Quote From: The President Dr. Jakaya M. Kikwete!

- Yaaani CAG kumbe ilikuwepo toka miaka ya 70? Sasa iweje wengine tuisikie kwa mara ya kwanza majuzi aliposhika Urais Dr. Jk, I mean unasema huko nyuma hakukuwa na wizi? Then how come haikuwekwa wazi tukaiona wote kama sasa?


William.

Hilo suali unapaswa kujiuliza mwenyewe. Hukufanya due diligence kabla ya kukurupuka na kumpongeza Kikwete.


Athante thana Jathuthi kwa majibu murua. Thank you. Wakola muno. Wabeja thana. Wakondya muno. Webale nyo.
 
hayo ni maneno tu-as long hakuna reaction yoyote-watu bado wapo wanakula bata-hio statement haina maana-ni sawa na ahaid za kwenye kampeni
 
- Mkuu Jasusi, naomba kukuuliza in a serious way: CAG ilikuwepo awamu ya kwanza?

William.

Athwaaaaaaaaa maana wakati nathoma government accounting pale Diethiei kurathini wilay ay temeke miaka hiyo tulijifunza habari zake na power yake na tulikuwa tukitayarishwa kwa ajili ya kwenda huko pia. bwaha ha ha ha ha ha
 
- Mkuu Jasusi, naomba kukuuliza in a serious way: CAG ilikuwepo awamu ya kwanza?

William.
William, nimesema in the 70's walikuwa wanakuja kukagua ubalozi hapa Washington. D.C. That itself should be an answer kwamba ilikuwepo. Au ulidhania Kikwete ndiye kaiweka? Ameikuta, na kuanzia mwaka 2006 alikataza ripoti zake zisitolewe hadharani, wewe unafikiria ni kwa nini? Ningemshauri Kikwete aache unafiki na harakati za kujitafutia umaarufu (cheap popularity.)
 
- Kwani CAG imekuwepo kwa muda gani? Maaana hii ni mara yangu ya pili kuisikia, mara yangu ya kwanza ilikuwa Dr. Kikwete aliposhika utawala mambo ya mabalozi walioiba, wengine wakafikishwa kwenye Sheria na wengine walilazimishwa ku-retire na kulipa walizoiba.

- Hii ni mara ya pili nawasikia tena CAG, naomba kukuuliza walianza lini hawa CAG? Mbona huko nyuma kwenye awamu zingine hatukuwahi kuwasikia?

William.

Hakuna lolote.harakati za kuzuia madhara ya upepo tu..kama angekuwa anajua maana halisi ya taarifa hizo za CAG kujadiliwa kwa uwazi angekuwa ameshawaadabisha mawaziri wote wabadhirifu toka hizi ripoti zilipoanza kujadiliwa...isingekuwa hiki kimbunga walichoanzisha akina zito hata huo ubadhirifu kwenye ripoti za mwaka huu ungeachwa upite tu,which makes JK's reasoning a no-brainer..huwezi kusifia uamuzi wako wa kununua neti miaka 6 iliyopita,wakati ulikuwa umeifungia kabatini mpaka rafiki yako alipokuelekeza mwaka huu jinsi ya kuitumia...idiocy.
 
Nimegundua kuna watu mnaweka maslahi ya siasa na chama. Akifanya vizuri JK msifie tu.
Kuna kila dalili mipango ya JK ikifanikiwa CCM chati inapanda wakati huohuo CDM chati inashuka

Mtu anasifiwa kwa matendo si maneno. So far hapo ni maneno. Matendo ni pale watu watakapo wajibishwa. Na hivi nikuulize kwani mwaka huu ndiyo mara ya kwanza report ya CAG kutolewa na madai ya rushwa? Hizo report zingine zilifanyiwa kazi gani? I will give him his credit when credit is due. So far ni maneno tu na experience inaonyesha hato fanya kitu unless aonyeshe otherwise.
 
Hearsay! Ambalo wengi hawajui, walimwaga mboga CAG kamwaga ugali, Mawaziri walitakiwa wamlinde wakati wa hoja ya Katibu Mkuu Kiongozi, wakakaa kimya wakati ana mazabe yao! Sasa na yeye ameamua kufunguka, JK hahahaha! We know
 
- Kwani CAG imekuwepo kwa muda gani? Maaana hii ni mara yangu ya pili kuisikia, mara yangu ya kwanza ilikuwa Dr. Kikwete aliposhika utawala mambo ya mabalozi walioiba, wengine wakafikishwa kwenye Sheria na wengine walilazimishwa ku-retire na kulipa walizoiba.

- Hii ni mara ya pili nawasikia tena CAG, naomba kukuuliza walianza lini hawa CAG? Mbona huko nyuma kwenye awamu zingine hatukuwahi kuwasikia?

William.

hakukua na ubadhirifu na uchafu km ilivo kwake yeye
 
U 4got '@'....... wherever
As a reminder '@' don't use it for larger cities instead use 'in'. @ Mtera....@ ambience @ same kwa Kilango
Then in NYC.... in DSM .... in Dodoma....
Gday..


"Nimefurahishwa na mjadala wa uwazi ulioendelea Bungeni na kwenye kamati ya wabunge wa CCM; nafurahi kwamba azma yangu ya kuzifanya taarifa za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ziwe zinafanyiwa kazi imeanza kutimia" Mhe. Jakaya M. Kikwete
 
kiukweli mh raisi kwahili anahitaji sifa zake,kwani waliowengi wameona hata raisi aliyepita ilikuwa ni ngumu sana kwa wabunge ama hata waandishi wa habari kuweza kuhoji,kwa sasa tumekuwa huru sana,tunaweza sema lolote na kuhoji chochote kile bila hata kuchukuliwa hatua na serikali husika,Hongera Mh Raisi kwa hili.tunaona nchi za wenzetu hali ni ngumu sana
nitawapa mfano mdogo tu

juzi serikali ya uchina ilitaka kumtia hatiana mwanaharakati kipofu kwa nia yake ya kuwaelelimisha wananchi juu ya haki yao ya kuelewa na kufahamu kila jambo serikali yao ilifanyalo.
lakini hapa Tanzania tuna uhuru hata wa kumwandika Raisi vibaya,hebu waulizeni waishio uchina kama wanadhubuti hata kunyanyua mdomo wao

tunakushukuru mh raisi kwa hilo,uwazi tunauona labda tatizo liwe ni utendaji na maamuzi magumu kwa wale waliofanya visivyo ktk nafasi zao
 
Hivi baada ya wabunge kujadili hii report na kutoa mapendekezo yao inabaki kazi ya nani kutekeleza hayo mapendekezo na kama Rais hakuwepo au kama anadharula na nashughuli za serikali zinakuwa zimesimama Willie anasema Rais hakuwepo hivyo ingekuwa vigumu mawazili kusimamishwa anasahau kuwa Urais ni taasisi hata hivyo Rais alishakuwa na hiyo report kwahiyo huo uozo anaufahau,kingine serikali inavyanzo vingi vya habari ikiwemo TISS kwa Rais ambaye yupo smart tulitegemea mambo yote haya anayafahamu hata kabla ya report ya CAG hawa kinaNgeleja na majumba yao tulitegemea wawe walisha hukumiwa jela tangu mwaka jana.Leo JK baada ya kubanwa mbavu anakuja kujisifu kwa kuipa makali ofisi ya CAG badala yakuja kutueleza hatua alizo chukua kweli JK hakuna kitu.
 
Extensionists wana msemo wao usemao...a good technology is that which extends itself....waswahili wakasema kizuri chajiuza.... Sasa haikutakiwa hadi tuhutubiwe ndiyo tujue kuwa sasa mambo haya na yale yamefanyika ilitakiwa sisi wenyewe to feel kweli kunajambo la tofauti limeundwa/fanyika...

Haya maneno yetu mengi hayatabadili ukweli wa kuwa hali wa wananchi wengi ni mbaya na pesa zinazunguka ndani ya circle ya watu wachache huku wengi wakikosa hata mlo mmoja wa siku ebu tukubali haya kwanza ili tuweze kujisaidia wenyewe!
 
"Nimefurahishwa na mjadala wa uwazi ulioendelea Bungeni na kwenye kamati ya wabunge wa CCM; nafurahi kwamba azma yangu ya kuzifanya taarifa za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ziwe zinafanyiwa kazi imeanza kutimia" Mhe. Jakaya M. Kikwete
"Nimesikitishwa na kufurahishwa kwa Mhe Jakaya M. Kikwete bila ya kuchukua hatua muafaka dhidi ya watu aliowachagua na kuwapa dhamana ya kulitumikia taifa, ambao badala yake wanaliibia taifa na kutamba kuwa hawang'oki ng'o. Kwa kuwa kauli au amri ya raisi ni sheria, asifurahishwe tu wakati wananchi tunateseka, bali aamrishe na kusimamia zoezi la kurejesha fedha iliyoliwa na hawa "panya wanaotafuna noti" na baadaye kupewa adhabu wanayostahiki."
 
Ikumbukwe wahisasani ili watoe fedha wanataka uwazi huu! Ila imetusaidia kujua uozo wa serikali ya ccm!

Umenena vyema kabisa sambamba na hilo state imecancel all credit guarantees, hii ripoti ya CAG imewekwa wazi kutokana na matakwa ya nchi wahisani

Kuhusu uwajibikaji kutokana na ripoti hii baada ya mfumo wa vyama vingi ikawepo haja ya usimamizi wa kamati hizi kuu 3 za bunge chini ya wapinzani sort of making a 'third eye' kwahiyo katika miaka 10 ya awamu ya tatu ambapo vuguvugu lilianza hakukuwa na utandawazi wa kina hivi

Vilevile kipindi hiki cha lala salama kwa awamu ya 4 ni muhimu kwa watendaji ambao watagombea nyadhifa muhimu kujipambanua na uchafu, sambamba na hayo hoja ya uwajibikaji ili isijenge sifa kwa upinzani imebidi hayo yatamkwe

Ni mara ngapi tumeona bunge kwa maana ya spika, serikali kwa maana ya waziri mkuu wakitetea jambo ambalo limeibuliwa na upinzani...kisha baadae moto ukizidi, Rais anajitenga na wote wawili km suala la posho ya wabunge

Katika vote of no confidence, JMakamba,Makinda na Mizengo pamoja na Nape hawakuipa uzito...ila rais alipokumbushwa kuwa ni upepo upesi akatoa tamko...
 
Back
Top Bottom