Rafiki yangu amekuwa tajiri mkubwa Dodoma, ninafuata njia zake. Tuzifuate

Binafsi napenda kuweka wazi kabisa kuwa Mimi Sera yangu ni utajiri, ninahubiri utajiri tu. Tafadhali Kama wewe una mawazo ya kimaskini hii post inaweza kukuletea shida ya msongo wa mawazo.
Rafiki yangu yupo dodoma muda mrefu Sana tokea tumalize wote chuo kipindi hicho.
Kwao ni dodoma na alianza harakati za maisha hata kipindi tunasoma, tulipomaliza alikuwa tayari kwenye mstari na Sasa hivi ni tajiri mkubwa tu huko dodoma.
Huyu amepata pesa kwenye mahindi kule kibaigwa, ni mahindi tu hakuna kingine zaidi ya hicho kilichompa utajiri. Ila Sasa hivi ana vingine(Malori).
Unaweza kupita sehemu na kudharau kumbe ndipo pesa inapatikana kirahisi hapo. Niseme ukweli sijawahi kupaelewa kibaigwa na nilipomueleza hili alinishangaa Sana.
Amenieleza kibaigwa Kuna pesa nyingi Sana ya mahindi, na hapa tunapoongea nimeomba kuweka pesa kwa kutumia mgongo wake.
Kijana mwenzangu kama upo jirani na kibaigwa hebu jaribu kwenda kufanya research uwekeze ulichonacho kwenye mahindi hata kwa kuanza mdogomdogo, tusidharau Sana sehemu hizi.
Binafsi nimetoa tayari mil 25 kwa ajili ya hii kitu na ninaeleza kupata mil 60 Kama mambo yakikaa vizuri. Najua Sana biashara na najua Kuna kupata na kukosa Ila ni lazima kchukua "risk".
Bila kuchukua risk huwezi kufanikiwa kabisa, huu ni ukweli mchungu.
Kijana mdogo(38) anamiliki Lori 6, na zote anajaza mzigo unaenda Kenya na sehemu zingine.
Nipo tayari kufuata hii njia pia, tukubali tukatae ni lazima tufanye vitu vingi ili tuweze kuwa matajiri bila hivyo tusahau kuwa matajiri.
Umaskini ni mbaya Sana ndugu zangu, na kitu kibaya zaidi ni mawazo ya kimaskini.
Ukiwa maskini hata ukiongea jambo la kuchekesha watu hawacheki.
Hivyo naongeza nguvu nyingine kwenye sekta hii na haswa kupitia mgongo wa huyu jamaa yangu
Naona ndoto nyingi Ila muda nahisi hautoshi kuzitimiza.................!
Pesa ipo sana, ila yapaswa kutumia akili kuipata...!

Utajiri wa mtu ni siri ,hawezi kukwambia jinsi alivyopata pesa,atakueleza kijuu juu tu.

Kaa humo.

Chamsingi ukiona fulsa sehem kaa kmya ukija humu utashambuliwa mpka bas, kibaigwa kweli wapo matajiri wengi wanaolima na kulangua mahindi mf cripsian mguri mudy pale kwny ofs ya tra n.k chamsingi pale uwende mwnyw ukiwa mgeni wanaogopa kukufanyia Kaz za shamba wanaogopa kutaopeliwa
 
Binafsi napenda kuweka wazi kabisa kuwa Mimi Sera yangu ni utajiri, ninahubiri utajiri tu. Tafadhali Kama wewe una mawazo ya kimaskini hii post inaweza kukuletea shida ya msongo wa mawazo.
Rafiki yangu yupo dodoma muda mrefu Sana tokea tumalize wote chuo kipindi hicho.
Kwao ni dodoma na alianza harakati za maisha hata kipindi tunasoma, tulipomaliza alikuwa tayari kwenye mstari na Sasa hivi ni tajiri mkubwa tu huko dodoma.
Huyu amepata pesa kwenye mahindi kule kibaigwa, ni mahindi tu hakuna kingine zaidi ya hicho kilichompa utajiri. Ila Sasa hivi ana vingine(Malori).
Unaweza kupita sehemu na kudharau kumbe ndipo pesa inapatikana kirahisi hapo. Niseme ukweli sijawahi kupaelewa kibaigwa na nilipomueleza hili alinishangaa Sana.
Amenieleza kibaigwa Kuna pesa nyingi Sana ya mahindi, na hapa tunapoongea nimeomba kuweka pesa kwa kutumia mgongo wake.
Kijana mwenzangu kama upo jirani na kibaigwa hebu jaribu kwenda kufanya research uwekeze ulichonacho kwenye mahindi hata kwa kuanza mdogomdogo, tusidharau Sana sehemu hizi.
Binafsi nimetoa tayari mil 25 kwa ajili ya hii kitu na ninaeleza kupata mil 60 Kama mambo yakikaa vizuri. Najua Sana biashara na najua Kuna kupata na kukosa Ila ni lazima kchukua "risk".
Bila kuchukua risk huwezi kufanikiwa kabisa, huu ni ukweli mchungu.
Kijana mdogo(38) anamiliki Lori 6, na zote anajaza mzigo unaenda Kenya na sehemu zingine.
Nipo tayari kufuata hii njia pia, tukubali tukatae ni lazima tufanye vitu vingi ili tuweze kuwa matajiri bila hivyo tusahau kuwa matajiri.
Umaskini ni mbaya Sana ndugu zangu, na kitu kibaya zaidi ni mawazo ya kimaskini.
Ukiwa maskini hata ukiongea jambo la kuchekesha watu hawacheki.
Hivyo naongeza nguvu nyingine kwenye sekta hii na haswa kupitia mgongo wa huyu jamaa yangu
Naona ndoto nyingi Ila muda nahisi hautoshi kuzitimiza.................!
Pesa ipo sana, ila yapaswa kutumia akili kuipata...!
Mkuu unataka tuje kununua mahindi yako yenye sumu? Tulisha tangaziwa kwamba mahindi ya huko Dodoma ya SUMU KUVU, wewe hilo tangazo halikukufikia?
 
Anything is possible.mm kibaigwa napajua sana biashara karibia zote.
Labda sijaelewa biashara yenu lakini kwamba biashara ya mahindi ununue malori mmmmh hapo nina Mashaka.

Wafanyabiashara wakubwa wa mahindi kibaigwa wanapeleka unga Zanzibar na faida ni ndogo sana.

Kenya wanapeleka wenyewe wakenya wanakuja kununua sokoni.Kwa mtanzania kupeleke Kenya ni ngumu kulingana na masharti ya wizara.

Mkuu nakushauri fuatilia hizo hela zako ni ngumu sana mtu kumaliza chuo 2018 ajue biashara ya kibaigwa Kwa mda mfupi.pale kibaigwa watu wanatapeliwa,wakenya wamelizwa sana (sijaamaanisha jamaako tapeli).

Kingine ambacho kinatakiwa kikushtue ni faida aliyokutajia yaani kutoka mil 25 hadi 60mil ni parefu sana.

Watu wanaopiga hela kidogo kibaigwa niwale wanaoweka stoo kina Gwajima wamejenga godowns lakini bado hawapati faida uliotaja.

Biasahara ya mahindi nimefanya tangu miaka 2005.

Take care

Lwanda Magere kashauri ukiona ndugu yako kapata mafanikio ya ghafla jaribu kuchunguza,Lwanda magere alipata utajiri kwa njia ya ushirikina(kutoa kafala) ila aliwadanganya ndugu zake yeye anafanya biashara.

Faida utakayoipata kwenye uwekezaji huo ndio una save hadi itimie, kwa ajili ya kununua subaru yako.
Trust mi hio 25m unaenda pigwa! Unless kuna biashara nyingine ya kificho ndani ya biashara ya mahindi!
 
M 25 kiuhalisia siyo pesa nyingi sana kwa watu wenye pesa zao ila kwa akina sisi "kajambanani" vizazi na vizazi vilivyopita hakuna aliyewahi kuishika nina imani ila wa kwanza nitakuwa mimi, niko Kigoma kuusaka💪💪💪
 
Mkuu nenda na kiteto kule mashamba ni makubwa na ni bei rahisi hayana thaman unaweza kupata shamba heka 20 kwa 500,000/= (laki tano tu) mahindi yanakubali sana na kupalilia watu wanapalilia heka 1 kwa tsh10k tu hivyo hivyo nq kuvuna.
Kwenye heka moja unaweza kupata had gunia 9 na gunia moja ni 45,000/=
Ukivuna heka 20 una uhakika wa 8M kama mambo yataenda vizuri
Huku wewe ukiwa umewekeza Sana sana 600k .
Mimi nimepata bahat ya kupata shamba heka 20 kwa laki mbili tu
(Nenda mwenyewe kafanya utafiti kama una nia kule pesa ipo na mvua ni nying tofaut kdogo na dodoma )
Haya ndiyo mawazo safi
 
Dodoma natamani connection ya zabibu..
Hapa Dar tunauziwa zabibu za kijani elfu nane kilo
Nimesikia Nairobi bei mara tatu
Mkuu nenda huko, hizo ndio vitu vinalipa. Sina connection ya zabibu, Ila jitahidi uende ukaangalie Hali ilivyo alafu nenda na Kenya pia uangalie huwezi kukosa sehemu wanayouza au kununua. Cha msingi nenda sehemu zote mbili, andaa pesa ya kuzunguka kwanza.
Nasisitiza hivi vitu vya hivi vinalipa Sana,watu wengi nachoona hawana tu pesa nyingi ya kuwekeza
All the best...
 
Back
Top Bottom