Anakutafuta wakati wa shida, muweke pembeni

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,891
ANAKUTAFUTA WAKATI WA SHIDA. MUWEKE PEMBENI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Moja ya Tabia Mbaya ya kibinafsi ambayo wanadamu wengi tunayo ni kumtafuta mtu Wakati wa shida. Wakati mambo yako yakiwa Safi aaaah! Kimya unajilia Maisha pekeako. Umepata kazi na unalipwa vizuri aaah! Hutafuti watu, alafu siku yakikupata ndio unatafuta Watu ati ni ndugu zako, Rafiki zako, au jamaa zako. Hivi wewe ni kichaa nini? Alafu unategemea usaidiwe. Huo ni ubinafsi.

Tabia Hii wanayo Watu wengi sio tuu marafiki au Ndugu Bali mpaka Wazazi. Mpaka unajiuliza Hii maana yake ni nini?

Taikon atasema ukweli wote. Uwe unanihusu Mimi mwenyewe au unamhusu yeyote. Ukweli utasemwa. Tuache Tabia Hii ya ajabuajabu.

Unampigia mtu simu ili umsalimie anajifanya Yuko busy. Sawa!

Tuanze na Wazazi. Unampigia mzazi simu Kwa lengo la kumsalimia yeye anakuletea mambo ya Pesa sijui matatizo. Haya unamuambia ngoja tujitahidi Mungu akijalia utamtumia, anaanza kukurushia maneno; ooh! Sasa ulinipigia nini simu, oooh! Sasa Huko mjini unafanyaje. Watibeli huwaga tunajibugi kwani huko uliko mnafanyaje?

Watoto wengi na Vijana wengi wapo kwenye changamoto Hii. Imefikia hatua Watoto wanashindwa kusalimia wazazi kisa wanaogopa masimango. Wengine wanaogopa kwenda nyumbani kuwaona wazazi Kwa kuogopa maneno ya karaha na dhihaka. Alafu wenyewe wazazi au walezi au Ndugu wanakuambia tunakutia hamasa. Acheni wendawazimu. Hakuna hamasa ya kumkejeli na kumpa maneno ya dhihaka MTU.

Wazazi wengi wakiwa na Mshahara wao au wamepokea mafao yao hawasalimii hata Watoto wao. Wakipigiwa simu wao muda wote wanafikiri wanaombwa Pesa. Ni nadra Sana mzazi wa kiafrika awe na Hali nzuri alafu ampigie mtoto wake amuambie, mwanangu nimepokea kiinua mgongo changu. Sasa ongea na Ndugu zako Mje hapa tufurahia, alafu mkifika Wakati WA Sherehe awaambie Watoto wake kuwa jamani hichi kihela ni kidogo msikitolee macho. Hata hivyo kila mmoja nitampa walau milioni tatu ili akabust mradi wake. Ni kiinua mgongo cha Baba/Mama yenu.

Ni ngumu Sana mzazi akutafute akiwa na Pesa. Ni ngumu Sana. Angalau wakina Mama wao wanajitahidi. Mkiwa mnatanguliza shida zenu kwenye Pesa za Watu eleweni mnabomoa upendo. Yaani kwenye Raha zako unitafuti lakini kwenye shida zako unanitafuta. Upendo gani huo kama sio uhuni.

Tuje Kwa Ndugu na Marafiki. Kimya! Kimya! Kimya! Mara paap! Simu, ooh! Unajua kesho kutwa ninaoa, wewe kwangu ni mtu muhimu sana. Ninaomba mchango wako. Laki tatu au Chini kabisa laki moja. Tuweni serious kidogo.

Nilishawahi kusema hapa, Utu na upendo haipimwi Kwa michango ya Pesa. Ukiwa na shida ya Pesa ndio unamtafuta MTU. Uthamini wako haupo kwenye huyo MTU Bali shida yako itatuliwe na Pesa za huyo mtu. Hiyo haijakaa Sawa.

Wengi wanaokutafuta Kwa sababu ya shida zao tayari wameshakuwekea kipimo cha msaada utakaotoa hivyo vyovyote utakavyofanya usipotimiza kiwango walichokuwekea watakupa ubaya walionao ndani ya Nafsi zao.

Utasikia jamaa bhana ATI katoa laki moja Wakati anauwezo wa kutoa laki tano. Mshahara wake ni milioni tano na watoto wake wanasoma nje ya nchi. Hiyo sio HAKI.

Tabia hiyohiyo Ipo kwenye mahusiano, mtu anakutafuta pale anapokuwa na shida Fulani. Mfano, Mwanaume akiwa Hana hamu ya ngono utashangaa zinapita Wiki na wiki hakutafuti na hata ukimtumia meseji hazijibu. Lakini Subiri siku hamu zimshike, utashangaa huyo anakuja na maneno elfu moja na moja. Ili tuu umpe tunda lako. Huo ni ubinafsi. Na hakuna upendo wa hivyo.

Shida haziunganishi Watu. Upendo ndio unaunganisha Watu. Alafu Watu wabaya na mashetani siku zote huunganishwa na shida. Au utasikia yakisema, Subiri naye atapatwa na shida tutaona. Ujue huyo ni shetani na mbinafsi.

Watu wema na wenye mioyo Safi huunganishwa na Mambo Mema. Hawezi kukuombea mabaya Bali anakuombea Mema ili mkutane kwenye Mema.

Hakuna Raha kama unapigiwa simu na Ndugu au Rafiki yako alafu anakuambia, amefanikisha mchongo Fulani hivyo anakualika wewe na familia yako muende mkafurahie. Au unampigia Ndugu yako au Rafiki yako Baada ya Kula bingo Fulani, na kumwambia njoo na familia yako tuje tufurahie. Huo ndio urafiki.

Urafiki na undugu au wazazi ni Wema na sio mabaya.

Mkijenga urafiki katika msingi wa matatizo hapo hakuna upendo kitakachofuata ni usaliti na unafiki. Urafiki na undugu imara utajengwa katika Mafanikio na furaha. Jambo lolote lenye matokeo huangaliwa zaidi kwenye dhamiri.

Mtu anaweza ukamuomba msaada na akakusaidia lakini akawa anafurahia matatizo yako na anatamani yaendelee kukuhenyesha. Wengine wanakuja kwenye matatizo yako ili kufurahia vile watakavyokuona unapata shida. Usoni wanaonyesha huzuni lakini MIOYONI mwao wanafurahia.

Hakuna mtu ambaye ataumia pale unapopata shida zaidi ya Yule ambaye akiwa na Mafanikio anakutafuta mfurahie Kwa pamoja Mafanikio yake. Na anataka nawe ufanikiwe kupitia Mafanikio yake aliyoyapata. Na hakuna MTU anayefurahia matatizo yako kama Yule anayekutafutaga Wakati akiwa na shida.

Matatizo ni yako binafsi lakini Mafanikio ni ya wote. Hiyo ni Kanuni ya upendo (Sacrifice). Huna haja ya kumpigia simu mtu umueleze shida zako ilhali mnamahusiano mazuri naye. Yaani kama MTU unawasiliana naye mara Kwa mara ni lazima ajue unahitaji msaada wake hata kama hutamwambia.

Kitendo cha kumpigia mtu au kuwasiliana na mtu Kwa mambo ya shidashida tafsiri yake nyakati ukiwa na raharaha huwasiliani naye. Na hapo ndipo Unafiki wenye ubinafsi unapozaliwa. Ni lazima tubadilike. Tujifunze kuwapenda Watu wetu wa karibu bila kujali Hali zao.

Tabia ya kutafutana kwenye shida ndio inaleta umungu MTU(ushetani) na kutanguliza Pesa Mbele badala ya utu.

Utibeli ni HAKI, UPENDO, AKILI na UKWELI.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
umeeleweka vyema kabisa Taikon

kwa wale ndugu/marafiki wenye ukaribu tunaosaidiana ni muhimu na salama zaidi kutafutana na kujuliana hali sio shida ndio ziwe sababu ya kukumbukana, kuna mtu ukiona kakutafuta ujue ni shida na kuna wale wengine wakikutafuta ujue unatakiwa uende ukazike au uchangie rambirambi.
 
Umepita mule mule, jana nimemchamba mtu kama bado hajaifuta namba yangu basi ana moyo wa shaba,
Ndugu huyu hakutafuti hadi awe ana shida ya pesa, na kisingizio chake kuumwa au kodi, nilimzoesha nikaona sasa tabia hii imekua sugu, hanitembelei kazi yake ni kuview status tu whatsapp, nikampa makavu yake.
 
hii tabia ni mbaya sana, juzi nmemtafuta ndugu yangu mmoja nikamsalimia tu akashangaa hakuna habari mbaya. Tulishazoeshana kutafutana kwa matatizo kama misiba.
 
ANAKUTAFUTA WAKATI WA SHIDA. MUWEKE PEMBENI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Moja ya Tabia Mbaya ya kibinafsi ambayo wanadamu wengi tunayo ni kumtafuta mtu Wakati wa shida. Wakati mambo yako yakiwa Safi aaaah! Kimya unajilia Maisha pekeako. Umepata kazi na unalipwa vizuri aaah! Hutafuti watu, alafu siku yakikupata ndio unatafuta Watu ati ni ndugu zako, Rafiki zako, au jamaa zako. Hivi wewe ni kichaa nini? Alafu unategemea usaidiwe. Huo ni ubinafsi.

Tabia Hii wanayo Watu wengi sio tuu marafiki au Ndugu Bali mpaka Wazazi. Mpaka unajiuliza Hii maana yake ni nini?

Taikon atasema ukweli wote. Uwe unanihusu Mimi mwenyewe au unamhusu yeyote. Ukweli utasemwa. Tuache Tabia Hii ya ajabuajabu.

Unampigia mtu simu ili umsalimie anajifanya Yuko busy. Sawa!

Tuanze na Wazazi.
Unampigia mzazi simu Kwa lengo la kumsalimia yeye anakuletea mambo ya Pesa sijui matatizo. Haya unamuambia ngoja tujitahidi Mungu akijalia utamtumia, anaanza kukurushia maneno; ooh! Sasa ulinipigia nini simu, oooh! Sasa Huko mjini unafanyaje.
Watibeli huwaga tunajibugi kwani huko uliko mnafanyaje?

Watoto wengi na Vijana wengi wapo kwenye changamoto Hii. Imefikia hatua Watoto wanashindwa kusalimia wazazi kisa wanaogopa masimango. Wengine wanaogopa kwenda nyumbani kuwaona wazazi Kwa kuogopa maneno ya karaha na dhihaka. Alafu wenyewe wazazi au walezi au Ndugu wanakuambia tunakutia hamasa. Acheni wendawazimu. Hakuna hamasa ya kumkejeli na kumpa maneno ya dhihaka MTU.

Wazazi wengi wakiwa na Mshahara wao au wamepokea mafao yao hawasalimii hata Watoto wao. Wakipigiwa simu wao muda wote wanafikiri wanaombwa Pesa.
Ni nadra Sana mzazi wa kiafrika awe na Hali nzuri alafu ampigie mtoto wake amuambie, mwanangu nimepokea kiinua mgongo changu. Sasa ongea na Ndugu zako Mje hapa tufurahia, alafu mkifika Wakati WA Sherehe awaambie Watoto wake kuwa jamani hichi kihela ni kidogo msikitolee macho. Hata hivyo kila mmoja nitampa walau milioni tatu ili akabust mradi wake. Ni kiinua mgongo cha Baba/Mama yenu.

Ni ngumu Sana mzazi akutafute akiwa na Pesa. Ni ngumu Sana. Angalau wakina Mama wao wanajitahidi.

Mkiwa mnatanguliza shida zenu kwenye Pesa za Watu eleweni mnabomoa upendo. Yaani kwenye Raha zako unitafuti lakini kwenye shida zako unanitafuta. Upendo gani huo kama sio uhuni.

Tuje Kwa Ndugu na Marafiki.
Kimya! Kimya! Kimya! Mara paap! Simu, ooh! Unajua kesho kutwa ninaoa, wewe kwangu ni mtu muhimu sana. Ninaomba mchango wako. Laki tatu au Chini kabisa laki moja.
Tuweni serious kidogo.

Nilishawahi kusema hapa, Utu na upendo haipimwi Kwa michango ya Pesa.

Ukiwa na shida ya Pesa ndio unamtafuta MTU. Uthamini wako haupo kwenye huyo MTU Bali shida yako itatuliwe na Pesa za huyo mtu. Hiyo haijakaa Sawa.

Wengi wanaokutafuta Kwa sababu ya shida zao tayari wameshakuwekea kipimo cha msaada utakaotoa hivyo vyovyote utakavyofanya usipotimiza kiwango walichokuwekea watakupa ubaya walionao ndani ya Nafsi zao.

Utasikia jamaa bhana ATI katoa laki moja Wakati anauwezo wa kutoa laki tano. Mshahara wake ni milioni tano na watoto wake wanasoma nje ya nchi. Hiyo sio HAKI.

Tabia hiyohiyo Ipo kwenye mahusiano, mtu anakutafuta pale anapokuwa na shida Fulani. Mfano, Mwanaume akiwa Hana hamu ya ngono utashangaa zinapita Wiki na wiki hakutafuti na hata ukimtumia meseji hazijibu. Lakini Subiri siku hamu zimshike, utashangaa huyo anakuja na maneno elfu moja na moja. Ili tuu umpe tunda lako. Huo ni ubinafsi.
Na hakuna upendo wa hivyo.

Shida haziunganishi Watu. Upendo ndio unaunganisha Watu.
Alafu Watu wabaya na mashetani siku zote huunganishwa na shida. Au utasikia yakisema, Subiri naye atapatwa na shida tutaona. Ujue huyo ni shetani na mbinafsi.

Watu wema na wenye mioyo Safi huunganishwa na Mambo Mema. Hawezi kukuombea mabaya Bali anakuombea Mema ili mkutane kwenye Mema.

Hakuna Raha kama unapigiwa simu na Ndugu au Rafiki yako alafu anakuambia, amefanikisha mchongo Fulani hivyo anakualika wewe na familia yako muende mkafurahie.
Au unampigia Ndugu yako au Rafiki yako Baada ya Kula bingo Fulani, na kumwambia njoo na familia yako tuje tufurahie. Huo ndio urafiki.

Urafiki na undugu au wazazi ni Wema na sio mabaya.

Mkijenga urafiki katika msingi wa matatizo hapo hakuna upendo kitakachofuata ni usaliti na unafiki. Urafiki na undugu imara utajengwa katika Mafanikio na furaha.
Jambo lolote lenye matokeo huangaliwa zaidi kwenye dhamiri.

Mtu anaweza ukamuomba msaada na akakusaidia lakini akawa anafurahia matatizo yako na anatamani yaendelee kukuhenyesha.
Wengine wanakuja kwenye matatizo yako ili kufurahia vile watakavyokuona unapata shida. Usoni wanaonyesha huzuni lakini MIOYONI mwao wanafurahia.

Hakuna mtu ambaye ataumia pale unapopata shida zaidi ya Yule ambaye akiwa na Mafanikio anakutafuta mfurahie Kwa pamoja Mafanikio yake. Na anataka nawe ufanikiwe kupitia Mafanikio yake aliyoyapata.

Na hakuna MTU anayefurahia matatizo yako kama Yule anayekutafutaga Wakati akiwa na shida.

Matatizo ni yako binafsi lakini Mafanikio ni ya wote. Hiyo ni Kanuni ya upendo (Sacrifice).
Huna haja ya kumpigia simu mtu umueleze shida zako ilhali mnamahusiano mazuri naye. Yaani kama MTU unawasiliana naye mara Kwa mara ni lazima ajue unahitaji msaada wake hata kama hutamwambia.

Kitendo cha kumpigia mtu au kuwasiliana na mtu Kwa mambo ya shidashida tafsiri yake nyakati ukiwa na raharaha huwasiliani naye. Na hapo ndipo Unafiki wenye ubinafsi unapozaliwa.

Ni lazima tubadilike. Tujifunze kuwapenda Watu wetu wa karibu bila kujali Hali zao.

Tabia ya kutafutana kwenye shida ndio inaleta umungu MTU(ushetani) na kutanguliza Pesa Mbele badala ya utu.

Utibeli ni HAKI, UPENDO, AKILI na UKWELI.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Somo zuri Sana nalipa nyota 5
 
Umepita mule mule, jana nimemchamba mtu kama bado hajaifuta namba yangu basi ana moyo wa shaba,
Ndugu huyu hakutafuti hadi awe ana shida ya pesa, na kisingizio chake kuumwa au kodi, nilimzoesha nikaona sasa tabia hii imekua sugu, hanitembelei kazi yake ni kuview status tu whatsapp, nikampa makavu yake.
Wewe unamtembelea ???
 
Wewe unamtafuta?
 
Safi sana
 
Kwingine kote umeongea sawa kabisa Ila umechemka kwa upande wa wazaz. Mzazi Hana muda Wala mipaka ya kuomba msaada kwako. Na kwa mila na desturi za kiafrika mtoto ndiye anatakiwa aanzishe salam, yani mtoto ndiye anapaswa kuwatafuta na kuwapgia wazazi sm ili kuwajulia hali. Ebu jiulize ni mara ngapi vijana wa kiume/kike wanawapgia wapenzi wao sm kwa siku/wiki na kuwahonga au kuwaomba pesa. Sasa inakuwaje mzazi aliyejinyima akakulea na kukusomesha hadi ukajitambua hadi leo umepata sm ya kuingia jf ushindwe kumpigia au ukimpigia akakuomba pesa unaona nongwa. Unadhani wakat baba yako anatafuta pesa ya kuhudumia familia na kukusomesha asinge tu Kula maisha ya raha na fraha na mke wake ( mama yako) au asingehonga michepuko alafu wewe ungekua kwa shida na pengine wakati unaugua angekuacha ufe tu.

Kijana aliyelelewa vyema kamwe hawezi kuthamini pesa kuliko mzazi wake, hawezi kulinganisha mzazi na kitu chochote bila kujali mzazi huyo alikulea vipi maan no matter what mzazi atabaki kuwa mzazi tu na mzazi hana mbadala. Tuwaheshimu wazazi wetu maana what goes around comes around.
 
ANAKUTAFUTA WAKATI WA SHIDA. MUWEKE PEMBENI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Moja ya Tabia Mbaya ya kibinafsi ambayo wanadamu wengi tunayo ni kumtafuta mtu Wakati wa shida. Wakati mambo yako yakiwa Safi aaaah! Kimya unajilia Maisha pekeako. Umepata kazi na unalipwa vizuri aaah! Hutafuti watu, alafu siku yakikupata ndio unatafuta Watu ati ni ndugu zako, Rafiki zako, au jamaa zako. Hivi wewe ni kichaa nini? Alafu unategemea usaidiwe. Huo ni ubinafsi.

Tabia Hii wanayo Watu wengi sio tuu marafiki au Ndugu Bali mpaka Wazazi. Mpaka unajiuliza Hii maana yake ni nini?

Taikon atasema ukweli wote. Uwe unanihusu Mimi mwenyewe au unamhusu yeyote. Ukweli utasemwa. Tuache Tabia Hii ya ajabuajabu.

Unampigia mtu simu ili umsalimie anajifanya Yuko busy. Sawa!

Tuanze na Wazazi. Unampigia mzazi simu Kwa lengo la kumsalimia yeye anakuletea mambo ya Pesa sijui matatizo. Haya unamuambia ngoja tujitahidi Mungu akijalia utamtumia, anaanza kukurushia maneno; ooh! Sasa ulinipigia nini simu, oooh! Sasa Huko mjini unafanyaje. Watibeli huwaga tunajibugi kwani huko uliko mnafanyaje?

Watoto wengi na Vijana wengi wapo kwenye changamoto Hii. Imefikia hatua Watoto wanashindwa kusalimia wazazi kisa wanaogopa masimango. Wengine wanaogopa kwenda nyumbani kuwaona wazazi Kwa kuogopa maneno ya karaha na dhihaka. Alafu wenyewe wazazi au walezi au Ndugu wanakuambia tunakutia hamasa. Acheni wendawazimu. Hakuna hamasa ya kumkejeli na kumpa maneno ya dhihaka MTU.

Wazazi wengi wakiwa na Mshahara wao au wamepokea mafao yao hawasalimii hata Watoto wao. Wakipigiwa simu wao muda wote wanafikiri wanaombwa Pesa. Ni nadra Sana mzazi wa kiafrika awe na Hali nzuri alafu ampigie mtoto wake amuambie, mwanangu nimepokea kiinua mgongo changu. Sasa ongea na Ndugu zako Mje hapa tufurahia, alafu mkifika Wakati WA Sherehe awaambie Watoto wake kuwa jamani hichi kihela ni kidogo msikitolee macho. Hata hivyo kila mmoja nitampa walau milioni tatu ili akabust mradi wake. Ni kiinua mgongo cha Baba/Mama yenu.

Ni ngumu Sana mzazi akutafute akiwa na Pesa. Ni ngumu Sana. Angalau wakina Mama wao wanajitahidi. Mkiwa mnatanguliza shida zenu kwenye Pesa za Watu eleweni mnabomoa upendo. Yaani kwenye Raha zako unitafuti lakini kwenye shida zako unanitafuta. Upendo gani huo kama sio uhuni.

Tuje Kwa Ndugu na Marafiki. Kimya! Kimya! Kimya! Mara paap! Simu, ooh! Unajua kesho kutwa ninaoa, wewe kwangu ni mtu muhimu sana. Ninaomba mchango wako. Laki tatu au Chini kabisa laki moja. Tuweni serious kidogo.

Nilishawahi kusema hapa, Utu na upendo haipimwi Kwa michango ya Pesa. Ukiwa na shida ya Pesa ndio unamtafuta MTU. Uthamini wako haupo kwenye huyo MTU Bali shida yako itatuliwe na Pesa za huyo mtu. Hiyo haijakaa Sawa.

Wengi wanaokutafuta Kwa sababu ya shida zao tayari wameshakuwekea kipimo cha msaada utakaotoa hivyo vyovyote utakavyofanya usipotimiza kiwango walichokuwekea watakupa ubaya walionao ndani ya Nafsi zao.

Utasikia jamaa bhana ATI katoa laki moja Wakati anauwezo wa kutoa laki tano. Mshahara wake ni milioni tano na watoto wake wanasoma nje ya nchi. Hiyo sio HAKI.

Tabia hiyohiyo Ipo kwenye mahusiano, mtu anakutafuta pale anapokuwa na shida Fulani. Mfano, Mwanaume akiwa Hana hamu ya ngono utashangaa zinapita Wiki na wiki hakutafuti na hata ukimtumia meseji hazijibu. Lakini Subiri siku hamu zimshike, utashangaa huyo anakuja na maneno elfu moja na moja. Ili tuu umpe tunda lako. Huo ni ubinafsi. Na hakuna upendo wa hivyo.

Shida haziunganishi Watu. Upendo ndio unaunganisha Watu. Alafu Watu wabaya na mashetani siku zote huunganishwa na shida. Au utasikia yakisema, Subiri naye atapatwa na shida tutaona. Ujue huyo ni shetani na mbinafsi.

Watu wema na wenye mioyo Safi huunganishwa na Mambo Mema. Hawezi kukuombea mabaya Bali anakuombea Mema ili mkutane kwenye Mema.

Hakuna Raha kama unapigiwa simu na Ndugu au Rafiki yako alafu anakuambia, amefanikisha mchongo Fulani hivyo anakualika wewe na familia yako muende mkafurahie. Au unampigia Ndugu yako au Rafiki yako Baada ya Kula bingo Fulani, na kumwambia njoo na familia yako tuje tufurahie. Huo ndio urafiki.

Urafiki na undugu au wazazi ni Wema na sio mabaya.

Mkijenga urafiki katika msingi wa matatizo hapo hakuna upendo kitakachofuata ni usaliti na unafiki. Urafiki na undugu imara utajengwa katika Mafanikio na furaha. Jambo lolote lenye matokeo huangaliwa zaidi kwenye dhamiri.

Mtu anaweza ukamuomba msaada na akakusaidia lakini akawa anafurahia matatizo yako na anatamani yaendelee kukuhenyesha. Wengine wanakuja kwenye matatizo yako ili kufurahia vile watakavyokuona unapata shida. Usoni wanaonyesha huzuni lakini MIOYONI mwao wanafurahia.

Hakuna mtu ambaye ataumia pale unapopata shida zaidi ya Yule ambaye akiwa na Mafanikio anakutafuta mfurahie Kwa pamoja Mafanikio yake. Na anataka nawe ufanikiwe kupitia Mafanikio yake aliyoyapata. Na hakuna MTU anayefurahia matatizo yako kama Yule anayekutafutaga Wakati akiwa na shida.

Matatizo ni yako binafsi lakini Mafanikio ni ya wote. Hiyo ni Kanuni ya upendo (Sacrifice). Huna haja ya kumpigia simu mtu umueleze shida zako ilhali mnamahusiano mazuri naye. Yaani kama MTU unawasiliana naye mara Kwa mara ni lazima ajue unahitaji msaada wake hata kama hutamwambia.

Kitendo cha kumpigia mtu au kuwasiliana na mtu Kwa mambo ya shidashida tafsiri yake nyakati ukiwa na raharaha huwasiliani naye. Na hapo ndipo Unafiki wenye ubinafsi unapozaliwa. Ni lazima tubadilike. Tujifunze kuwapenda Watu wetu wa karibu bila kujali Hali zao.

Tabia ya kutafutana kwenye shida ndio inaleta umungu MTU(ushetani) na kutanguliza Pesa Mbele badala ya utu.

Utibeli ni HAKI, UPENDO, AKILI na UKWELI.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Taikon WA fasihi 📌🔨 💪💪💪
 
Back
Top Bottom