La Quica
JF-Expert Member
- Dec 19, 2017
- 957
- 2,201
Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk 21.07.2024 alijiuzulu ubunge wa kuteuliwa na Rais, akiwa Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Jumapili, 21.07.2024 usiku, Balozi Mahmoud Thabit Kombo akateuliuwa kuwa Waziri katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 55(4) inaeleza “Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa wabunge.”
Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ameteuliwa kuwa WAZIRI kabla ya kuteuliwa kuwa MBUNGE. Kinyume na Uteuzi wa Mawaziri, Sheria ya 1984 Na. 15
Nini kinaanza? Kiapo cha ubunge au kiapo cha uwaziri? Katiba ya JMT haipo kimya. Katiba ya JMT imeweka masharti, mbunge atakula kiapo katika bunge.
Katiba ya JMT Ibara yake ya 68 inasema “Kila Mbunge ataapishwa katika Bunge la JMT kiapo cha uaminifu kabla hajaanza kushiriki shughuli za Bunge”
Kiapo cha utii kwa wabunge kimetajwa katika kanuni za kudumu za bunge 24(1) zilizotungwa chini ya Ibara ya 89(1) ya Katiba ya Tanzania, Sura ya pili.
Kwa maoni yangu, RAIS amevunja KATIBA ya TANZANIA. Katiba ambayo aliapishwa kuhifadhi, kuilinda, kuitetea kwa mujibu wa Sheria iliyowekwa.
Au vinginevyo, tuoneshwe kwamba Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk baada ya kujiuzulu UBUNGE, aliteuliwa kuwa MBUNGE na akateuliwa kuwa WAZIRI.
Kama tunataka MAWAZIRI wasiotokana na UBUNGE, RAIS aanzishe kuanzisha mchakato wa KATIBA MPYA, aachane na wabunge kuwa MAWAZIRI.
I stand to be corrected. Karibu.
Martin Maranja Masese, MMM.