Rafiki wa Mchumba wangu ana shida nimsaidie?

Rafiki wa Mchumba wangu ana shida nimsaidie?

Waadau habari za wkend....
jana meshindwa kumjibu mdada ambae ni rafiki wa karibu na girlfriend wangu,alinipigia simu na kuniomba nimsaidie kiasi flani cha fedha amtoe kuna rafiki yake yupo polisi.
nilimwambia kuna kazi nafanya ntamjibu baadae....
kuna maswali nimejiuliza.
1.kwanini asipitie kwa rafiki yake ambae ni mchumba wangu?
2.nikimsaidia je gf wangu akija kujua si atajua tulikuwa na mahusiano kabla?
3.Nikimwambia gf wangu si ndo anaweza kuzua ugomvui kati yao?
4.niuchune tuuu.
Ungekuwa wewe ungefanyaje?anajua kuwa uwezo wa kumsaidia unao.
ufs:Madame B,Lara1,gfsonwin,Mtambuzi,Paloma,Bujibuji,Watu 8,Snowhite,Munkari,lady Doctor,lady furahia.
CC;Wadau wote waliopo kwenye uhusiano,wanaotegemea kuwa na mahusiano.

Mtego wa Shem huo Kaka, Ingia Ndonga Ndonga uone
 
msaidie hilo ni jambo la haraka
acheni kuwaza mambo mengine na kama ni mtu mwelewa mwambie asimwambie mchumbako
wanawake wana wivu wa kijinga ila sio wote, kama ni mtu mwelewa ataelewa.
ndio maana wafrika hatuendelei tuna ile roho ya kwanini..we msaidie akikubwatukia huyo mchumba
wako na kama analipa unamchukua yeye alahh:smile-big:
 
Kwa hiyo akiwaza tu kukulipa kwa njia hiyo huku tayari zipu inafunguka dushelele wima na automatically ndani ya papuchi!!! Kwa yeye kuwaza tuuuuu????!!

Hebu kokotoa kwa njia ndefu kama jawabu litabaki hilihili

Nimezungumzia mazingira yanayoweza kumpelekea mtu kufikia hitimisho kuwa huenda huu ni mtego. Suala la kufungua zipu ni jingine kabisa haliingii hapa.

Halafu kama ukishajua ni mtego unafikiri kuna haja ya kuuingia, eti kwa sababu una dhamira ya kuukwepa.
 
Nimezungumzia mazingira yanayoweza kumpelekea mtu kufikia hitimisho kuwa huenda huu ni mtego. Suala la kufungua zipu ni jingine kabisa haliingii hapa.

Halafu kama ukishajua ni mtego unafikiri kuna haja ya kuuingia, eti kwa sababu una dhamira ya kuukwepa.

Kama hukatai ulichokiandika basi hukuelewa umeandika nini

Mtego wa shemeji kama kweli upo ni ku demolish ndo dawa sio kuukimbia
 
Huwezi jua kama ni kweli ana mtu kawekwa kizuizini na polisi au lah, maana kwa shida kubwa kama hiyo nina uhakika angeanza na aliyemzoea zaidi kama rafiki yake mkubwa (gf wako).
USHAURI: Mpe gf wako taarifa (mapema) ukiwa na lengo la kumsaidia huyo rafiki yake, maana girls bwana wana trics zao ambazo ukijakushtuka pamekucha

Na kwa kifupi huo mtego....mwambie amwombe gf wako....then na ww mjulishe gf wako mapemaaaa....
 
Nijuavyo mimi cwezi kumuomba mume wa dada yangu Pesa bila dadangu kujua kwanza tena yeye dadangu ikibidi ndo aniombee!(Mume sio mchumba tena wa dadangu) Sasa itakua rafiki jamani? Hapana mi nasema huyo shemejio hana Heshima na sio rafiki mzuri wa gf wako kuwa makini.

Sent from my BlackBerry
 
Mimi sidhani kama kumsaidia kuna tatizo endapo wewe unajiamini na mnaaminiana na gf wako japo umakini unahitajika.
1. Mweleze gf wako ukweli, kisha sikia anasemaje (ushauri wake) kama ni kweli kuna mtu polisi we msaidie hata kama gf wako atakataa, kuwa na gf au bf haimanishi ukubali kutosaidia mtu kwa sababu yake, huo ni ubinafsi.
2. Kama ni kweli utakubali kutomsaidia kwa sababu ya gf wako utakuwa unalea tabia ambayo itakuja kukutokea puani maana kuna siku atakukataza usimsaidie mama yako kwa sababu yoyote ile ambayo kwake ataiona ya msingi.
3. Inawezekana mahusiano yenu ni ya wasiwasi yaani wewe kiwembe na shem wako kicheche mpatapo fursa tu huitumia kisawasawa ndo maana unahisi gf wako hatokuelewa.
4. Utakapo msaidia kubali yote akikurudishia sawa asipofanya hivyo nayo sawa ili usijeingia mtegoni kama shem wako ni kicheche na katumia tatizo kama sababu ya kukupata.
5. Usiwe na mtazamo hasi kwa wadada, kama unajiheshimu na mahusiano yako yana mipaka na shem zako na mnaheshimiana sidhani kama unge-doubt, inawezekana mna mazoea yasiyokuwa na mashiko.
6. Mshauri utaratibu mzuri wa kutaka huduma/msaada kwako kuwa si busara kuja moja kwa moja huku akijua rajiki yake yupo na ndiye mpenzi wako hivyo ni vema akamwomba rafiki yake naye rafiki yake kama hatoweza atakuja kwako nawe ukisha msupport gf wako naye atamsaidia rafikiye.
7. In fact mnatakiwa kujiamini na kuaminiana huku mkijitambua na kujiheshimu, wapendeni watu na kuwasaidia wahitaji, mkono wa birika si mzuri.
 
Balaa gani utaanzisha mapenzi yanatakiwa yaanze kwenye misingi ya upendo na uaminifu, yaani kama ni Gf halafu unataka kuchukua nafasi ya maisha yangu yote huo utumwa. Kama muungano hauna faida unaacha unaendelea mbele mambo ya kugombana hayafai........
 
Msaada kitu cha muhimu ushasema ulienae ni rafiki wa GF wako kwanini uwe na mawazo hayo kama HUJALA tunda la pembeni?
 
kwa muda huu sijui kama bado waitaji ushauri vile msaada ulikuwa waharaka.....inawezekana ameona italeta shida kwa gf wako labda kutokana na anavyomwelewa....waweza kuongea nae na kumwiliza sababu za kuja mmoja kwa moja bila kupita kwa rafiki yake
 
Hadi kufikia hatua ya kusita na kuanza kujiuliza maswali juu ya jambo kama hilo, inaonekana mawazo hasi yametawala sana katika kichwa chako. Ivi inakuaje uogope kufanya jambo ingawa unauwezo wa kulifanya na hakuna sheria itayokuhukumu kwa kwa kumsaidia!, inaonekana we na mpenzio hamuaminiani, au niwewe mwenyewe ndio unawasiwasi kwa sababu ya tabia zako!.. Ila sikiliza, wanasema alie ng'atwa na nyoka akiguswa na jani anastuka, sina imani na wewe. Hilo si jambo la kuhofu kumsaidia rafiki wa mpenzio unahofu kwa sababu hakuna uaminifu kati yenu, au utashindwa kueleza ukweli wa tukio kwa mwenzako, au wewe mwenyewe unaweza ukawa na ajenda nyuma ya pazia...!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom