Vipi ile taarifa ya CAG (Mhilu) ya mwaka 2009 kabla ya hajawa rais. Je, wahusika wa wizara ya ya Mambo ya nje ambayo ni kati ya wizara zilizoongoza kwa kutafuna. alikasirika.
Reflesh Your Memory Box!!
Vipi ile taarifa ya CAG (Mhilu) ya mwaka 2009 kabla ya hajawa rais. Je, wahusika wa wizara ya ya Mambo ya nje ambayo ni kati ya wizara zilizoongoza kwa kutafuna. alikasirika.
Kweli umeishiwa points za kuongeaMkuu ni JK anatisha sana, majambazi na wezi wanamuogopa sana.
Ila naona tatizo anafight alone maana huku kwenye maidara kuna mchwa
Ok Willy,
But unachukuliaje suala la kuomba kwanza ushauri kwenye CC ya chama juu ya kuwashughulikia wabadhirifu serikalini?
Huoni kama inaleta picha kua anawaogopa so anatafuta cha kujitetea kua ni CC ndo imewafukuza na sie yeye??
"Nimefurahishwa na mjadala wa uwazi ulioendelea Bungeni na kwenye kamati ya wabunge wa CCM; nafurahi kwamba azma yangu ya kuzifanya taarifa za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ziwe zinafanyiwa kazi imeanza kutimia" Mhe. Jakaya M. Kikwete
"Nimefurahishwa na mjadala wa uwazi ulioendelea Bungeni na kwenye kamati ya wabunge wa CCM; nafurahi kwamba azma yangu ya kuzifanya taarifa za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ziwe zinafanyiwa kazi imeanza kutimia" Mhe. Jakaya M. Kikwete
Well said,
Kama nimekuelewa vyema tuna matatizo makubwa kwenye sheria zetu, na hapo ndio wafujaji wanapozichakachua kwa
kujua weakness zake.
Well said my brother
Mkuu, ufisadi au uovu wowote haudhibitiwi na mtu bali unadhibitiwa na mfumo wa kitaasisi! Mathalani, Rais unaweza kuwa mkali kweli kweli kwenye masuala ya rushwa, basi mfumo wa kitaasisi sio mzuri! What next, ina maana ukishaondoka madarakani basi kila kitu kitakuwa shaghalabaghala! Inasemekana Nyerere alikuwa anachukia sana ufisadi, lakini alipoondoka tu, ufisadi ukaota mizizi...why? Coz' hakuacha mfumo unaopiga vita ufisadi! Ufisadi ulikuwa unachukiwa na yeye binafsi na sio taasisi...hayo ni mapungufu makubwa! Anachofanya JK, ni kujenga mfumo utakaokuwa against na ufisadi! Mfano mzuri, ni hili la CAG! Ni utawala wa JK ndio uliamua kumu-attach DCI na TAKUKURU ili pale mapungufu as a result of CAG Report yakionekana, basi kama kuna dalili za rushwa basi hapo moja kwa moja TAKUKURU wanaingia na kama kuna dalili za wizi, moja kwa moja DCI anaingia!
Nilishapa kusema hapo kabla.....tatizo lililopo, TAKUKURU, DCI na DPP hawafanyi kazi zao inavyopaswa!! Inasemekana, hawa watu hawana meno, jambo ambalo si kweli hata kidogo! Madai kwamba wanashindwa kufanya kazi kwavile nafasi zao ni za kuteuliwa na Rais, nayo ni madai mfu!!
Brother Willy,
Hapa TZ wezi wa kuku ndio watafungwa tu. Sio wa Kagoda, EPA, RADA, walioingia mikataba inayofilisi hii nchi kama IPTL, DOWANS, RICHMOND nk. Hii ni babaisha ***** tu. Huu ni mwaka wa 7 wa raisi, lakini takwimu zinaonyesha ufisadi ndio unaongezeka. In fact, hapa alikuwa anataka sifa apewe yeye tu.
Huko nyumba wizi ulikuwa unafanyika, lakini uchumi uliimarika. Leo inflation rate ni 24 (tena hiyo ni official ambayo mara nyingi ni ya kuwahadaa wananchi waone mambo yako sawa, deni la taifa linakua kwa kasi ya 36%), na uchumi unakua kwa 6%, yet tunapewa maneno ya kutupa moyo kama haya.
Nione watu kama Chenge, Rostam, wakilala prison ndio nitaona kuwa hizo taasisi zimefanya kazi. Watawatoa Kafara akina Gray Mgonja, Mramba kwa sababu ni marafiki wa Mkapa tu basi. Wala rushwa hawatafanyiwa chochote
- Baba yangu ameniambia mara nyingi sana kwamba huwezi kuongoza bila kukubaliana na wenzako, HOWEVER: hivi ni kweli alienda CC kuomba ushauri au CC ndio waliomuomba on their own kwa niaba ya chama,
- I mean Rais alikuwa nje, amerudi amekuta saga la CAG na mawaziri, eti ni siku hiyo hiyo aliyoshuka anawafukuza mawaziri na kutangaza baraza jipya? Siamini kwamba alienda CC kuomba ushauri, ninaamini kwamba kilikuwa ni kikao cha kawaida kila mwisho wa mwezi, lakini hata kama alienda kule for that bado ni within the rules za chama, au?
William.
- Kwani CAG imekuwepo kwa muda gani? Maaana hii ni mara yangu ya pili kuisikia, mara yangu ya kwanza ilikuwa Dr. Kikwete aliposhika utawala mambo ya mabalozi walioiba, wengine wakafikishwa kwenye Sheria na wengine walilazimishwa ku-retire na kulipa walizoiba.
- Hii ni mara ya pili nawasikia tena CAG, naomba kukuuliza walianza lini hawa CAG? Mbona huko nyuma kwenye awamu zingine hatukuwahi kuwasikia?
William.
"Nimefurahishwa na mjadala wa uwazi ulioendelea Bungeni na kwenye kamati ya wabunge wa CCM; nafurahi kwamba azma yangu ya kuzifanya taarifa za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ziwe zinafanyiwa kazi imeanza kutimia" Mhe. Jakaya M. Kikwete
"Nimefurahishwa na mjadala wa uwazi ulioendelea Bungeni na kwenye kamati ya wabunge wa CCM; nafurahi kwamba azma yangu ya kuzifanya taarifa za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ziwe zinafanyiwa kazi imeanza kutimia" Mhe. Jakaya M. Kikwete
- Nimesema mara nyingi sana kwamba siasa ni kama biashara ya utumbo, huwezi kuifanya huku unaogopa harufu, I mean unajua how long nimekuwepo hapa JF, huwa yanakuja na kupita ila ukweli unasimama mpaka mwisho,
- Kwamba Dr. Jakaya M. Kikwete, huenda ni the best kuliko wote waliopita, I have said that before na ninasema tena now!, unaposema kiongozi mmoja hafai unamlinganisha na wanaofaa, ndio maana ninasema anawazidi wote waliopita! Na mfano mdogo ni hii CAG, mnasema imekuwepo toka Awamu ya kwanza, mna maana toka enzi zile tunanunua Mandege mabovu ya ATC, Gapex, BOT, mnasema CAG walikuwepo?
William.
Lakini jamani nauliza: Hivi JK alianza urais mwaka jana? Ameingia mwaka wa saba sasa, ni miaka mingi wa rais mwenye nia ya kupigana na ufisadi kufanya hivyo na angalau ufanisi ukaonekana kwa sasa. Mwaka 2006 alienda Wizara ya Ardhi na kusema inanuka rushwa na kwamba atahakikisha wafanyakazi pale wanabadilika au sivyo kuna wengi wako nje wanazitaka hizo nafasi zao. Hadi leo wizara hiyo bado inaongoza kwa rushwa na hajarudi pale.
Mwaka huo huo 2006 April aliuambia mkutano wa watendaji wa Halmashauri nchini kwamba hatasita kuzifuta (dissolve) zile ambazo hazitabadilika katika utafunaji wa fedha nk. Hajaifuta hata moja na leo bado anazilalamikia hizo halmashauri.
Mnasema tatizo ni mfumo? Hapana. Tatizo ni kukosa ujasiri wa kuchukuwa maamuzi na kwa JK sababu ya hilo linajulikana, hasa ukizingatia namna alivyoupata urais.
Acheni ku-beat about the bush a.k.a kubwabwaha. Ukweli ni huu.
hivi lengo la kikwete ni kweli kupambana na ubadhirifu huu au ni usanii tu wa kupata ujiko/sifa kwa kuonekana kama kweli anakerwa na ubadhirifu huo...wenye busara walisema cag apewe meno ya kuweza kuwafikisha mahakamani na kuwashtaki hawa wafujaji wa mali ya umma na ripoti yake itumike kama zile ripoti za daktari za sababu ya kifo cha mtu zinavyotumika mahakamani...ushahidi wa cag wala hauhitaji kupelekwa bungeni na kujadiliwa...kungekuwa na nia ya dhati, dpp angekuwa ameshaanza kuaanda mashtaka kwa watuhumiwa wote waliotajwa kwenye ripoti ya cag lakini kama kawaida ya sheria zetu zilizotungwa kuwalinda mafisadi itachukua miaka mpaka hawa jamaa kufikishwa mahakamani na hata wakifikishwa wengi wao kama si wote wataachiwa...kikwete akamuonyeshe mwanaasha hivyo viini macho lakini sisi wenye akili zetu hatudanganyiki...!"Nimefurahishwa na mjadala wa uwazi ulioendelea Bungeni na kwenye kamati ya wabunge wa CCM; nafurahi kwamba azma yangu ya kuzifanya taarifa za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ziwe zinafanyiwa kazi imeanza kutimia" Mhe. Jakaya M. Kikwete