Rafiki yangu amekuwa tajiri mkubwa Dodoma, ninafuata njia zake. Tuzifuate

Unaweka 25m kupata 60m baada ya muda gani?
Kwa wazee wa kubeti tunasema hizo ni odds 2.7 ambazo ndani ya dakika chache tu bila kukanyaga jaruba hata moja la mahindi unaweza kuwa umetia kibindoni hio hela🤓🤓🤓
 
Kwa wazee wa kubeti tunasema hizo ni odds 2.7 ambazo ndani ya dakika chache tu bila kukanyaga jaruba hata moja la mahindi unaweza kuwa umetia kibindoni hio hela
Hahahah! (Bila kukanyaga jaruba hata moja)

Ila kilimo kina watu wake, kama mimi sipendi kabisa kilimo bora nifanye mambo mengine, Ila sababu nimeona waliofanikiwa kwa kilimo so nawapa moyo wote wakipendao.
 
Binafsi napenda kuweka wazi kabisa kuwa Mimi Sera yangu ni utajiri, ninahubiri utajiri tu. Tafadhali Kama wewe una mawazo ya kimaskini hii post inaweza kukuletea shida ya msongo wa mawazo.
Rafiki yangu yupo dodoma muda mrefu Sana tokea tumalize wote chuo kipindi hicho.
Kwao ni dodoma na alianza harakati za maisha hata kipindi tunasoma, tulipomaliza alikuwa tayari kwenye mstari na Sasa hivi ni tajiri mkubwa tu huko dodoma.
Huyu amepata pesa kwenye mahindi kule kibaigwa, ni mahindi tu hakuna kingine zaidi ya hicho kilichompa utajiri. Ila Sasa hivi ana vingine(Malori).
Unaweza kupita sehemu na kudharau kumbe ndipo pesa inapatikana kirahisi hapo. Niseme ukweli sijawahi kupaelewa kibaigwa na nilipomueleza hili alinishangaa Sana.
Amenieleza kibaigwa Kuna pesa nyingi Sana ya mahindi, na hapa tunapoongea nimeomba kuweka pesa kwa kutumia mgongo wake.
Kijana mwenzangu kama upo jirani na kibaigwa hebu jaribu kwenda kufanya research uwekeze ulichonacho kwenye mahindi hata kwa kuanza mdogomdogo, tusidharau Sana sehemu hizi.
Binafsi nimetoa tayari mil 25 kwa ajili ya hii kitu na ninaeleza kupata mil 60 Kama mambo yakikaa vizuri. Najua Sana biashara na najua Kuna kupata na kukosa Ila ni lazima kchukua "risk".
Bila kuchukua risk huwezi kufanikiwa kabisa, huu ni ukweli mchungu.
Kijana mdogo(38) anamiliki Lori 6, na zote anajaza mzigo unaenda Kenya na sehemu zingine.
Nipo tayari kufuata hii njia pia, tukubali tukatae ni lazima tufanye vitu vingi ili tuweze kuwa matajiri bila hivyo tusahau kuwa matajiri.
Umaskini ni mbaya Sana ndugu zangu, na kitu kibaya zaidi ni mawazo ya kimaskini.
Ukiwa maskini hata ukiongea jambo la kuchekesha watu hawacheki.
Hivyo naongeza nguvu nyingine kwenye sekta hii na haswa kupitia mgongo wa huyu jamaa yangu
Naona ndoto nyingi Ila muda nahisi hautoshi kuzitimiza.................!
Pesa ipo sana, ila yapaswa kutumia akili kuipata...!
Mkuu umeandikaa vyemaa sema hujaelezeaa kinaga ubagaa Jinsi ya kufanya Biashara hapo Kibaigwaa.... either Ni kwa kulima or kununua Mazao na kuyauza...
 
Back
Top Bottom