econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 22,138
- 32,715
Niwe mkweli, public reception ya Mpina haijawa kubwa kivile kama ilivyotegemewa. Hii ni tofauti na public reception waliyopata Maalim Seif alipoanzisha KAMAHURU na baadaye CUF, Mrema kuhamia NCCR na Lowassa kuhamia CHADEMA. Hawa walipohama walihama na wanachama wa CCM na viongozi wao na jamii iliwapokea kwa kishindo.
Nikija upande wa Mpina naona ni kama yeye yupo tofauti. Kwanza kahamia upinzani pekee yake na Hana kundi la wanachama au viongozi wa CCM aliyo hamia nao upinzani na jamii pia haijampokea Mpina kama mpinzani halisi wa kuiondoa CCM madarakani.
Sababu Kuu tatu zinazo pelekea Mpina kukosa huge Public Reception ni kama ifutavyo:
1. Sababu ya kwanza, Ni kwamba wananchi hawana Imani Tena na wagombea urais wa kutoka CCM kuja upinzani. Historia inaonesha wagombea wengi wa aina hiyo, walirudi CCM baada ya uchaguzi mkuu au walibaki upinzani na kuwa vibaraka wa CCM. Lowassa na Membe walirudi CCM ila Mrema alibaki upinzani kama kibaraka wa CCM. Hivyo basi, wananchi wengi wanaamini Mpina atarudi CCM baada ya uchaguzi mkuu.
2. Sababu ya pili, Kuna vuguvugu la mabadiliko ya Sheria na kanuni za uchaguzi. Hili limefunika ujio wa Mpina kwenda upinzani. Kwamba wengi wanaona Mpina anatumika kupambana na kauli mbili ya No Reform No Election. Kwamba Mpina ni kama chambo ya kuhalalisha ufanyikaji wa uchaguzi mkuu mwaka huu na kuonesha kwamba kasoro zilizopo ni ndogo Sana kuweza kuwafavour CCM dhidi ya upinzani.
3. Timing ya Mpina kuja upinzani. Logic ni kwamba Mpina hakuwa na ambition ya kuwa Rais akiwa CCM Wala kujitangaza, yeye ambition yake ilikuwa ndio ubunge ghafla kaja upinzani anataka urais.
Wengi wanadhani Mpina kaja upinzani kimaslahi. Na kwamba kaja upinzani kwa sababu ya kukatwa kwenye ubunge huko CCM. Kwa kujua kwamba hawezi kuwa Mbunge maana system ya CCM na serikali yake imemkalia kidete ndio kaamua Kuja upinzani. Wengi wanadhani ingekuwa Bora Mpina kuhamia upinzani kipindi ambacho ni Mbunge na sio kipindi ambacho kakatwa kugombea ubunge ndani ya CCM. Na alistahili Kuna upinzani akiwa anafahamika na umma kuwa anataka kugombea urais tangu akiwa ndani ya CCM.
Kwa kumaliza napenda kusema ya kwamba nguvu ya Mpina kwenye ubunge ni kubwa Sana kuliko nguvu kwenye urais. Hivyo basi Mpina angeendelea kugombea ubunge pale Kisesa kwa kupitia upinzani angepita bila shida ila kwenye urais Kuna mambo mengi yatamkwamisha maana Kwa macho ya wengi ni mwanaccm sio mpinzani.