Rafiki wa Mchumba wangu ana shida nimsaidie?

Rafiki wa Mchumba wangu ana shida nimsaidie?

1.Mpe hela
2.wewe umejuaje kama ni rafiki na demu wako?Kama demu wako alikuambia ni rafiki yake,kwa nini wewe uwe na wasiwasi?Vingine si rafiki yake kama uweka mashaka kuwa itakuwaje
3.wewe kaona ndio utakuwa msaada kwake tena unajiuliza uliza,inategemea anakuchukuliaje,usifikir hana akili kukuomba wewe.
4.kwani huyo demu kakuambia usimwambie demu wako?Mpaka uwe na wasiwasi,kwani mahusiano mpaka umpe hela,unaweza ukawa nae mahusiano bila kumpa hela,sasa kwa nini kigezo cha hela ndo pekee kimshitue demu wako
5.kwani demu wako hakuamini kabisa kiasi cha wewe kuhofia,demu wako ukimweleza hatakuamini?kama hamuamini kiasi hiki huo uhusiano ni majanga.

1.Nimejua ni rafiki wa demu wangu aliwahi kunitambulisha siku moja,na kuna siku alikuwa na shida my gf akamwelekeza kiwandani niliipo akaja nika tatua fasta alikuwa anahitaji bidhaa flani,hivyo nikatumia tu uzoezu pale kazini akapata fasta.so ikawa tayari ana namba yangu pia ameshajua ninaweza ku solve issues akipata shida.
2.kuna comments watu wametoa kuwa utajuaje sasivi kweli ana hio shida ya selo?coz anakupigia simu,ukimsaidia isije kuwa ndo balaa baadae?
3.Hjaniambia nisimwambie bt logic kwanini yeye asimwambie ili apitie kule?haoni kuwa atakuwa ame bypass halafu itaonekana kama kulikuwa na jambo flani linaendelea?
4.Ananiamini,imani ipo ila inabidi ilindwe kwa busara,unaweza kufanya jambo kwa nia njema halafu likawa baya baadae.
 
Ni kweli hii pia nimeipenda,kwasababu huwezi jua kuwa ni kweli mtu kawekwa kizuizini,selo huenda ni mawazo mengine,nilitegemea apitie kwa gf wangu kwanza.

HOW OLD ARE YOU!!!!
Una nia ya kumsaidia au its just a puzzle to monitor peoples reaction???!!!!Kwani hapo polisi wanaingia kwa viza????Take your time nenda kituoni ujue kama tatizo ni halisi au jakubumba!!
 
Am ur bro,that my age.
asubuhi hii kanipigia simu kuwa amesolve,tukaongea mengine the akakata simu.
Najiuliza maswali yafuatayo.
1.jana nilikuwa job,sikuweza kufuatilia,leo nifuatilie kuwa ile issue ni kweli au niache.
2.kufuatilia kunaweza kunifanya nijue ukweli wake,bt kutofatilia ni ishara ya kuomaa pia.ni kuzuri kutaonuesha kuwa kweli nilikuwa bussy.
3.
 
Waadau habari za wkend....
jana meshindwa kumjibu mdada ambae ni rafiki wa karibu na girlfriend wangu,alinipigia simu na kuniomba nimsaidie kiasi flani cha fedha amtoe kuna rafiki yake yupo polisi.
nilimwambia kuna kazi nafanya ntamjibu baadae....
kuna maswali nimejiuliza.
1.kwanini asipitie kwa rafiki yake ambae ni mchumba wangu?
2.nikimsaidia je gf wangu akija kujua si atajua tulikuwa na mahusiano kabla?
3.Nikimwambia gf wangu si ndo anaweza kuzua ugomvui kati yao?
4.niuchune tuuu.
Ungekuwa wewe ungefanyaje?anajua kuwa uwezo wa kumsaidia unao.
ufs:Madame B,Lara1,gfsonwin,Mtambuzi,Paloma,Bujibuji,Watu 8,Snowhite,Munkari,lady Doctor,lady furahia.
CC;Wadau wote waliopo kwenye uhusiano,wanaotegemea kuwa na mahusiano.
UPDATES:Leo asubuhi amenipigia simu na kuniambia kuwa tayari ame solve.tukaongea na mengine akakata simu.
My take is:
1.Kweli alikuwa na tatizo au,coz tangu jana nilikuwa kazini,leo nipo off.
2.Tangu alipokuja kazini majuma kazaa yaliopita pale alipokuwa na shida,alimuambia my gf,akapewa my number akaja kiwandani nikamsaidia kwa kufanya logistic fasta akapata bidhaa yake mapema akaondoka.
3.Kuna siku my gf aliwahi kuniomba number ya huyo rafiki yake kuwa yeye ameisahau kwenye number yake nyingine ilioisha charge,nilimwambia sina,na kiukweli niliisha ifuta coz,nikiwa na shida na najua ntamuomba my gf,pia hatuna connection ya kuwa tunawasiliana kila wakati,hivyo sikuona umuhimu wa kuendelea kuwa nayo,though najua yeye alikuwa nayo.ok baada ya hapo kwanza hakuamini tukajadiliana weee,mwisho akajua kweli niliifuta akawa mpole akasema akirudi home simu yake yenye hiyo number atampigia.
4.mi sijui kila kitu kuhusu wao bt ni marafiki walisoma wote Utabibu.au sijui ananichukuliaje.
Now nina amani kuwa amesolve ,mengine yeye atajiongeza,kama alikuwa na lingine,Rafiki wa My gf namuheshimu sana.
5.Je kuna umuhimu wa kufuatilia kama alikuwa na tatizo?
BUT Thanks amesolve hata kama siju anamaanisha nini....
 
