Quran: Huyu Issa bin Maryam ni nani? Kwanini aitwe hivi?

Uislam unasomwa kwa hatua ,ni lazima usome foundation ndo utaelewa mambo mazito kama hayo,kumjua issa bin mariam ni sawa na kumpa mtihani wa fom 6 mtt wa class one,Unaonekana huijui uislam kiundani ,anza kujifunza kutia udhu ndo uje umsome issa bin mariam

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maomba mnaojua Kuran naomba mnijibu maswali haya yanayonitatiza:
Kuran inaelezaje kuhusu kupaa kwa Issa bin Mariam, kwanini alipaa na asingekufa kawaida!?
Atakaporudi siku ya mwisho, atakuja kuhukumu au atakuja kuuawa?
Kama alikuwa mtume wa kawaida, kwanini asingezaliwa kwa njia za kawaida kabisa kama walivyo binadamu wengine?

Hizo hadithi tu mkuu
Zisikuchoshe
 
Bora ya Issa kazaliwa vp kuhusu Adam??? Atakavorud hatakuja kuhukum kwn yey cyo hakimu (yaan Mungu) Bali atawapinga vikal woote waliokengeusha mafundisho yake na kumfanya yeye mungu(gods) badala ya kumuabudu Mungu (God).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
quran na biblia vyote ni vitabu vya Mwenyezi Mungu, na vyote vinaelezea historia ya uumbaji wa dunia, manabii na mitume. swali kati ya quran na biblia kitabu kipi kilianza kuandikwa? na kati ya vitabu hivyo viwili tukifahamu kipi kilianza kumuandika huyu Mariam ina maana kitabu kingine ni kiongo?
Kuna watu wanaamini Mungu wa Agano la kale na Agano jipya ni Miungu miwili tofauti,Mungu wa Agano la kale alikuwa mkali na Mungu wa Agano jipya anaonekana ni mpole.
 
Kuna watu wanaamini Mungu wa Agano la kale na Agano jipya ni Miungu miwili tofauti,Mungu wa Agano la kale alikuwa mkali na Mungu wa Agano jipya anaonekana ni mpole.
Umekosea kidogo tu.
Mungu ni yuleyule ila katika Agano la kale alitaka kujidhihirisha wa watu ili wamtbue kuwa ndiye aliyeumba mbingu na mchi, ana nguvu kupita wote, ukosea ni mkali, anaweza kuhaisha na kufisha, ni mkali na pia ni mpole nk.
Baadae aka ahidi kuweka Agano jipya na binadamu kwani ameisha julikana sasa na haitaji tena kutisha watu au kuua au kuwa mkali.
Soma anavyoahidi katika Yeremia 31 : 31.
Hivyo katika Agano Jipya Mungu ni Mpole sana kwa Wachamungu na Kwa waovu.
Wale waovu amewapa mda wa kutubu, kama wakikaidi kutubu basi atawaondoa katika ufalme wake siku ya mwisho, na kuwaashibu pamoja na Ibirisi Shetani.
Ndio maana katika Agano la kale Mungu anaagiza kuwa watu waaifanye vita na bimadamu wenzao, warumie njia ya mapatano kama watakosana (ndugu alikikukosea liambie Kanisa, usifanye vita naye)
Anasisitiza katika Agano Jipya kuwa vita ya bimasamu iwe dhidi ya Ibirisi Shetani na jamaa zake, majini, mapepo, mizimu, vindondocha, uchawi nk.
Ndio maana unaona Wakristo hawapendi vita ya mtu na mtu na kamwe hawata iruhusu labda kwa kujitetea na kifo.
Ndivyo ilivyo mpendwa katika Kristo.
Tz mbongo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swala la imani za kidini ni tata sana!, swala la uwepo wake ni jepesi sana kuliamini.Tatizo kuu ni pale baadhi ya watu wanapojikabidhi mamlaka ya kuwashawishi watu kumtii kwa njia wanazozitaka wao!.Hapo ndipo baadhi ya watu wenye logic za ndani mfano Wachina wanapolikataa jambo hilo.Kihulasia kwa sisi wapagani (tusiokubali dini za mapokeo) tunaona mkanganyiko ulio wazi!.Kwani Kuhusu imani ya kuwa Mungu ndiye mwenye mamlaka makuu linaweza likaingia akilini,lakini pale walioanzisha imani hizo wanapojumlisha mienendo ya tamaduni zao kuwa ndio njia za kimaisha kwa waumini hapa si kweli!.Kwani inafika mahala ili uonekane muislam safi basi uishi kwenye tamaduni za kiarabu!,au mkiristo safi basi ukopi maisha ya kizungu!.Tuzinduke Waafrika,maswala ya imani yajikite kwenye kuaminisha ukuu wa mungu lakini njia za kuabudu wajichagulie watu kulingana na tamaduni zao!

Sent using Jamii Forums mobile app
Yani watu kujichagulia njia zao wenyewe za kuabudu unaona ni sawa ila mtu kuamua kuabudu njia iliyobuniwa tofauti na tamaduni ndio sio sahihi.

Aisee! hii napata nayo shida kuingiza kichawani,maana huko kuabudu kwenyewe tu tumejitungia lakini et ukifuata walivyotunga watu wa jamii nyengine inakuwa potofu.
 
Umekosea kidogo tu.
Mungu ni yuleyule ila katika Agano la kale alitaka kujidhihirisha wa watu ili wamtbue kuwa ndiye aliyeumba mbingu na mchi, ana nguvu kupita wote, ukosea ni mkali, anaweza kuhaisha na kufisha, ni mkali na pia ni mpole nk.
Baadae aka ahidi kuweka Agano jipya na binadamu kwani ameisha julikana sasa na haitaji tena kutisha watu au kuua au kuwa mkali.
Soma anavyoahidi katika Yeremia 31 : 31.
Hivyo katika Agano Jipya Mungu ni Mpole sana kwa Wachamungu na Kwa waovu.
Wale waovu amewapa mda wa kutubu, kama wakikaidi kutubu basi atawaondoa katika ufalme wake siku ya mwisho, na kuwaashibu pamoja na Ibirisi Shetani.
Ndio maana katika Agano la kale Mungu anaagiza kuwa watu waaifanye vita na bimadamu wenzao, warumie njia ya mapatano kama watakosana (ndugu alikikukosea liambie Kanisa, usifanye vita naye)
Anasisitiza katika Agano Jipya kuwa vita ya bimasamu iwe dhidi ya Ibirisi Shetani na jamaa zake, majini, mapepo, mizimu, vindondocha, uchawi nk.
Ndio maana unaona Wakristo hawapendi vita ya mtu na mtu na kamwe hawata iruhusu labda kwa kujitetea na kifo.
Ndivyo ilivyo mpendwa katika Kristo.
Tz mbongo

Sent using Jamii Forums mobile app
Maelezo yako yanaonesha kuwa Mungu amebadilika kutoka kuwa mkali hadi kuwa mpole,hivyo mwanzo hakuwa na upole.

Maelezo kama hayo ndio sababu ya watu wengine kuamini kuna Miungu miwili tofauti.

Na hata ukiangalia wakristo hawakubaliani na suala la Mungu kuwa mkali bali humtambua ni mpole tu,ukimpa maaandiko yenye kuonesha ukali wake huishia kusema hilo ni Agano la kale ila hakubali ukali wa Mungu.
 
Ukielewa chimbuko La dini hizi utakuwa huru Sana. Kabla ya kutumia upanga kusambaza uislam Mohamad alijaribu kuwaingia wakristo kwa mafundisho yake nao wakamkataa. Hivyo Basi, aliiba/alikopi baadhi ya hadithi na mafundisho yao kwenye mahubiri yake, ili iwe rahisi kuwaingia. Ndio maana unaona baadhi ya hadithi kwenye kuran na biblia zinafanana kiasi, with minor twists. Technique tu, Hakuna jipya. Hata wakristo wenyewe walikopi wayahudi, ambao walikopi wapagani. Total mess, Ila it's good to know, otherwise tutaendelea kubishana Kama swala wenye vichaa
Kuongea ni rahisi ila kuyaweka hayo kwenye uhalisia ndio shida.
 
kwanza kabisa niwaweke waz kwamba huyo Isah bin maryam ni mtu tofauti kabisaaa na Yesu kristo.....in short Yesu kristo ni level nyingine kabisa na mziki wake duniani unaeleweka yaani ukilitaja hilo jina kwa mtu mwenye majin ndo utajua vzr jns majin yapatavyo tabu but kuhusu Issah ni hadith inayotia shaka kwakweli
Basi mkuu ingekuwa haina haja ya mtu mwenye mapepo kwenda hadi kanisani ili litajwe jina Yesu ndio aondokewe na mapepo,angeweza kufanyiwa au hata kufanya mwenyewe nyumbani kwa kuita tu "Yesu" na mapepo kukimbia.

Unazungumziaje hili?
 
Tangu lini mtu akajitibu mwnyewe?.....Pia tambua kwamba jina la Yesu limebeba authority kwa mwenye kuifaham hiyo authority na akaiamini kisawasawa, nao ndio hawa waliopewa Authority hiyo yaani waaminio na kubatizwa nakumkili Yesu kristo kwamba ndiye Mwana wa Mungu nakuziamin kaz zake kisha wakajitenga mbali na dhambi na kila aina ya uchafu huku wakifunga kuomba na kutafakari neno.
 
Duh! kumbe masharti kama yote,mi nilidhani kwa uzito wa hilo jina ukitaja linatenda miujiza kumbe ni kwa watu maalumu.
 
Duh! kumbe masharti kama yote,mi nilidhani kwa uzito wa hilo jina ukitaja linatenda miujiza kumbe ni kwa watu maalumu.
Hata ww unaweza endapo utaamua bila kulazmishwa kumuamin nakubatizwa kisha kuwa mfuasi wake kwakuyaacha mabaya its very simple na ndiyo maana pepo halitoki nakutii kwa jina lolote lile duniani Isipokuwa kwa jina la Yesu......hakuna mahali popote pale mtu anaweza kutoa pepo ati kwa jina la ISSA BIN MARYAM😂
 
Hao watu wenye hizo sifa wanahesabika hapa duniani na ndiyo maana tunaona watu wakienda makanisani kutolewa mapepo kwa maana hawana hizo sifa.

Na cha ajabu tunaambiwa kuna manabii wa uongo ila wote tunaona wanatenda miujiza na hutaja jina la Yesu.
 
Maelezo yako yanaonesha kuwa Mungu amebadilika kutoka kuwa mkali hadi kuwa mpole,hivyo mwanzo hakuwa na upole.

Maelezo kama hayo ndio sababu ya watu wengine kuamini kuna Miungu miwili tofauti.

Na hata ukiangalia wakristo hawakubaliani na suala la Mungu kuwa mkali bali humtambua ni mpole tu,ukimpa maaandiko yenye kuonesha ukali wake huishia kusema hilo ni Agano la kale ila hakubali ukali wa Mungu.
Hapana na ndio.
Hapana, kwamba ni Miungu wawili tofauti.
Ndio, kwamba lile lilikuwa Agano la Kale.
Kumbuka katika Agano la Kale Mungu huyo huyo, alimpa Musa Amri Kumi ili watu wake wazishike na kuzifuata.

Katika Agano Jipya Mungu huyohuyo amezungumza kupitia Nafsi ya Yesu Kristo kuwa sasa ni Amri mbili tu za kuzishika na kizitekeleza. Na sio kumi tena, Amri hizo ni hizi hapa

Mathayo 22
33 Na makutano waliposikia, walishangaa kwa mafunzo yake.
34 Na Mafarisayo waliposikia ya kwamba amewafumba kinywa wale Masadukayo, walifanya shauri pamoja.
35 Mmoja wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu;
36 Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?
(1). 37 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.
38 Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
(2). 39 Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
40 Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.

