Racism within TZ as Arusha hotel denies access to Blacks

Kutokana na kichwa cha habari, hata Obama asineona ndani.

Hivi tunasheria inayomlazimisha mwenye mali kumhudumia kila mtu anaetaka huduma hiyo bila kubagua? Tofauti na mheshimiwa waziri alivyosema, hii hoteli ni ya wenye miliki na sio ya watanzania. Tulipoziuza tumepoteza milki yetu. Mimi ushauri wangu ni badala ya kukimbilia kwa wanasiasa tuanzishe kampeni ya kuzisusia hoteli zote zenye taratibu hizo. Na zaidi ya hivyo, tupeleke habari huko wanakotoka hao watalii kuwa hoteli hizo ni za kibaguzi. Hivyo hivyo kwa hayo maduka ya Mlimani City.

Amandla....
 
sasa mimi nikianza kuongelea upendeleo kwa watu wetu naambiwa kwamba "mbaguzi na mgumu kuelewa" tatizo kubwa na watanzania ni wagumu sana kuukubali ukweli tunaiangalia dunia vinginevyo kabisa utawaona akina mwakijiji na wenzake siku zote wakipiga domo kuwatetea wageni hapa kwetu mimi nimesema ni lazima tutoe upendeleo kwa watu wetu kwamba watu woote ambao hawana asili ya kwetu hata kama wamezaliwa hapa kwetu ni lazima tuwatofautishe na kuwanyima kwa makusudi kabisa haki sawa na sisi kwani ndivyo dunia ilivyo, kupingana na hilo ni kujaribu kuukataa ukweli ambao upo dhahiri, wewe mwenyewe umesema kwamba huko ulipo unabaguliwa na ukija hapa nyumbani pia unabaguliwa sasa swali linakuja Je ni mpaka lini tutaendelea kuwa watu wa kudharauriwa? Kumbukeni kwamba mwanadamu anaishi dunia kwa miaka mingi sana na mpaka leo hajweza kubadilisha huo ukweli wa upendeleo sasa nyie akina mwanakijiji ni kina nani mnaofikiri kwamba mna suluhisho la matatizo ya binadamu?
Narudia tena VITAMBULISHO TOFAUTI KWETU NA WATU WENYE ASILI YA NJE KWANI KILA KITU KINAANZIA HAPO BAADA YAPO TUNAKUJA SHULE, KAZI, MAKAZI, MAZISHI, USAFIRI n.k

wewe unahitaji kumuona daktari with your xenophobic rant!
 
sasa angalia yale yale unaukataa ukweli tena, hayo yoote unayoyasema yanasababishwa na kutokuwa na upendo wa kweli kwa nchi yetu na watu wetu, mapenzi ya kweli yanatokana na kuthamini watu wako, lugha yako, nchi yako kwanza na mengineyo yote ni daraja la pili sasa wewe kwa kuandika kiingereza wakati sisi sote hapa ni watz tayari unaonyesha mapungufu ktk fikra zako, sasa utawezaje kuanza kufikiria kukomesha rushwa kama unathamini wageni kuliko wenyeji????? watu kama ninyi na akina mwanakiji ni sarakani ktk nchi yetu!

the previous recommendation still stands..
 
Huu ni mfano tu wa matatizo mengi yanayoendelea kwenye hoteli hizi za kitalii hasa huko Zanzibar ambako mahoteli ya kitalii yanayomilikiwa na wa Italia.

Nakubaliana nawe mkuu, ukifika kule Kiwengwa Hotel na Bravo Hotel huko Zanzaibar weusi hawaruhusiwi kufika huko labda uwe na rafiki yako wa kizungu au unafahamiana na wafanyakazi wa pale. Mahoteli haya yako kama km 3 toka mjini na kwenye beach nzuri kabisa. Mbaya zaidi mahoteli haya booking inafanyikia Italia na malipo yote yanafanyikia Italia. Ukitaka kwenda kwenye hizo Hotel wanakwambia ingia kwenye internet ulipie online. Sasa najiuliza Serikali ya Zanzibar haiyafahamu haya? Ina maana hata kodi hawa jamaa hawalipi maana malipo hayafanyikii hapa. Huu nao ni ufisadi mwingine inawezekana kabisa kuna wakubwa wanakula pamoja na hawa mamafia wa Kiitaliano. Afrika sijui tuna laana gani jamani, kwa wazungu huku kwao hakuna ujinga kama huo ila wakija kwetu kwakuwa walishajua akili zetu zilivyo wanatu-manipulate wanavyotaka. Ukisema sana unaambiwa usiwabughudhi wawekezaji. Jamani kama uwekezaji ndo huo mimi naona hautufai hata kidogo. Maana kodi hawalipi, ndege wanazopanda ni za kwao, hoteli wanayofikia hawa jamaa ni ya kwao, sasa sisi tunapata nini? Au dada zetu kwenda kujiuza kwao ndo faida kwetu? Hii si faida hata kidogo bali ni kuongeza laana tu kwani zinaa huleta laana. Nafikiri sasa ni wakati wa kuamka kwenye usingizi huu wa pono. Usiku umeendelea mno sasa mchana umekaribia.
 
Jamani mie nilie tu mtoto wa KAYUMBA.
Ndani ya nchi yako unanyimwa haki yako ya kupumzika na kustarehe baada ya kazi?
Haishangazi kuona WABUNGE WETU walivyozuiliwa kuingia ktk hotel MOJA huko serenget kwamba HAWANA HADHI YA KUIJAGUA..
Kuna haja ya kufikiria upya ..............
 
hahaha, jamaa mmoja hivi ananifanya nicheke hapa, tulikuwa tunadiscuss hiyo. anasema ati tatizo wabongo wengine washamba mno, wanaboa na wanakua sio wastaarabu, mazingira yale wanakuwa ni wageni na wanakuwa kama kero kwa watu waliozoea ustaarabu. amekandamiza zaidi hasa zenji kuwa ati hata yeye angekuwa na hotel yake, anajua duniani kuna ugaidi, akashangaa mtu anakuja amejaa mindevu uso mzima, na kanzu ndeefu, au kavaa ushungi anaonekana vimacho tu, angempiga stop.

KWA UPANDE WANGU SIUNGI MKONO KULETA UBAGUZI HUU. si vizuri. ila, wakati mwingine wenye mahotel wanakuwa na logic fulani. watalii wanajali sana usalama wao, hasa kwenye ulimwengu huu wa ugaidi. hapa hapa bongo osama alikuja akahonga hela weusi wenzetu, wakalipua. juzi tu hapa kulikuwa na mzenji guantanamo bay. watalii wengi ni wamarekani na watu wa western countries ambao wanaogopa sana ugaidi.

Tanzania, to tell you, ina image mbaya duniani kuhusu masuala ya usalama, ndio maana watalii wengi wanaprefer kenya kuliko hapa pamoja na kwamba vivutio vingi viko hapa bongo.wabongo tumetangaza hadi tunachoka watalii hawaongezeki. kisa ni mtazamo negative walionao western countries against muslims. na Tz ina waislam wengi zaidi ambao mara nyingi tu wamekuwa wakiandamana na usalama hapa ni mchache sana kusema ukweli. hivyohivyo na zanzibar, watu wanaenda kwa uangalifu sana. lolote linaweza kutokea. osama na kundi lake walishatangaza kuwaua wamarekani na marafiki wa israel popote pale duniani including tz. hivyo, watalii wanataka kujua kama osama hajalipa hela magaidi kuwalipua hapa.

tz kuna watu wana hela nyingi na hazijulikani wanazipataje. hao kina Rostam aziz na kina manji, hela zingine pamoja na kwamba wamefisadi nchi yetu, inawezekana wanazipata kwa kina osama. mpaka nchi yetu itakapojisafisha kuwa inawalinda watalii ndo mambo haya hayatakuwepo, hakuna mtu anayetaka kupoteza mtaji wake wa hotel kwasababu hotel yake imelipuliwa ili kuua mmarekani mmoja. hawakatai kwasababu wabongo ni wachafu au nini, wanakataa kwasababu wabongo wengi hawaaminiki kwa mambo ya usalama wa hotel.

kikwete ameonekana mstari wa mbele kusapoti iran(bad image tayari), kikwete anamsapoti gaidi rais wa sudan(ambako osama alifanya sana makao previously), waislam walishaandamanaga hadi ubalozi wa marekani kulaani mambo ya iraq na palestine(egypt hata hawajafanya hivyo, ndo maana kwa mwaka wanapata watalii si chini ya milioni kumi), na ile kusoma tu kwenye cia fact book kuwa waislam tz ni wengi kuliko wakristo, watu hawaielewi kabisa hii nchi. cha maana, waislam wajue kuwa, udini wa kiextremist ni hasara, sio faida. hata mimi kama mtu amekuja hotelini kwangu na ndevu kama osama, ana kanzu kama hotelini kwangu kuna msikiti, au hata identity halisi, inabidi apigwe stop ili hotel zangu zisipate jina baya. nahitaji kufanya biashara aseee.
 
Exposure ya hao managers ni ndogo mno. Angeulizwa kuna terrorist wangapi wenye ngozi black au watanzania waliyo kwenye wanted list. Wengi wao wana ngozi nyeupe. I would not be surprised that some of their guests might be terrorist cooling off their heels.
 
Kweli huyu mwenye hotel ni lazima awajibike kwa kutudhalilisha. Mzungu ana label? je anapekuliwa? Kwa hiyo rangi ndio ticket ya kutokuwa terrorist? HUU NI UPUUZI MTUPU!
 
:confused:WHEN THE BLIND RULE THE BLINDES
Heshima mbele wakuu... ukweli ni kwamba hii mambo ya ubaguzi kwa sasa ni kila mahali.... nenda hata pale Mlimani city, kuna maduka ukiingia kuna walinzi wanakuwa aimed kukuangalia wewe.... sikatai kwamba kuna vibaka lakini kuna ways to control that than the way they are doing now sababu kwa kweli inatia aibu. kibaya zaidi watu wanaokuwa mstari wa mbele kutubagua ni waswahili wenzetu tena wanakuwa wakali kuliko hata mabosi wao.... SHAME ON THEM!!
 
Tukio ni la kweli na wenyewe wamekili siku saba za nini??? na ukishapata hayo maelezo ya kupika je utafanya nini au ndo funika kombe mwanaharamu apite??? huu nao ni udhaifu pia, Hivi hoteli sasa yamilikiwa na nani?
 
Security concerns or intra racial racism?

``Since terrorists have no labels, the management decided to restrict an influx of local people into the lodge,`` the hotel boss noted.

Ushasema terrorists have no labels, then una ji contradict kwa kusema una restrict influx ya locals, kama terrorists hawana label utajuaje kwamba unaowaruhusu sio terrorists?

Badala ya kutafuta njia itakayo wa identify terrorist wanaamua kutokana na uzembe kukataza waafrika weusi wote.

That is, if their story is legitimate, and it may very well not be at all!
 
Kuna watakaochagua kuzipiga mpaka waruhusiwe, hawa huishia kuitiwa security na kutolewa ngeu kama sio kuuawa.

Kuna wengine wanapigana kwenye sheria huko na ma lawsuit (huyu jamaa angekuwa katika lawsuit society yenye money hungry lawyers angekuwa anachekelea tu sasa hivi) au kuwashtaki kwa mawaziri huko.

Mara nyingine inafaa kutumia akili zaidi kuliko nguvu.
 
Hizi hoteli alipewa Kotak...fisadi kishenzi! Alishindwa kuzifanyia matengenezo hizi hoteli kama walivyokubaliana na serikali na ilikuwa anyang'anywe!
Sasa hao ma terrorist kweli waende Manyara kulipua! Na hao mameneja wana utaalam gani wa kujua huyu ni terrorist na huyu sio.Mtu kaja na familia yake,sasa hayo mabomu kamfunga mwanawe au mkewe! Kwani yule shoe bomber si alikuwa ni mzungu? Timothy Mc Veigh nae si alikuwa mzungu?
Hapa viongozi wamezubaa sana.Namsifu waziri wa Maliasili angalau alienda kujionea mwenyewe na kuwabwatukia.
Vitendo kama hivi ni vingi sana hapa.Zanzibar huko kwenye mahoteli ndio usiseme,tena wala hubaguliwi na mzungu,ni mweusi mwenzako.Wa South Africa ndio usiseme,ukienda Masaki sio tena kama zamani,eti ni sehemu wanakaa matajiri tuu,siku hizi wanaufanya ndio mji wao,maana kuna restaurants huko,hata shoprite wameweka duka huko...maofisi mengi sana yako huko.Baada ya miaka kama kumi,kutakuwa na mabadiliko makubwa sana huko,maana hata manispaa wamebadilisha sheria uwa sasa hivi kwenye kiwanja kilichokuwa na nyumba moja zamani sasa hivi wanajenga apartments.Ukienda mswahili unataka kununua unaambiwa 300,000 usd,mzungu au mhindi anaambiwa 200,000 au 250,000 usd! Wanakaa wenyewe,na viongozi wapo wanaangalia tu,kwa sababu nao wanazo kama hizo!
 