namba kaipata kwa rafiki yake,ambae ni gf wangu na alipewa wakati ana shida fulani kuja kununua bidhaa huku kiwandani hivyo alipewa anitafute akifika kiwandani ninakofanyia kazi.
Ok kama alipokuwa na shida wakati huo alipita kwa gf wako nadhani ni busara alitakiwa pia apite huko, ila shida haina adabu anaweza akawa amechanganyikiwa ila my take: hakikisha gf wako anajuwa hili kabla/baada tu ya kumsaidia but preferably kabla hujamsaidia,hii itakujengea uaminifu kwa gf wako na ataona umemthamini sana.pia litakuwa funzo kwa huyo rafiki yake next time awe anapita masijala(gf wako) kabla ya kukuona bosi. Na km gf wako mko karibu mpe yeye ili ampe hyo pesa rafiki yake. Km huyo dada alikuwa na nia mbaya basi nadhani atajuwa uko makini kiasi gani na ni jinsi gani unamthamin mchumba wako#MTAZAMO TU
 
msaidie tu maana amekuomba msaada kama shemeji yake
 
safi...Ahsante hii imekaa vema sana nimeipenda.....haizui mkwaruzo.political and logical approach.ahsante Tuko.

Kwa nini unatumia nguvu nyingi hivyo kumficha Gf wako?
Una ajenda gani na huyo rafiki? Yaani mkae kabisa mkubaliane kupika story ya kumhadaa Gf wako! Huyo rafiki atamdharau sana Gf wako. Labda mimi mgumu kuelewa ila hii hapana.
CC. OLESAIDIMU
 
Last edited by a moderator:
Am ur bro,that my age.
asubuhi hii kanipigia simu kuwa amesolve,tukaongea mengine the akakata simu.
Najiuliza maswali yafuatayo.
1.jana nilikuwa job,sikuweza kufuatilia,leo nifuatilie kuwa ile issue ni kweli au niache.
2.kufuatilia kunaweza kunifanya nijue ukweli wake,bt kutofatilia ni ishara ya kuomaa pia.ni kuzuri kutaonuesha kuwa kweli nilikuwa bussy.
3.

Bro kuna young na elder na ushaurqi huzingatia hayo!!!

Tatizo limeisha sasa tunasubiri taarifa kuwa amekuwa mchumba na mke mtarajiwa maana gf status is volatile
 
Kwa nini unatumia nguvu nyingi hivyo kumficha Gf wako?
Una ajenda gani na huyo rafiki? Yaani mkae kabisa mkubaliane kupika story ya kumhadaa Gf wako! Huyo rafiki atamdharau sana Gf wako. Labda mimi mgumu kuelewa ila hii hapana.
CC. OLESAIDIMU

Habari unaizunguka kwenye tofauti ya mwanaume na mvulana ila ndo kama ulivosema wewe ni mgumu kuelewa hili mpaka sasa!!!!

Tatizo limeisha na muhitaji katoa feedback kwa muombwa!!!Hii inakueleza nini????

Either ways shemeji zangu wakija mimi nashughulika na.tatizo objectively kutokana na yanavyokuja na taarifa kwa mke itaenda kama ni muhimu kufanya hivyo!!!!

Ingekuwa anaomba mchango wa send-off sawa ila tatizo. La kupimika na genuine wala sijiulizi kama liko ndani ya uwezo,mke /mume gani asiyependa mwenza mtenda mema!!????

Dunia mapito marejeo kwa muumba so kutenda mema ndo amal zenyewe! !!!!
 
Hilo ndio la msingi.
 
Hilo ndio la msingi.
The aftermath;

1. He didnt show his stand on the matter rather just escaped through a busy situation!!!!!
2. If she has a plot,and she is smart the dude is still targetable and availabe!!!!!
3.He didnt get to know the reality so the cloud of doubts and suspicions are his visiting partners still!!!
4.If the girl was real in trouble and they are good friends;if by chance she asked the permission from her and was granted, then the scar is irreparable and he is the jinxy in the white house!!!!

Tatizo kuisha wakati wako hai na bond bado ipo sio ushindi wa moja kwa moja ni kupooza njaa kwa kula mua!!!!
 
kaka ukpenda boga...........halaf pia ulichoombwa ni msaada wa kifedha na sio mapenz, na msaada wenyewe n kwaajili ya matatzo yanayotukumba wanadam bila hata taarfa...yawezekana mchumba wako kaambiwa akwambie akaunyaunya, akaelekeza akwambie mwenyewe. Fanya lililosahihi kwa wakat muafaka, utakuja kupata jibu la kumsaidia wakat ushachelewa
 
Thankk you MAPI
 
The aftermath;

1. He didnt show his stand on the matter rather just escaped through a busy situation!!!!!
2. If she has a plot,and she is smart the dude is still targetable and availabe!!!!!
3.He didnt get to know the reality so the cloud of doubts and suspicions are his visiting partners still!!!
4.If the girl was real in trouble and they are good friends;if by chance she asked the permission from her and was granted, then the scar is irreparable and he is the jinxy in the white house!!!!

Tatizo kuisha wakati wako hai na bond bado ipo sio ushindi wa moja kwa moja ni kupooza njaa kwa kula mua!!!!
Mkuu ntafuatilia taratibu ntajua tuu,ili niridhishe moyo ataniambia,next week naanza likizo so its grate for me,slowly but sure,nyerere alisema hivi "Mtu mwenye busara huyatilia shaka hata maamuzi yake mwenyewe" mi niliyatilia shaa maamuzi yangu ya pande zote.but mwenyewe anajua kuwa huwa namsaidia kama alivyokuja kazini kiwandani bidhaa,ok hajamaindi ila anajua jamaa hufikiri kwanza kabla ya kuamua,hata my gf akisikia hawezi kukasirika,pia mimi sikuwa mtu wa mwisho full back wa kumsaidia...hivyo sio issue sana,kama kweli alikuwa na tatizo amelitatua na amejua nipo bussy kwa nature ya kazi yangu,hilo huwa analijua hata yeye.....anyway,nasubiria siku labda anitanie kuwa mimi nikoje kwa kilichotokea....
 
Mpe kisha mgegede rafiki wa mchumba wako ni mchumba wako pia...shauri yako. ..hebu niPM namba yake nimsaidie mie...utamwambia mie ni mfanyakazi mwenzako umeniagiza...kisha namgegeda...nyama inajileta ww unazingua????
 
yaleyale ya shoga kumzunguka mwenzie.leo ukimpa kesho utackia shemeji wk end atutokii.
 
Waadau habari za wkend....
jana meshindwa kumjibu mdada ambae ni rafiki wa karibu na girlfriend wangu,alinipigia simu na kuniomba nimsaidie kiasi flani cha fedha amtoe kuna rafiki yake yupo polisi.
nilimwambia kuna kazi nafanya ntamjibu baadae....
kuna maswali nimejiuliza.
1.kwanini asipitie kwa rafiki yake ambae ni mchumba wangu?
2.nikimsaidia je gf wangu akija kujua si atajua tulikuwa na mahusiano kabla?
3.Nikimwambia gf wangu si ndo anaweza kuzua ugomvui kati yao?
4.niuchune tuuu.
Ungekuwa wewe ungefanyaje?anajua kuwa uwezo wa kumsaidia unao.
ufs:Madame B,Lara1,gfsonwin,Mtambuzi,Paloma,Bujibuji,Watu 8,Snowhite,Munkari,lady Doctor,lady furahia.
CC;Wadau wote waliopo kwenye uhusiano,wanaotegemea kuwa na mahusiano.

ongea na mchumba wako kwanza umueleze la sivyo yatakutokea puani,huyo rafiki wa mchumba wako ni mpuuzi
 
Ni best yake my gf,alipewa my no.alikuwa na shida ya kununua vifaa flani huku kiwandani,so ili apate urahisi akawa anaongea na my gf,my gf akamwambia kuwa mimi nipo huko akampa namba yangu ili akija nimsaidie mambo yaende haraka,nilifanikisha vizuri sana zoezi lile pale kiwandani,so hilila sasa linanitaka niingie mfukoni,so its too personal,alipokuja kiwandani wala sikuingia mfukoni just uzoefu tuu akafanikiwa,sasa namba yangu anayo anawasiliana direct nami,labda kaona haina haja ya kupitia kwa my gf.coz number yangu anayo.mi nimeona nipotezee,niuchune kwanza.kama vipi na hii issue ya hela apitie kwa gf wangu.

wadau wamekupa mawazo mengi na mazuri, ila kinachonikera mimi ni jinsi unavyorudia rudia jinsi ulivyokiuka taratibu kumsaidia huyo rafiki wa gf wako huko kiwandani kwenu. Hivi wote tukifanya kazi kwa kujuana maeneo yetu ya kazi mambo yataenda kweli? Imefikia wakati sasa tutambue kuwa ni dhambi kukiuka taratibu kwa ajili ya kufavour watu tunaowajua, hiyo ni sawa na RUSHWA tu. Wakifanya hivyo madaktari, polisi n.k hali si itakuwa mbaya.
 
Mi sina tatizo na wewe kumsaidia au kutomsaidia. Ila nataka igeuze kwa namna hii,
Ikitokea cku ukasikia gal friend wako kaenda kuomba msaada wowote ule iwe fedha, lift ya gari, ushauri nk.kwa rafiki yako bila kukwambia Utajisikiaje?
Akili za kuambiwa changanya na zako......
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom