Racism within TZ as Arusha hotel denies access to Blacks

Mkuu soma vizuri. Taarifa inasema"local people". Haizungumzii watu weusi! Maana yake ni kuwa mmatumbi asiyekuwa local ataruhusiwa. Taarifa imekuzwa pasipo sababu.

Hauwezi kuzungumzia hiki unachokiita ubaguzi bila kuzungumzia sababu ambazo zinazoweza kuwafikisha hapo.

Profiling ipo hata kama hatupendi. Naamini njia nzuri ya kukomesha tabia kama hii ni kuzisusia sehemu hizo wala si kulazimisha kuingia.

Amandla.......


....kwa hiyo wana haki ya kumzuia mmatumbi Local?? Si yale yale?? Fundi, nakuaminiaga, Lakini hapa unaniangusha mkuu...!
 

Taarifa inasema"local people". Haizungumzii watu weusi! Maana yake ni kuwa mmatumbi asiyekuwa local ataruhusiwa. Taarifa imekuzwa pasipo sababu.

Naamini njia nzuri ya kukomesha tabia kama hii ni kuzisusia sehemu hizo wala si kulazimisha kuingia.

Fundi Mchundo, heshima mbele kama jana, na leo, na kesho, na siku zote.

Mtu anapokubagua usiingie sehemu halafu wewe ukamsusia ni kwamba umemnyima kunde. That is the point of segregation, hakutaki uende pale. Ukisusa unampunguzia mashuzi.

Umesema huu sii ubaguzi wa rangi. Ni kweli. Ni ubaguzi wa wazawa. Difference without distinction. Samahani kwa kuchanganya ubaguzi wa wazawa na ubaguzi wa rangi. Ila si vema unapojaribu kusema tuelekeze macho yetu kwenye chanzo cha ubaguzi huu, kwamba tunawaibia wazungu kamera zao. Hiyo ni kutaka kuhalalisha, kusafisha, ubaguzi kwa sababu eti mbaguzi anayo sababu. Na ni kuvunja sheria za nchi. Huwezi kutuambia kwamba tuache kuwaibia wazungu kamera ndio watukubalie kuingia kwenye hoteli zao, wasitubague.

Utapopinga, unapopigania haki na kuheshimiwa kwa Wahindi humu ndani, basi pigania, pinga, linda haki na heshima za wazawa pia kwa nguvu ile ile.

Hata mimi ninaweza kukupa sababu lukuki hapa za kufanya niwachukie wahindi, ambao kiukweli kabisa ndani ya moyo wangu nina wa-maindi ila najitahidi kujizuia, kuwapenda. Nimewajua Wahindi tuko utotoni kama ni watu ambao walikuwa hawakanyagi upande wa pili wa reli ninakoishi mimi, wanajitenga kwenye viota Upanga na Kisutu, akikuajiri kwenye duka lake utakuwa mpagazi tu, huwezi kupanda ukawa meneja, hawana uchungu na utajiri wa nchi wanauhamisha nje, wana pasi za nchi tatu tatu, duka la mhindi akikuuzia the wrong item usithubutu kurudisha dukani. Kijamii, sio rahisi kuoa na kuolewa na mhindi, mpaka watu wanaanzisha thread hapa kutaka msaada wa jinsi ya kuona na mhindi. Udhia mtupu. Lakini pamoja na yooote hayo, unatufundisha, wewe Fundi Mchundo karibia peke yako, unatuasa humu ndani kila kukicha tusibague, tusichukie Wahindi, tusisingizie Wahindi kwa umaskini wetu. Na tunakusikiliza, tunajifunza kwako.

Leo unatamka kwamba yule mteja mzawa angekuwa ni "mmatumbi asiyekuwa local" angekubaliwa kuingia pale hotelini? Wale walinzi getini walijuaje kwamba jamaa sio "mmatumbi asiyekuwa local," waliomba ID inayoonyesha kabila na local address au walimuona tu sio mzungu, wakajua ni "local," mzawa? Wakabagua mzawa. Leo unatamka kwamba habari ya ubaguzi wa wazawa "imekuzwa"? Waziri kasafiri kwenda kupigana na ubaguzi ana kwa ana mpaka wenye hoteli wamekiri wewe Fundi Mchundo unasema hadithi "imekuzwa"?

Ninapinga kwa ukomo wa masikitiko ulivyokataa kulaani ubaguzi wa Wazawa nchi mwetu wenyewe kinyume na sheria za nchi, kinyume na kila aina ya maadili ya jamii zilizostaarabika.
 
Fundi Mchundo,
Mkuu, kwani David Maige ni kati ya hao local people?..na ni akina nani hawa local people haswa tufahamishe..
No mkuu wangu huwezi kususia kitu kipo chumbani mwako!.. Ukisusa utaonekana wee mjinga sawa na kukataa kula kwa sababu mkeo kamsongea ugali mgeni kabla yako..
 
Afu ninye Elites mkibaguliwa ndio mnakumbuka kuwa na nyinyi ni watu weusi.
 
Dilunga na wengine.
Najua kuwa nimewaudhi wengi kwa dhana ya kuonekana kuwa natetea ubaguzi. Si hivyo hata kidogo. Ninachotaka kusema ni hivi:

a) Sheria zetu zinasema nini juu ya "right of admission?". Mwenye mali ana haki gani ya kuamua nani atumie facility zake? Kwa mfano, je mwenye mali anaweza kusema kuwa hapa ni mahali pa wanaume tu? Au kama wanavyofanya kwenye kitchen party, wanawake tu? Au tunavyofanya bila kusema katika sehemu nyingi za starehe n.k., hapa mwenye ulemavu atumiae kiti cha magurudumu hakaribishwi? Nakumbuka hapo zamani kuna mmatumbi mwenzetu alimlalamikia Mwalimu kuwa wamatumbi wanazuiwa kuingia Kilimanjaro Hoteli ya wakati ule. Mwalimu alimjibu, waachie bwana, pale mahali ni pao!

Ingawa inachukiza lakini hatuwezi kumlazimisha mtu mwenye biashara yake kuingiza kila anayetaka kuingia kwenye sehemu yake. Tusimtupe mtoto na maji aliyoogea kutokana na vitendo cha watu wachache. Lakini hii isituzuie kuangalia kama sheria zetu zinazuia ubaguzi wa aina zote.

b) Ninaposema kuwa hii habari imekuzwa ni kwa sababu tunazungumzia habari ya upande mmoja. Tunaambiwa kuwa mtu mmoja alizuiwa, akaenda kwa mwenye nguvu, mwenye nguvu akawaita wahusika, nao wakasema kweli policy ipo ya kibaguzi ipo nao wataibadilisha mara moja! Hata kama hiyo policy ipo lakini kweli inaweza kubadilishwa kirahisi namna hiyo? Zaidi ya hapo, habari inadai wanaoruhusiwa ni foreigners na power elites? Tunajua kuwa kuna foreigners kibao walio weusi, hasa hapo Arusha kwenye Mahakama ya Rwanda. Power elites ( labda ndiyo maana Waziri alikaribishwa kirahisi) wengi wao ni weusi na watanzania. Walijuaje kuwa mhusika hayumo katika moja ya makundi haya? Walimuuliza pasi yake? Walimwona hajavaa Armani? Walijuaje? Mimi hapa ndipo panaponisumbua. Kitakachofanyika sasa ni kumuingiza mhusika katika kundi la Power Elites na locals wa kawaida wataendelea kuzuiwa kama kazi.

c) Tunapozungumzia ubaguzi ni lazima pawe na pattern. Kusema mtu mmoja amezuiwa kwa hiyo hao ni wabaguzi haitoshi. Mtu anaweza kujitetea kuwa mhusika alikuwa katika hali isiyopendeza na hatutakuwa na la kusema. Tuwe wavumilivu. Tupate ushahidi wa pattern of discrimination, halafu tuwasulubu. Kwa kuanzia, wamatumbi wote waliozuiwa kuingia kwenye hiyo hoteli wangeorodheshwa. Pafunguliwe mahali ( web-site, ofisi ya kata ya kijiji n.k.) ambapo kila atakaezuiwa atajiorodhesha. Na wenye hoteli waambiwe kuwa hicho kinaendelea.

d) Desemba 1, 1955, wakazi weusi wa mji wa Montgomery, Alabama waliamua kususia mabasi hadi hapo watakapo ruhusiwa kukaa popote watakapo. Mgomo huu ulidumu zaidi ya mwaka mmoja na ni mmoja wa catalysts wa Civil Rights Movement ambayo ilisaidia kuondoa official ubaguzi Marekani. Kwa habari zaidi soma hapa: Civil Rights Movement 1955-1965: The Montgomery Bus Boycott.

Hivi karibuni wanafunzi wa vyuo kadhaa maarufu marekani walitangaza kuwa watasusia makampuni yote ambayo hayaajiri wanasheria weusi kwa kiwango kinachoridhisha. Walianza kukusanya takwimu za pattern za ajira za maofisi hayo. Mengi ya maofisi hayo kusikia hivyo yakaanza kampeni ya kuhakikisha kuwa wanatoa nafasi zaidi kwa ethnic minorities katika ajira zao.

Ninaposema tususie simaanishi kuwa tususie kimya kimya. Tunasusia na kueleza umma kwa nini tunafanya hivyo. Tunasusia na kuwaambia wageni walio nchini kitu gani kinachoendelea katika hiyo hoteli. Tunasusia, na kuwaambia BBC kinachoendelea. Na kadhalika , na kadhalika. Lakini hii kwetu ni kazi kubwa. Tunapenda majibu rahisi ya shujaa kuja kwenye farasi na kutuokoa. Ndiyo maana tutaendelea kunyanyaswa kwenye vi-supamaketi na mahoteli uchwara maana wanajua hatuna jinsi. Haya haya yanaendelea kwa hao tunaowaita wahindi. Sisi ambao ni vijisenti vyetu ndivyo vinaendesha biashara zao, bado tunaendelea kujikomba kwa wale kati yao ambao wanatubagua wazi wazi! Kama kweli huo ubaguzi upo na unatuuma, kwa nini bado kila tukipata tunakimbilia kuwapelekea?

e) Marekani na sehemu nyingi tu kuna profiling inafanyika. Ni hivi karibuni tu ambapo familia ya kiislamu ilishushwa kwenye ndege baada ya kusikika wakiulizana wapi mahali salama zaidi kukaa. Hata baada ya kuonekana kuwa hawana hatia, shirika la ndege husika kwa kiburi lilikataa kuwachukua na kuwarudishia gharama walizoingia kukata tiketi katika shirika lingine. Habari ikapelekwa kwenye vyombo vya habari. Shirika likagundua kuwa kuna waislamu na sympathizers wao kibao ambao wako hatarini kuwakosa. Haraka haraka wakaomba msamaha na kuahidi kurudisha gharama zote na ziada!

Fundisho ni kuwa, ukitaka kumuumiza mfanya biashara, mpige kwenye pochi yake. Mpaka tutakapostukia hili, tutaendelea kubaguliwa hapo tulipo. Naam, najua ubaguzi upo. Lakini waziri kuja kutoa tamko si solution. Tunahitaji kuwaambia hao wabaguzi kuwa vijisenti vyetu na vya ndugu zetu ndivyo vinavyowaweka hapo. Lakini wakati tukifanya hivyo, tuambiane wenyewe kuwa tuache vitabia vya kijinga ambavyo vinawapa visingizio wabaguzi kutubagua.

Amandla...........
 
Fundi Mchundo,
Mkuu, kwani David Maige ni kati ya hao local people?..na ni akina nani hawa local people haswa tufahamishe..
No mkuu wangu huwezi kususia kitu kipo chumbani mwako!.. Ukisusa utaonekana wee mjinga sawa na kukataa kula kwa sababu mkeo kamsongea ugali mgeni kabla yako..

Mkandara.

Kwa hiyo mkewe akimsongea ugali mgeni kabla yake dawa ni kumpiga? Atakaeonekana mjinga ni nani? Yule aliyempiga au yule aliyejiamulia kuondoka?

Amandla.......
 
