Kuna kauli kaitoa Mwigulu leo walati anahutubia Baraza la Maulidi ilinifikirisha sana nikajiuliza bahati mbaya au?
""Wakati fulani nilikua waziri wa mambo ya ndani,nilipobadilishwa nikaita mkutano jimbani,watu walifikiri nitaenda kutoa kauli ngumu,nilivyofika nikasema sisi watoto wa wafugaji ukijiandaa kwenda kuchunga halafu baba akakuambia usiende wewe leo ni zamu ya huyu haukasiriki bali unavua viatu na kufanya kazi nyingine uliyopangiwa,hivi ndivyo ilivyo haya kwenye uongozi".
Hapa lipo jambo sio bure.