Mungu aliahidi kuliacha Agano Jipya kwani tayari alisha jitambulisha kwa watu wake na walikuwa wanamjua tayari.
Hivyo mambo ya kupigana hayakuwa na maana tena.
Agano Jipya linasisitiza sana upendo kwa Mungu na Jirani yako.
UPENDO

Tunasoma katika Yeremia 31

31 Angalia, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.
32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema BWANA.
33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema BWANA; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
34 Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue BWANA; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema BWANA; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.
35 BWANA asema hivi, awapaye watu jua, ili kuwa nuru wakati wa mchana, na amri za mwezi na nyota, ili kuwa nuru wakati wa usiku, aichafuaye bahari, hata mawimbi yake yakavuma; BWANA wa majeshi, ndilo jina lake;
37 BWANA asema hivi, Kama mbingu zikiweza kupimwa, na misingi ya dunia ikiweza kugunduliwa huko chini, ndipo wazao wa Israeli pia nitawatupilia mbali, kwa ajili ya hayo yote waliyoyatenda, asema BWANA.

Agano Jipya ndilo linalotumika kwa sasa na Wakristo.
Wakristo wanasoma pia Agano la kale kwa minajiri ya kujua mambo mbali mbali kama vile ya kujua

Historia ya Mwanzo wa Imani yao.
Dini ya Ibrahimu na Uyahudi ambazo zilikuja kuasisi Ukristo baadae
Namna ya uumbaji ulivyofanyika na Mungu.
Mungu na utambulisho wake kwa Taifa la Israeli.
Amri za Agano la Kale.
Sifa za Manabii wa Mungu katika Agano la kale.
Miujiza na nguvu za Mingu.
Ukoo wa binadamu wa kwanza hadi kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
NAKADHALIKA.

Hivyo ukiuliza, Mbona Mungu wenu Yehova aliamrisha kuuwa watu ?
Utajibiwa matukio hayo ni ya Agano la Kale.
Sasa hivi amri ya Upendo ndio inayotawala.
Sasa hivi Mungu hataki tena kuchinjana.
Adui yetu sio binadamu tena, bali ni Ibirisi Shetani, huyo ndio wa kimpiga vita.

Ndivyo ilivyo mtu wa Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao watu wenye hizo sifa wanahesabika hapa duniani na ndiyo maana tunaona watu wakienda makanisani kutolewa mapepo kwa maana hawana hizo sifa.

Na cha ajabu tunaambiwa kuna manabii wa uongo ila wote tunaona wanatenda miujiza na hutaja jina la Yesu.
kumbe kama unaamin wapo ila wanahesabika waswas wako ni nn unapowaona manabii wa uongo je hukumskia Yesu aliposema siku ya mwsho watakuja watu wakidai tulitoa pepo kwa jina lako nitawaambia ondoken nyie c wangu?😊
 
hili ni suala ambalo limekuwa likinitatiza sana. kwenye quran kuna nabii anaitwa Issa Bin Maryam. nmekuwa nikimsoma mara nyingi na kusoma hadith mbalimbali za quran. nachojiuliza ambacho naomba Mauramaa mnisaidie kwa nini huyu nabii aliitwa kwa jina la mama yake na si baba yake?

je katika uislamu kuna utaratibu huo?kuna nabii mwingine ambaye aliitwa kwa jina la mama yake badala ya la baba yake? tusaidiane tafadhali kwa namna ya elimu ya uelewa mzuri, kwa hikma na busara. pasipo jazba na kashfa.
Inavyoonekana haujawahi hata kusoma quran kwa nini nimekwambia hivi ? Ni kuwa haujui tofauti ya hadithi na quran zina utofauti gani.eti hadithi za kwenye quran ili uonekane umesoma THEOLOGY? na wakati hata kuandika tu Ulamaa unadika Uramaa? Nenda kwanza kasome kiswahili kisha ndiyo uje uulize swali lako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom