Quote From: The President Dr. Jakaya M. Kikwete!

Zitto kiboko ya JK na Pinda mpaka sasa wanahaha kudilute hoja ya Zitto ya kuwataka wabunge kumpigia waziri mkuu kura ya kutokuwa na imani nae ndio msingi wa haya yote tunayo yaona mara kamati kuu ya ccm,mara nilikuwa na dhamira ya dhati kuimarisha office ya CAG,mara nimefurahiya mjadala bungeni wa report ya CAG basi ni kuhaha tu mpaka raha.
 
- Nimesema mara nyingi sana kwamba siasa ni kama biashara ya utumbo, huwezi kuifanya huku unaogopa harufu, I mean unajua how long nimekuwepo hapa JF, huwa yanakuja na kupita ila ukweli unasimama mpaka mwisho,

- Kwamba Dr. Jakaya M. Kikwete, huenda ni the best kuliko wote waliopita, I have said that before na ninasema tena now!, unaposema kiongozi mmoja hafai unamlinganisha na wanaofaa, ndio maana ninasema anawazidi wote waliopita! Na mfano mdogo ni hii CAG, mnasema imekuwepo toka Awamu ya kwanza, mna maana toka enzi zile tunanunua Mandege mabovu ya ATC, Gapex, BOT, mnasema CAG walikuwepo?

William.
EPA,RICHMOND Mbona kaufyata hata kuwapa wezi muda warejeshe fedha, NYIE, BABA ZENU JK WENU Wote Pambaffffffff
 
Kwenye hotuba ya leo JK alianza stori ya kasheshe la bungeni alipofika katikati mpambe wake akamletea Vi-MEMO kama viwili hivi akaipindisha akaanza stori za ripoti ya CAG ya huko nyuma halafu akaipotezea. Nilikuwa nasubiri aseme kilichojiri bungeni na hatua ambazo anachukua kwani allisema aidha mawaziri wawajibike au wawajibishwe halafu akaishia hewani.
 
William, nimesema in the 70's walikuwa wanakuja kukagua ubalozi hapa Washington. D.C. That itself should be an answer kwamba ilikuwepo. Au ulidhania Kikwete ndiye kaiweka? Ameikuta, na kuanzia mwaka 2006 alikataza ripoti zake zisitolewe hadharani, wewe unafikiria ni kwa nini? Ningemshauri Kikwete aache unafiki na harakati za kujitafutia umaarufu (cheap popularity.)

Jasusi, hapa sasa unataka kutupiga fix...fix za aina hii ziliwezekana wakati wa Nyerere na sio kipindi hiki cha Informative Era! Yaani unataka kutuambia wakati wa Nyerere, Mwinyi na Mkapa ripoti za CAG zilikuwa zinatolewa hadharani na 2006 JK akapiga marufuku?! Uongo mwingine hauna maana hata kidogo!!

Ni kweli kwamba, CAG ilikuwepo tangu zamani lakini ni mabadiliko ya mwaka 2008 (Sheria ya Ukaguzi wa Umma Na. 11 ya 2008) ndiyo yaliyoifanya ofisi ya CAG kuwa huru kiasi hiki. CAG mwenyewe anathibitisha hili katika Dibaji yake, nanukuu: " Uhuru wa kiutendaji wa ofisi yangu kwa kiasi kikubwa umeimarika baada ya kuanza kutumia sheria ya Ukaguzi wa Umma Na 11 ya mwaka 2008.hata hivyo kulingana na viwango vya kimataifa maboresho zaidi yanahitajika hasa kwa upande wa kupanga mishahara na ajira za watumishi wa ofisi yangu ili kuniwezesha kutekeleza majukumu yangu ya kikatiba kwa ufanisi zaidi.

Kutungwa kwa Sheria ya Ukaguzi wa Umma Na. 11 ya mwaka 2008 kumeongeza mawanda ya ukaguzi wangu kwa kunipa madaraka ya kufanya kaguzi nyingine zaidi ya ukaguzi wa kawaida wa taarifa za fedha. Kwa mujibu wa sheria hii natakiwa kufanya ukaguzi wa ufanisi, utambuzi na mazingira na kaguzi mbalimbali maalum kama zinavyojitokeza. Ni matumaini yangu kwamba, kwa kuanzishwa kwa sheria mpya ya Ukaguzi wa Umma, Ofisi yangu itaweza kuimarisha udhibiti wa fedha na kuisaidia Serikali kuimarisha uwajibikaji. Sheria hii pia itaniwezesha kuwa huru katika kulithibitishia Bunge masuala yanayohusu uwajibikaji, uwazi na matumizi bora ya rasilimali hasa kuona kwamba rasilimali hizo zimetumika vizuri kwa kuzingatia uchumi,ufanisi na kama ilivyotarajiwa na kupitishwa na Bunge."

Hivyo, ingawaje ni ukweli kwamba CAG alikuwepo tangu zama hizo, ni kipindi hiki ndipo ofisi hiyo imekuwa huru zaidi. Inasikitisha kuona kwamba hata mtu kama wewe ni miongoni mwa wanaufurahi kuona serikali ikifanya vibaya ili tiketi kwa wengine! Kwamba, zuri linapofanyika ni kutafuta sifa na umaarufu ni kauli mfu inayopaswa kutolewa na mtu asiye na uelewa au mwenye political interests! Hata kama ni kweli bado kuna mapungufu lakini si sahii kubeza hata lile lenye mwelekeo mzuri!
 
Hivi JK yeye si mfujaji wa mali za umma? wapi watu wake wa EPA, wapi genge lake la safari za nje kukagua miradi ya nyanya brazil, wapi ikulu yake kumvua ubunge Lema na gharama kubwa za kurudia uchaguzi, Ampishe mteule halali wa Magogoni Dr.Slaa afanye vitu vyake
 
William, nimesema in the 70's walikuwa wanakuja kukagua ubalozi hapa Washington. D.C. That itself should be an answer kwamba ilikuwepo. Au ulidhania Kikwete ndiye kaiweka? Ameikuta, na kuanzia mwaka 2006 alikataza ripoti zake zisitolewe hadharani, wewe unafikiria ni kwa nini? Ningemshauri Kikwete aache unafiki na harakati za kujitafutia umaarufu (cheap popularity.)

- Tatizo ni kwamba binafsi sikujua kama ilikuwepo kwa sababu sikuwahi kuisikia wala ripoti yake, na wala sikuwahi kusikia Viongozi wakifukuzwa wala kusimamishwa kazi kwa sababu ya CAG, ukweli ni kwamba Dr. JK anahitaji heshima kwamba sasa wananchi wote tunaijua CAG na pia tunajua kwamba tuna viongozi wezi na busara ni kwamba hawakuanza leo, huko nyuma walikuwa wanasamehewa lakini sasa tunakula nao sahani moja!

- Dr. JK anakuwa na heshima kwa sababu kwanza ameruhusu ripoti iwekwe wazi wananchi wote tuione, pili ameruhusu mjadla wa kuwangoa wale wote wanaotuhumiwa wizi na ripoti, ukiweza kunionyesha Awamu iliyowahi kufanya hayo kabla ya Awamu ya Nne, basi nitakubali maneno yako!

- Otherwise, Dr. JK anakuwa the best of all waliopita!

William.
 
Jasusi, hapa sasa unataka kutupiga fix...fix za aina hii ziliwezekana wakati wa Nyerere na sio kipindi hiki cha Informative Era! Yaani unataka kutuambia wakati wa Nyerere, Mwinyi na Mkapa ripoti za CAG zilikuwa zinatolewa hadharani na 2006 JK akapiga marufuku?! Uongo mwingine hauna maana hata kidogo!!

Ni kweli kwamba, CAG ilikuwepo tangu zamani lakini ni mabadiliko ya mwaka 2008 (Sheria ya Ukaguzi wa Umma Na. 11 ya 2008) ndiyo yaliyoifanya ofisi ya CAG kuwa huru kiasi hiki. CAG mwenyewe anathibitisha hili katika Dibaji yake, nanukuu: " Uhuru wa kiutendaji wa ofisi yangu kwa kiasi kikubwa umeimarika baada ya kuanza kutumia sheria ya Ukaguzi wa Umma Na 11 ya mwaka 2008.hata hivyo kulingana na viwango vya kimataifa maboresho zaidi yanahitajika hasa kwa upande wa kupanga mishahara na ajira za watumishi wa ofisi yangu ili kuniwezesha kutekeleza majukumu yangu ya kikatiba kwa ufanisi zaidi.

Kutungwa kwa Sheria ya Ukaguzi wa Umma Na. 11 ya mwaka 2008 kumeongeza mawanda ya ukaguzi wangu kwa kunipa madaraka ya kufanya kaguzi nyingine zaidi ya ukaguzi wa kawaida wa taarifa za fedha. Kwa mujibu wa sheria hii natakiwa kufanya ukaguzi wa ufanisi, utambuzi na mazingira na kaguzi mbalimbali maalum kama zinavyojitokeza. Ni matumaini yangu kwamba, kwa kuanzishwa kwa sheria mpya ya Ukaguzi wa Umma, Ofisi yangu itaweza kuimarisha udhibiti wa fedha na kuisaidia Serikali kuimarisha uwajibikaji. Sheria hii pia itaniwezesha kuwa huru katika kulithibitishia Bunge masuala yanayohusu uwajibikaji, uwazi na matumizi bora ya rasilimali hasa kuona kwamba rasilimali hizo zimetumika vizuri kwa kuzingatia uchumi,ufanisi na kama ilivyotarajiwa na kupitishwa na Bunge."

Hivyo, ingawaje ni ukweli kwamba CAG alikuwepo tangu zama hizo, ni kipindi hiki ndipo ofisi hiyo imekuwa huru zaidi. Inasikitisha kuona kwamba hata mtu kama wewe ni miongoni mwa wanaufurahi kuona serikali ikifanya vibaya ili tiketi kwa wengine! Kwamba, zuri linapofanyika ni kutafuta sifa na umaarufu ni kauli mfu inayopaswa kutolewa na mtu asiye na uelewa au mwenye political interests! Hata kama ni kweli bado kuna mapungufu lakini si sahii kubeza hata lile lenye mwelekeo mzuri!

- Saafi sana yaani hakuna la kuongeza wala kupunguza!

William.
 
Hivi baada ya wabunge kujadili hii report na kutoa mapendekezo yao inabaki kazi ya nani kutekeleza hayo mapendekezo na kama Rais hakuwepo au kama anadharula na nashughuli za serikali zinakuwa zimesimama Willie anasema Rais hakuwepo hivyo ingekuwa vigumu mawazili kusimamishwa anasahau kuwa Urais ni taasisi hata hivyo Rais alishakuwa na hiyo report kwahiyo huo uozo anaufahau,kingine serikali inavyanzo vingi vya habari ikiwemo TISS kwa Rais ambaye yupo smart tulitegemea mambo yote haya anayafahamu hata kabla ya report ya CAG hawa kinaNgeleja na majumba yao tulitegemea wawe walisha hukumiwa jela tangu mwaka jana.Leo JK baada ya kubanwa mbavu anakuja kujisifu kwa kuipa makali ofisi ya CAG badala yakuja kutueleza hatua alizo chukua kweli JK hakuna kitu.

Hapo ndo W.malecela anajichanganya sana na binafsi nahisi ako na ajenda nyingine zaidi ya kusema anamsifia JK, Karibia wiki sasa amekuwa na thread nyingi za kuponda watangulizi na kumsimamisha pahala flani JK pa usafi mno!
 
- Ndivyo wanasiasa wetu walipotufikisha huwa hatuamini anything, siku zote tunaamini kuna agenda inaeleweka!

William.
 
- Tatizo ni kwamba binafsi sikujua kama ilikuwepo kwa sababu sikuwahi kuisikia wala ripoti yake, na wala sikuwahi kusikia Viongozi wakifukuzwa wala kusimamishwa kazi kwa sababu ya CAG, ukweli ni kwamba Dr. JK anahitaji heshima kwamba sasa wananchi wote tunaijua CAG na pia tunajua kwamba tuna viongozi wezi na busara ni kwamba hawakuanza leo, huko nyuma walikuwa wanasamehewa lakini sasa tunakula nao sahani moja!

- Dr. JK anakuwa na heshima kwa sababu kwanza ameruhusu ripoti iwekwe wazi wananchi wote tuione, pili ameruhusu mjadla wa kuwangoa wale wote wanaotuhumiwa wizi na ripoti, ukiweza kunionyesha Awamu iliyowahi kufanya hayo kabla ya Awamu ya Nne, basi nitakubali maneno yako!

- Otherwise, Dr. JK anakuwa the best of all waliopita!

William.

W. malecela,ikiwa wewe hukuwa unafahamu wala hukuwahi sikia watu wanawajibishwa doesnt/couldnt mean haikuwepo. Ikiwa sasa umefahamu still kuna ambao hadi leo hawajajua mambo hizi ama kwa kutofuatilia kwao,watakapokuja anza fuatilia mambo haya na kufahamu haitakuwa sahihi kwao kusema "sijawahi isikia....", Still kwa namna unavojaribu kumpamba Jk kwa "Dr's" naona wazi ni kujikomba na kujikosha flani kuliko uhalisia wa unachotaka kuelezea/aminisha watu
 
"Nimefurahishwa na mjadala wa uwazi ulioendelea Bungeni na kwenye kamati ya wabunge wa CCM; nafurahi kwamba azma yangu ya kuzifanya taarifa za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ziwe zinafanyiwa kazi imeanza kutimia" Mhe. Jakaya M. Kikwete

Hypocritic statement.
Naona aibu kushabikia quote hii. Kweli ukipenda!
 
W. malecela,ikiwa wewe hukuwa unafahamu wala hukuwahi sikia watu wanawajibishwa doesnt/couldnt mean haikuwepo. Ikiwa sasa umefahamu still kuna ambao hadi leo hawajajua mambo hizi ama kwa kutofuatilia kwao,watakapokuja anza fuatilia mambo haya na kufahamu haitakuwa sahihi kwao kusema "sijawahi isikia....", Still kwa namna unavojaribu kumpamba Jk kwa "Dr's" naona wazi ni kujikomba na kujikosha flani kuliko uhalisia wa unachotaka kuelezea/aminisha watu
Pamoja sanaaaaa. No research no right to spea.....k
 
".. nafurahi kwamba azma yangu ya kuwawajibisha Wabadhilifu na wasiowajibika imetimia kama nilivyotamka wakati nazindua Bunge" Mhe. Jakaya M. Kikwete

Kama ingekuwa hiyo quote ningejadili vinginevyo tutaidhalilisha JF.
 
W. malecela,ikiwa wewe hukuwa unafahamu wala hukuwahi sikia watu wanawajibishwa doesnt/couldnt mean haikuwepo. Ikiwa sasa umefahamu still kuna ambao hadi leo hawajajua mambo hizi ama kwa kutofuatilia kwao,watakapokuja anza fuatilia mambo haya na kufahamu haitakuwa sahihi kwao kusema "sijawahi isikia....", Still kwa namna unavojaribu kumpamba Jk kwa "Dr's" naona wazi ni kujikomba na kujikosha flani kuliko uhalisia wa unachotaka kuelezea/aminisha watu

- Nilidhani utarekebisha record ya nani kati ya awamu zilizopita aliyewahi kuwajibishwa kwa sababu ya CAG ripoti kama tunavyoona Awamu ya nne, badala yake unaniletea ngonjera zile zile mkuu understand kwamba hizi taarabu naziskia kila siku zimesha-expire, wewe weka hoja muhimu kwa taifa, mimi ni jiwe la chuma utajiumiza mwenyewe tu mimi ninaondoka mwendo ni mdundo! ha! ha! ha!

William @DSM City!
 
Back
Top Bottom