Mimi siamini kama kuna hoteli inayoweza kuwa na policy ya kuzuia watu weusi nchini Tanzania. Kuwa makini nao, ndiyo lakini kuwazuia hapana. Kuzuiwa mtu mmoja si lazima itokane na ubaguzi. Inabidi wazuiwe wengi zaidi ambao wana stahili ya kutumia hizo huduma ndiyo tuseme kuna ubaguzi.

Swali ambalo wengi tunalipiga chenga ni jee mwenye hoteli ana haki ya kuchagua nani ambae ataruhusiwa kupata huduma yake? Je, mwenye hoteli akisema kuwa huduma za baa zitatolewa kwa wale waliopanga vyumba na wanachama wa klabu yake napo ataonekana ni mbaguzi?

Najua vitendo hivi vinakera. Lakini wakati tunalalamika ni vyema tukiwageukia ndugu zetu na kuwaambia kuwa vitabia vyao vinatuharibia wengi! Hakuna mfanyabiashara atakaependa wateja wake watembee kwa hofu ya kushambuliwa au kuibiwa wakiwa katika eneo lake. Tembea na kamera yako waziwazi katika fukwe zetu saa za jioni halafu uone yatakayokupata! Hii haipaswi kuwa hivi. Kwetu wenyewe na hasa kwa wageni wetu.

Amandla....
 
Mimi siamini kama kuna hoteli inayoweza kuwa na policy ya kuzuia watu weusi nchini Tanzania. Kuwa makini nao, ndiyo lakini kuwazuia hapana. Kuzuiwa mtu mmoja si lazima itokane na ubaguzi. Inabidi wazuiwe wengi zaidi ambao wana stahili ya kutumia hizo huduma ndiyo tuseme kuna ubaguzi.

Swali ambalo wengi tunalipiga chenga ni jee mwenye hoteli ana haki ya kuchagua nani ambae ataruhusiwa kupata huduma yake? Je, mwenye hoteli akisema kuwa huduma za baa zitatolewa kwa wale waliopanga vyumba na wanachama wa klabu yake napo ataonekana ni mbaguzi?

Najua vitendo hivi vinakera. Lakini wakati tunalalamika ni vyema tukiwageukia ndugu zetu na kuwaambia kuwa vitabia vyao vinatuharibia wengi! Hakuna mfanyabiashara atakaependa wateja wake watembee kwa hofu ya kushambuliwa au kuibiwa wakiwa katika eneo lake. Tembea na kamera yako waziwazi katika fukwe zetu saa za jioni halafu uone yatakayokupata! Hii haipaswi kuwa hivi. Kwetu wenyewe na hasa kwa wageni wetu.

Amandla....

Mkuu Fundi Mchundo, heshima mbele.

Labda sijakuelewa vizuri, unasema huamini kwamba kuna policy kama hiyo, mbona wenyewe wamekubali?

Two of its senior officials - Group Operations Manager Fred Tenga and General Manager Hamis Juma... saying ``Since terrorists have no labels, the management decided to restrict an influx of local people into the lodge,`` the hotel boss noted. A panicky Tenga apologized and said the policy was being withdrawn with immediate effect.

Na wamezuiwa wengi, kijumla jumla, sio mmoja. Sasa sijui kwa nini unasema "...inabidi wazuiwe wengi zaidi ambao wana stahili ya kutumia hizo huduma ndiyo tuseme kuna ubaguzi." Labda sijakuelewa kwa kweli.

Halafu kuhusu hilo "swali tunalolipiga chenga" la haki ya mmiliki kujiamulia wateja wawe wanachama au waliopanga vyumba, nadhani hilo swala ni muhimu sana lakini sidhani, Fundi Mchundo, kama linahusika hapa. Na hata hilo la wizi wa kamera za watalii, hilo nalo ni tatizo lakini tusilichanganye hapa kwa kuufinika baibui ubaguzi ambao mwenyewe umesema unakukera. Wengine tanaona ubaguzi sio unakera, la, unavunja sheria za nchi.

Kwa hiyo nadhani, Fundi Mchundo, hayo mengine sio kwamba tunayapiga chenga, hayapo uwanjani hayo. Huyu mmiliki hapa hakusema amekatalia mtu kwa sababu hakukodi kitanda pale, la, ni kwa ajili ya rangi yake, nukta.
 
UbungoUbungo naona akili yako imekosea njia kidogo au unafikiria kwenye dini zaidi hivi hujui kuwa kwa sasa kenya ndio inatisha kwa usalama wa watalii, kwa rank gani ya kusema tanzania ina usalama mdogo kuliko kenya?

Watalii hawaji kwa kuwa watu wanaolipwa kufanya matangazo hawafanyi na kama unmengalia taharifa ya CAG leo utadhibitisha hilo watu wanalipwa lakini hakuna ushaidi wa kutosha kuwa matangazo yalifanyika.

London watu walipewa mapesa kibao wameweka vibango viwili tu halafu wanadai rundo la mapesa, jamani tusijidhdlilishe kiasi hicho hakuna mtanzania tena umasaini anayeweza kuwa gaidi, huyo wa zanzibar fuatilia asili yake utagundua kuwa perhaps alidanganywa au DNA yake si ya tanzania.

Hapa serikali itakaa kimya wala haitasema kitu wakati watu wamedhalilishwa, pia sisi watanzania ni wapole sana kwa neno la heshima otherwise naweza kusema ni wajinga maana jamaa alikuwa ametoka kwenye umasikini huyo kwa kudai fidia ya kunyimwa haki yake ya kwenda anapotaka ndani ya tanzania provided hakuvunja sheria na hakuna sheria yeyote iliyovunjwa kwa yeye kwenda hapo

Watanzania tuamke na kuanza kudai fidia kwa vitu vidogo kama hivyo, tuige mfano wa Wapale kwa kupenda kesi kwani ndio njia pekee ya kufanya watu wakawa na responsibility.
 
Mkuu Fundi Mchundo, heshima mbele.

Labda sijakuelewa vizuri, unasema huamini kwamba kuna policy kama hiyo, mbona wenyewe wamekubali?

Two of its senior officials - Group Operations Manager Fred Tenga and General Manager Hamis Juma... saying ``Since terrorists have no labels, the management decided to restrict an influx of local people into the lodge,`` the hotel boss noted. A panicky Tenga apologized and said the policy was being withdrawn with immediate effect.

Na wamezuiwa wengi, kijumla jumla, sio mmoja. Sasa sijui kwa nini unasema "...inabidi wazuiwe wengi zaidi ambao wana stahili ya kutumia hizo huduma ndiyo tuseme kuna ubaguzi." Labda sijakuelewa kwa kweli.

Halafu kuhusu hilo "swali tunalolipiga chenga" la haki ya mmiliki kujiamulia wateja wawe wanachama au waliopanga vyumba, nadhani hilo swala ni muhimu sana lakini sidhani, Fundi Mchundo, kama linahusika hapa. Na hata hilo la wizi wa kamera za watalii, hilo nalo ni tatizo lakini tusilichanganye hapa kwa kuufinika baibui ubaguzi ambao mwenyewe umesema unakukera. Wengine tanaona ubaguzi sio unakera, la, unavunja sheria za nchi.

Kwa hiyo nadhani, Fundi Mchundo, hayo mengine sio kwamba tunayapiga chenga, hayapo uwanjani hayo. Huyu mmiliki hapa hakusema amekatalia mtu kwa sababu hakukodi kitanda pale, la, ni kwa ajili ya rangi yake, nukta.

Mkuu soma vizuri. Taarifa inasema"local people". Haizungumzii watu weusi! Maana yake ni kuwa mmatumbi asiyekuwa local ataruhusiwa. Taarifa imekuzwa pasipo sababu.

Hauwezi kuzungumzia hiki unachokiita ubaguzi bila kuzungumzia sababu ambazo zinazoweza kuwafikisha hapo.

Profiling ipo hata kama hatupendi. Naamini njia nzuri ya kukomesha tabia kama hii ni kuzisusia sehemu hizo wala si kulazimisha kuingia.

Amandla.......
 
Back
Top Bottom