Public plea, Kitila, Zitto, Mnyika na wapiganaji wengine... Dont quit

Wakuu, nalazimika kuomba public plea kwa wapiganaji kadhaa ambao walikua chachu ya habari na mijadala hasa yenye kuelimisha members na non members wengine humu jamvini

Bado tunawahitaji, hasas kipindi hiki cha mpito kuelekea uchaguzi, kumbukeni kwamba kuna vijana na watu wengine wenye interest kubwa na nchi hii, and believe me, hakuna avenue nyingine ya kupata as neutral as possible news zaidi ya JF, kwingine kote kuna bias tupu!!

Kama mzalendo na mepnda nchi, na mchukia unyonyaji na ufisadi, nawaomba rudini kundini muungane na waliopo akina MMM, FMES, Rev. nk. kuweka nchi panapostahili

Najua baadhi yenu mmepitia jeshi na baadhi yenu mmesoma sana habari za vita, kugeuka nyuma kunadeserve risasi ya mgongo, please dont do that

Lets strengthen mapinduzi ya kweli ya kiuchumi, kisiasa na kiutamamduni pamoja

DN

Mbona huwaiti wa chama cha majungu!
 
Mkamap, una uhakika gani kama ma invisible na mamoderator wamebashiri bashiri kuwa wewe unatumia ID zaidi ya moja? Unajiunga kwenye bandwagon ya kubashiri bashiri.

Mainvisible na mamoderator ni high tech, je hiyo suggestion yako ya PHP script na mambo ya kulocate IP address hawajui?

Zaidi, kama walikuandikia PM mkadiscuss hayo, nadhani na wewe ingekuwa vizuri ungefanya vivyo hivyo.

Samahani kama nimekukwaza.

Naomba nikuulize
Kati ya ma high tech ma-invisible na mimi mwenyewe ni nani mwenye uhakika 100% kwamba mimi nina ID moja??

Nakwambia hivi wameshanitumia PM kunionya kutumia ID zaidi ya moja, wakati hata leo Mungu akishuka sijawahi tumia ID zaidi ya moja humu JF.Sasa niambie anayebashiri ni nani.?

Na hata hivyo nimewapa ushauri ma -invisible lakini pia ushauri wanaweza kuupuzia kama ni wakipuuzi ama haujengi.

Ma high tech kama ulivyowaita waongeze ka script kadogo tu ktk forum ili mtu aki-login tu aonekane yupo nchi gani na public IP address yake, hiyo nafikiri itakuwa angalau ni high tech kuweza kumsort out mtu.

Japo kunauwezekano zaidi ya mtu mmoja kutumia IP hiyohiyo lakini itakuwa afadhali inatoa picha kamili.Ni nani anayebadilika badilika.
Na hizo information ziwe kila mmoja anaziona ili hukumu ikitoka agalabu kila mmoja anakuwa amejiridhisha.Nafikiri huo ndo mfumo huru.
 
Wana majukumu mengine kibao ya ndani ya Chama hivyo huwa wanafanya kazi ila Mnyika huwa anakuja hapa na kutupa habari
 
Kweli mkuu Invisible, I think its high time strict rules ziwekwe na kuwa adhered na mods ili kuhakikisha wakati wote jukwaa linatawaliwa na hewa safi.
 
Bahati mbaya kuchafuana via JF hakutavumiliwa; ni kwakuwa tuko in middle of something, tunashindwa ku-deal na wachafuzi wenye dhamira ya kuudhi watu badala ya kujadili hoja; once we're done (April 2, 2010) tutakuwa wachungu sana kwa wachafuzi wote, hatutamwangalia mtu usoni.

Meanwhile, ni vema watanzania hasa wana JF tukawa na staha wakati wa kuwasilisha hoja, hakuna kitu kinakera kama kuja na allegations dhidi ya mwanachama bila kufanya utafiti wenye kuwa na uhakika pasi na waa lolote.

Madai dhidi ya wanachama wenzetu na watanzania wenzetu zikiambatana na uthibitisho wa allegations zinasimama zenyewe na kumwongezea heshima mwenye kuzileta, lugha za kejeli, name calling n.k haviruhusiwi na havitavumiliwa kamwe ndani ya JF.

USHAURI: Ukiona ambapo kuna mwanachama amefanya kitu na hujaridhishwa nacho (matusi, kejeli, uchafu wa aina yoyote n.k) tafadhali usihangaike kujibizana nae au usihangaike kuandika alipoandika; bonyeza sehemu unayoona ina alama hii:

report.gif

Kisha sisi tutachukua hatua haraka sana, aidha unaweza kutufahamisha via support@jamiiforums.com nasi tukarekebisha haraka.

Reporting ya kosa lolote ndani ya JF inakuongezea credits kwenye profile yako!

Mkuu Invisible,

Tatizo ni kwamba mnashughulikia dagaa na kuacha kambare wanachafua wengine bila adhabu yoyote. Ni mambo yale yale kama siasa za TZ ambapo mdogo huadhibiwa ipasavyo lakini wakubwa wana get away with murder.

Kuna watu mpaka wanaweka maneno ya kukashifu wana JF wenzao kwenye signatures zao na hakuna kinachochukuliwa sasa hapo kweli mtasema mko serious?

Kuna watu hapa JF wanatoa matusi ya ajabu tena mpaka ya nguoni na sijaona wakifungiwa lakini dagaa kibao wanafungiwa kila siku.

JF lazima iwe mahali pa kuibua kila aina ya scandals za wahusika bila kuogopa mhusika ni nani, lakini pia lazima wanatoa hizo kashfa wawe na burden ya aina fulani ya kutoa ushahidi. Sio mtu anaimba tu kila siku insible mwizi huku hujawahi hata kuiba kuku wa mtu. Tukifanya hivyo tutakuwa hatuwatendei haki wale ambao wanajulikana kwa majina yao.

