Bongotunacheza
JF-Expert Member
- Dec 7, 2018
- 718
- 1,643
To cut short story huyu jamaa ni rafiki yangu wa tangu utotoni.
Mwaka 2012 nikiwa vizuri sana kiuchumi alipatwa na msiba wa baba yake mzazi. Yeye kwao ndio wa kwanza na ndio mtoto anae tegemewa na familia nzima. Kwao ni Dar ila msiba ulimkuta akiwa kaenda kufanya interview ya kazi Kigoma (alikuwa ndio kamaliza chuo)
Jamaa hakuwa na option zaidi ya kujaribu msaada kutoka kwangu. Nilimlipia nauli ya gari kutoka Kigoma to Dar na alivyofika mjini nikampa Milioni moja na laki nane ili asimamie zoezi lote la msiba. Kwao ni uswazi, michango ya wananzengo haikufika hata 80. Wanaukoo wao njaa tupu. Wote wanamuangalia yeye kwa sababu " alikuwa anasoma chuo kikuu Udsm ambapo huwa wanasoma na kulipwa( bumu) so atakuwa na hela nyingi tu huyu jamaa"
Insha'allah msiba uliisha salama.
Miaka miwili baadae jamaa alipata kazi Serikalini (wizara ya ardhi) hapa hapa mjini Daslamu. Maisha yakasonga.
Mwaka 2020 wakati huo vyuma vikiwa vimekaza kweli kweli kuna mtu mmoja alisema anataka kuuza eneo lake. Kwa bahati nzuri kwangu nilipata mteja ambae alikuwa analihitaji hilo eneo na alikuwa na uwezo wa kulinunua. Ila kabla ya kulinunua jamaa alitaka kujiridhisha kwamba hilo eneo linamilikiwa kihalali na muuzaji.
So nilitakiwa kwenda wizara ya ardhi pale kufanya online search kuona kama huyu jamaa ndio mmiliki halali wa eneo na kama halina mgogoro wowote. Mtu ambae angenisaidia kwa haraka haraka ni huyu jamaa yangu rafiki wa tangu utotoni.
Nilichotaka kwake ni yeye kuingia kwenye system kisha anipe taarifa za hiyo plot.
Ebwana eeh jamaa kasema yeye hana access ya kutazama hizo taarifa ila mtu wa juu yake ndio ana access. So kama nataka suala hilo liende natakiwa nitoe laki mbili. (duh jamaa aliniona kama boya vile) I told him sipo vizuri sina chochote ila eneo likiuzwa basi nitampa hiyo laki mbili anayo akaniambia ngoja aongee kwanza na basi wake.
Majibu boss kagoma anataka laki mbili. Nikamwambia ngoja nikatafute hiyo pesa ikiwa tayari nitamtafuta huku moyoni nikisikitika yaani huyu mwamba anataka kunipiga kwa ishu ambazo hutolewa bure kabisa na Serikali.
Nilikuwa nna mtu mwingine ninae mfahamu ambae alikuwa hapo hapo wizara ya kazi nikamvutia waya wala haikuchukua hata lisaa akanipa taarifa za hicho kiwanja bila kudai hata senti tano.
Jamaa nilimuwekea alama ya x kwenye nafsi yangu.
Novemba 2023: Jamaa kaja na ngonjera sijui kasimamishwa kazi blah blah blah nyumbani hakuna chakula. Nikamwambia sina hata senti tano hela yote Nimetoka kulipa ada (Nilivyo kwama niliwapelekaga hadi watoto wangu shule ya kayumba kutoka English Medium nikaanzisha hadi Uzi hapa JF now nimewarudisha tena English Medium mambo ya hela yamekaa sawa tena.
# Tujifunze kulipa fadhila kwa watu waliowahi kutusaidia.