Quote From: The President Dr. Jakaya M. Kikwete!


- Yaaani CAG kumbe ilikuwepo toka miaka ya 70? Sasa iweje wengine tuisikie kwa mara ya kwanza majuzi aliposhika Urais Dr. Jk, I mean unasema huko nyuma hakukuwa na wizi? Then how come haikuwekwa wazi tukaiona wote kama sasa?


William.
 
Hizo report zina tolewa kila mwaka. Kila mwaka kuna madai ya rushwa. Kila mwaka raisi ana ahidi kufanyia kazi report. KILA MWAKA HAMNA ANAE WAJIBISHWA NA REPORT INA PITA KAMA UPEPO!

Mnaojipa matumaini poleni. Hapa ni yale yale tu.
 
William kwa kweli ukiandika vitu kama hivi vinakushushia hadhi kabisa mdogo wangu. Hii ni aibu kwa kabisaaaaa. Muulize baba yako kama kitu umeandika ni sahihi arafu rudi tujadili. Kukaa kwako US kumekufanya usielewe mambo mengi yanayoendelea katika nchi, na ni ajabu umerudi na kasi ya kutaka kutumikia nchi kwenye wadhifa mkubwa bila kujua vitu vidogovidogo, nadhani ilikuwa correct kutokupa ubunge wa EA.
Fuatilia kwanza mambo ya nchi hii kabla hujaenda hata mtera jimboni. Usitutie haya.

 
"kuna watumishi wamegeuza pesa za halmashauri kama za ubani ambazo hazihitaji kuulizwa zimetumikaje" j.k leo kazidi kupaa
 
Hivi inahitaji uchunguzi gani kuwachukulia hatua hawa wezi kaka inahitaji kupewa muda gani?kilakitu kipo wazi inamaana JK haiamini ripoti ya CAG inamaana mapendekezo ya wabunge na kamati zao hayapo sahihi mpaka apewe muda wa kuyapitia tena na tena hapa ndipo yalipo madhaifu ya JK nasisitiza maneno mengi vitendo hakuna.
 
Hizo report zina tolewa kila mwaka. Kila mwaka kuna madai ya rushwa. Kila mwaka raisi ana ahidi kufanyia kazi report. KILA MWAKA HAMNA ANAE WAJIBISHWA NA REPORT INA PITA KAMA UPEPO!

Mnaojipa matumaini poleni. Hapa ni yale yale tu.

Nimegundua kuna watu mnaweka maslahi ya siasa na chama. Akifanya vizuri JK msifie tu.
Kuna kila dalili mipango ya JK ikifanikiwa CCM chati inapanda wakati huohuo CDM chati inashuka
 
Alitakiwa kulifumua baraza lake la Mawaziri kwa kuwa ripoti ya CAG alikuwa nayo kabla haijapelekwa bungeni.....alikuwa anasubiri nini kwa huo uhozo?
 

- Mkuu umesema mengi sana ambayo wala hayahusu! ha! ha! ha! swali langu ni very simple, kwamba Dr. JK anastahili pongezi sana kwa sababu huko nyuma sikuwahi kuisikia hii ripoti ikimtoa kiongozi yoyote kazi, wala kumfikisha mahakamani that is my point, wewe umeeenda mbali sana mpaka kwenye Ubunge wa EAC, mara baba, mara kuishi nje! duh! ! duh! ha1 ha! ha! ha! ha!

William.
 

Narudia tena ni aibu mtu kama wewe kuandika utumbo huu plzzzzzzzzzzzzzzzz
 
Mabosi wa DPP na PCCB wapo kusafisha maswahiba wa JK mafisadi basi. Hosea kazi yake kubwa ni kusema "tunachunguza' au 'hakuna kigogo aliyehusika na ufisadi katika tuhuma za radar'.

Mkuu hapa kuna tatizo la security of tenure. DG - PCCB si cheo cha kikatiba. DPP ni cheo cha kikatiba lakini mwenye mamlaka ya kuteua na kufukuza kwa hivyo vyeo viwili yapo kwa mtu mmoja. Kwa upande mwingine CAG na ofisi yake vipo kikatiba na Rais ana uwezo wa kumteua CAG lakini hawezi.kuamka tu na kumfuta kazi. Hii inasaidia CAG kuwa independent; hii ikisaidiwa na utashi wa kisiasa kama alivyosema Rais basi inamfanya CAG afanye kazi yake without fear or favour. Hawa DG - PCCB na DPP wanakosa uhakika wa kazi zao na pia naona hata kama kuna political will lakini huenda hawaamini kama inatosha. Katiba mpya iitambue PCCB na iwape security of tenure hawa maafisa.
 
JF Premium Member Array


Join Date : 5th February 2008
Posts : 2,186
Rep Power : 971
Likes Received102
Likes Given63


[h=2]
JK alikusudia Kutudanganya, au alidanganywa ili atudanganye?[/h]
Katika hotuba yake kwa watanzania kupitia sherehe za Mei Mosi leo, Rais Kikwete amezungumza mengi kuhusu taarifa za CAG na utekelezaji aw mapendekezo ya CAG. Mojawapo ya mambo aliyosema ni kwamba aliagiza CAG aweke taarifa za ukaguzi wazi ili wananchi wazijadili. Sijawahi kusikia hiyo kauli wala waraka unaoelekeza hivyo. Lakini hilo siyo tatizo.

Enzi za utawala wa BWM, idara na Wizara nyingi za serikali ndo ziliwezeshwa kuanzisha tovuti na kuweka taarifa muhimu za serikali. Ofisi ya CAG nayo ilianzisha tovuti yake kipindi hicho, kama ilivyokuwa nyingine, kwa ufadhili aw serikali za nje.

Wakati huo CAG alikuwa akibandika taarifa zote za ukaguzi. Yaani taarifa kuu kama zinazobandikwa sasa (serikali kuu, serikali za mitaa naMashirika ya umma. Alifanya zaidi, akibandika taarifa za ukaguzi na hesabu za kila Wizara, shirika la umma na kila halmashauri na mkoa. Hakuishia hapo, alitoa nakala zilizosainiwa kwa mtu yeyote ( mtu yeyote) aliyeomba nakala ya ukaguzi ya taasisi yeyote ya umma.

Kuanzia mwaka 2006, CAG hajabandika taarifa za ukaguzi za taasisi moja moja na alikataa kutoa nakala za taarifa hizo pale zilipoombwa. Madai yake yalikuwa " Ni maagizo kutoka juu" Pia ukifuatilia taarifa hizo kwenye taasisi husika zimezuiwa kwa maelezo hayo hayo.

Ni vema ikaeleweka kwamba aina ya taarifa anazobandika CAG tangu 2006, hazimuwezeshi mtu kupata picha nzima ya financial management ya taasisi moja moja na hivyo hutaweza kutoa maoni wala kutatua matatizo yaliyopo. Pengine ndiyo maana, kama alivyosema Rais, hati safi zimeongezeka kipindi cha utawala wake, lakini pia amekiri viwango vya ufujaji wa pesa za umma vimepindukia kila ngazi ya serikali.

Swala la pili, Rais amesema aliagiza mjadala wa wazi aw ripoti za CAG bungeni. Hilo niwaachie mpime wenyewe

Nimeona nitoe maoni yangu tu​





Reply
Reply With Quote
 

Nilichosema ni hiki ulichoandika hapa chini mkuu wangu

-


Bila shaka umenielewa.
Nimesema kamuulize mzee Malecela kama kweli ndio mara ya kwanza ripoti hiyo kuonekana nchi hii.
Yaliyobaki ni ukweli kuhusu maisha yako ya kisiasa nchi hii be careful maana usipokuwa mjanja hata Lucy nde atakushinda.


 
- Yaaani CAG kumbe ilikuwepo toka miaka ya 70? Sasa iweje wengine tuisikie kwa mara ya kwanza majuzi aliposhika Urais Dr. Jk, I mean unasema huko nyuma hakukuwa na wizi? Then how come haikuwekwa wazi tukaiona wote kama sasa?


William.

Hilo suali unapaswa kujiuliza mwenyewe. Hukufanya due diligence kabla ya kukurupuka na kumpongeza Kikwete.
 
Kwa hili la uwazi, Kikwete tutamkumbuka. Maana kabla yake repoti ya CAG huwa inabaki ikulu na haipelekwi kwa wananchi. Kwa hili Bravo Kikwete.
Mkuu, inategemea unaangalia vigezo gani na vingapi.
Je, uwazi wa EPA upo wapi? Unajua Kagoda inamilikiwa na nani na nani amechukua dhamana ya tuhuma dhidi yake?
Je, uwazi wa Jairo, Mwanyika n.k upo wapi?

Wale akina Karamagi, Msabaha n.k wamechuliwa hatua gani baada ya kubainika kufanya madudu?
Je, uwazi wa rada aliyoshiriki kutia saini kama waziri wa mambo ya nje upo wapo?
Je, uwazi wa Kiwira iliyorudishwa serikalini upo wapi?
Je, uwazi wa meremeta, Tangold upo wapi?
Je, uwazi wa kumwajibisha Hosea, Mwanyika na Luhanjo upo wapi
Hayo ni kwa uchahe tu!

Nikukumbushe kuwa taarifa ya CAG imekuwepo mezani kwake tangu achukue nchi kama Rais.
Miaka 5 iliyopita hakuliona hilo na nani amechukuliwa hatua japo kwakuanzia tu!
Ukitafuta nyuzi hapa JF malalamiko kuhusu taarifa ya CAG yanaweza kukupa nyuzi 50 kama si 100. Hivyo hakuna jipya analolisema au kulifanya. Ni kucheza na akili za Watanzania na anafanikiwa kwani anashangiliwa hata pasipostahili.

Kama historia itamhukumu vema Kikwete basi haitaacha kumtaja kama mlezi wa rushwa na ufisadi, vinginevyo historia hiyo ni batili.
 
Kwa hili la uwazi, Kikwete tutamkumbuka. Maana kabla yake repoti ya CAG huwa inabaki ikulu na haipelekwi kwa wananchi. Kwa hili Bravo Kikwete.

Uwazi ni kitu kimoja na utekelezaji wa maamuzi baada ya mijadala ni kitu kingine. Kwangu mm kama hakuna uamuzi wa kubadili mazoea tukaishia kujadili tu ni bora kusiwe na uwazi kabisa maana uwazi huu unawavunja moyo hata wale wachache waliokuwa wanaishi kwa matumaini maana haibadili hali halisi zaidi ya ku-propagate na kuweka wazi njia za wizi wa mali ya umma hata kuwafanya wengine nao wajaribu bahati yao ya kuchuma bila kupanda.
 
Nimegundua kuna watu mnaweka maslahi ya siasa na chama. Akifanya vizuri JK msifie tu.
Kuna kila dalili mipango ya JK ikifanikiwa CCM chati inapanda wakati huohuo CDM chati inashuka

Inawezekana, lakini itachukuwa muda mreeefu sana.
 


Nakupa

  • tu inatoosha
 
Kwahiyo kipindi cha baba yako ndio wizi ulikuwa mkubwa kwasababu hiyo ripoti ya CAG ilikuwa haipelekwi bungeni?
 

Nguruvi3,
Asante. Ndugu yetu Gurudumu ameandika kuwa kuanzia mwaka 2006 serikali ilikataza CAG asitoe ripoti yake hadharani.
Leo nawashangaa watu ambao wanaanza kumsifia mbaya wetu katika harakati za ufisadi eti ghafla amekuwa shujaa wa kupambana na ufisadi serikalini. Ukistaajabu ya Firauni.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…