Leo unatamka kwamba yule mteja mzawa angekuwa ni "mmatumbi asiyekuwa local" angekubaliwa kuingia pale hotelini? Wale walinzi getini walijuaje kwamba jamaa sio "mmatumbi asiyekuwa local," waliomba ID inayoonyesha kabila na local address au walimuona tu sio mzungu, wakajua ni "local," mzawa? Wakabagua mzawa. Leo unatamka kwamba habari ya ubaguzi wa wazawa "imekuzwa"? Waziri kasafiri kwenda kupigana na ubaguzi ana kwa ana mpaka wenye hoteli wamekiri wewe Fundi Mchundo unasema hadithi "imekuzwa"?

Swali langu exactly. Hiyo policy inayodaiwa ilikuwepo ilikuwa practised vipi? Kila mmatumbi alikuwa akiulizwa pasi kabla ya kuruhusiwa? Au kila mmatumbi alikuwa akizuiwa? Kama ni hivyo, waziri aliingiaje? Au aliwapigia simu kwanza? Kama aliwapa taarifa ya ujio wake alikosea. Kwa nini asimtume mtu kwanza kuthibitisha hayo aliyoambiwa? Kwa nini asimtangulize private sectrary wake aende akajaribu kuingia? Au Katibu Kata wa kijiji cha jirani. Badala ya hivyo, Mkuu anapanda farasi wake na kwenda kupigania haki ya wazawa based kwenye testimony ya mtu mmoja! Hivi angesubiri na kuestablish hiyo pattern, pangepunguka nini? Baada ya kufanya hivyo wala asingekuwa na haja ya kwenda Manyara ( BTW kwa gharama ya mlipa kodi). Angeita press conference na kuweka wazi shutuma hizo na kama kuna sheria imevunjwa angewaagiza wahusika wachukue hatua maana ushahidi tosha angekuwa nao. Kwa kufanya alivyofanya, amewapa nafasi jamaa watoe platitudes tupu za kufurahisha jamvi.

Haya ya kupeana siku saba hayasaidii kitu. Tunaweka bandeji kwenye kidonda tu. Tutaweza kupigana na ubaguzi wa kila aina kwa kuonysha kwa vitendo kuwa una gharama. Mbaguzi ajue kuwa atalipia vitendo vyake na kuwa hatuna mas'hara.

Amandla......
 
Last edited:
Bado nimo. Kitu ambacho wengi hatukioni ni kuwa kilichofanyika hapa si ubaguzi wa rangi bali wa kitabaka. Ubaguzi huu ni more insidious kwa vile unazidi kukubalika katika jamii yetu. Shirika lenye policy ya kibaguzi wa rangi haliwezi kuwa na mmatumbi katika senior position. Mbaguzi wa rangi nyeusi hataki kumwona mtu mweusi katika nafasi yeyote inayolingana na ya kwake, period. Bwana Maige alizuiwa kwa sababu alionekana hayumo katika tabaka linalokaribishwa mle ndani na si rangi yake. Walinzi walimpima kutokana pengine na nguo alizovaa yeye na familia yake. Walimpima pengine kwa kuangalia simu aliyokuwa nayo. Walimpima bila shaka kutokana na usafiri uliomleta. Walimpima pengine kutokana na lahfudh yake anapoongea kiingereza. Hivi ndivyo vimekuwa vipimo vyetu. Wala si rangi. Bila shaka angevaa Armani, angeendesha Lexus na watoto wake wangeongea kwa lahfudh ya waliotoka majuu, milango ingefunguliwa! Tumekuwa a class based society bila kujitambua.

Kuna thread humu ndani ambamo kuna quotation ya namna mabinti fulani wanavyotukanana matusi ya nguoni. Mojawapo ya matusi ni kuwa " umezaliwa Manzese...!" Tumefika mahali ambapo vijana wetu wanapimana kutokana na alikozaliwa mtu kana kwamba kuzaliwa Manzese au Buguruni ni kosa! Tunakoelekea ni kubaya.

Amandla......
 
Habari hii inanikumbusha Mhe. John Mamosa Cheyo alivyofukuzwa kama mbwa kwenye Hotel ya wazugngu kule kigamboni naye pia alilalamika sijui hatua gani zilichukuliwa.
 
Hii hotel si waliuziwa Wahindi wa Gapco? Sikumbuki vizuri lakini nadhani hivyo. KAma nimekosea nisamehewe.

Now , Indians ,Indians, Indians. .............na ubaguzi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom