuona kofia zinagaiwa kwa upendeleo au kwa minajili ya rushwa.
Baadaye ndani ya ukumbi, wakati wa kufungua kikao, Dorothi aliposimama alisema 'wajumbe wa Kilombero (ambao walikuwa wamesimama pia), Kilosa, Ulanga msiniangushe.'

"Ndipo wajumbe wa Kilombero ambao walisimama, wakaanza kuimba huku wakilitaja jina la James Masunga. Kinachoonekana, Dorothi ambaye ni mwenyekiti ni mstaafu na Inocent walishawaweka wajumbe wamchague Masunga na siyo Duduma.

"Kuna habari kwamba, Inocent kwa kuwa ni Mbunge wa Morogoro Vijijini na Duduma ni Mwenyekiti wa CCM Moro Vijijini, alimhofia akiwa wa mkoa, uchaguzi wa 2025 angemsapoti mtu anaitwa Mtigumba ambaye anaiva naye na kumwangusha yeye.

Kwa upande wa Dorothi, inadaiwa, Masunga ni mtu wake sana na amemuweka kiaina. Huyu Nasoro amepigwa zenge sana akiwa hajui, Watu wakitaka ukweli waende ndani ya geti la mahali ulipofanyika uchaguzi," alisema mjumbe huyo.
 
Back
Top Bottom