Ninaunga mkono hayo maelezo hapo juu...........asanteni sana Wakuu
 
Kwa hili kuna ukweli kiasi kikubwa na nadhani invisible na wenzako mmeweka either ni trust kwa baadhi ya watu au sijui ni nini kwani there are few abusers ambao wameachwa kuwa too much huru!!

Lets scrutinize each other... but at the same time, ombi langu kwa makamanda liko palepale
 
Pamoja ya yote hayo aliyosema invisible na members. Ni busara kuwe na strict rules ambazo haziangalii makunyazi. Mimi ni shahidi kuna member hapa huwa anajifanya mtemi sana na sijui ameshafungiwa mara ngapi. Si kazi yangu kutaja ID hapa ila basi kuanzia leo nikikutana na post yake amemjibu member mwingine kusikostahili hata kama si mimi binafsi nitabonyeza kitufe. Sasa basi nitapenda mods kushughulikia ipasavyo kwa members wote kuanzia wale wa 2006 and before if any!!! Nafikiri wale members wa zamani wanafahamiana kwa kiasi, hata kama si wote!!! Na kufahamiana huko basi kusilegeze sheria na taratibu za forum. Let us maintain some very important core values, like fairness, transparent and respect!

Na kwa wale ambao mnakwazika na majibu ya baadhi ya member basi usijibu kwa jazba, ni vema kutojibu mhusika kwani ukijibishana na asiye na busara basi nawe utaonekana huna busara na kwa mantiki hiyo bonyeza kale ka kitufe cha report post na weka ujumbe wako kwa mods. "Let us save our country, share your constructive ideas/comments and work out the best solutions...."
 
Wana majukumu mengine kibao ya ndani ya Chama hivyo huwa wanafanya kazi ila Mnyika huwa anakuja hapa na kutupa habari

Na Dr. Kitila anaonekana sana tu hapa JF..................na alishatuambia kuwa uchangiaji wake utakuwa mara chache.................
 
Kwa matusi ya hapa JF siku hizi, wale wanaojulikana kwa majina yao wanakuwa target ya baadhi ya watu bila sababu za msingi.

Zamani ilikuwa mjadala unaweza kuchukua hata wiki na kusiwe na matusi lakini siku hizi kumekuja wajanja wanaona matusi na personal attacks ndio agenda kubwa.

lazima tutegemee watu wengi watapotea na wale ambao ni wapenzi wa JF basi wanaishia kusoma kama guests na hata wakitaka kuchangia mada wanajiuliza mara mbili mbili.

Msiogope matusi, wanamapinduzi wakweli si waoga, je ingekuwa ni makabiliano ya risasi si huyo kabwe angebakia uko ujerumani akatuacha tukiuana huku, arudi atueleze JF members ana jipya lipi?
 
Na Dr. Kitila anaonekana sana tu hapa JF..................na alishatuambia kuwa uchangiaji wake utakuwa mara chache.................
na hilo ndilo ombi langu... michango yao ni muhimu sana
 
Mimi nipo na sijakwazika kwa kiwango cha kukimbia. Kidogo kuna kubanwa na kukosa muda wa kupita hapa. Nitajihidi sana nichangie, ukizingatia huu ni mwaka wa vituko, mbwembwe na madoido mengi!

Cheers!
 
Pamoja ya yote hayo aliyosema invisible na members. Ni busara kuwe na strict rules ambazo haziangalii makunyazi. Mimi ni shahidi kuna member hapa huwa anajifanya mtemi sana na sijui ameshafungiwa mara ngapi. Si kazi yangu kutaja ID hapa ila basi kuanzia leo nikikutana na post yake amemjibu member mwingine kusikostahili hata kama si mimi binafsi nitabonyeza kitufe. Sasa basi nitapenda mods kushughulikia ipasavyo kwa members wote kuanzia wale wa 2006 and before if any!!! Nafikiri wale members wa zamani wanafahamiana kwa kiasi, hata kama si wote!!! Na kufahamiana huko basi kusilegeze sheria na taratibu za forum. Let us maintain some very important core values, like fairness, transparent and respect!

Na kwa wale ambao mnakwazika na majibu ya baadhi ya member basi usijibu kwa jazba, ni vema kutojibu mhusika kwani ukijibishana na asiye na busara basi nawe utaonekana huna busara na kwa mantiki hiyo bonyeza kale ka kitufe cha report post na weka ujumbe wako kwa mods. "Let us save our country, share your constructive ideas/comments and work out the best solutions...."

Nina imani haya yote yatakuwa addressed by April 2 mbili... Na ni muhimu iwepo namna ya kutupa updates za reporting kwani nimeshawahi kureport posts, sasa sijui ni wangapi wanareport nini kwa siku!!!

Labda tuwe na hiyo feedback ambayo itatusaidia kujua ni abuser gani anaachwa, na hata level ya punishment inaweza kuendana na number of reports received for the concerned offense!!
 
Bado nasisitiza kwamba wapigananji mrudi tuendelee na mapambano, hiki ni kipindi kigumu sana kwetu wanaJF na pia taifa kwa ujumla

busara na hoja na majadiliano ni muhimu sana kwa nchi

naona list ya walioondoka imekua kubwa sana hadi akina Josh Michael, GT, FMES, Malafyale, Mtanzania, Zitto, Lunyungu nk wote sasa kimya

Hata farida hapatikani

GUys, sisi ni members na pia ni wapiganaji kwa namna yetu

TUSIWE SAWA NA MABAHARIA WA MV MAPENZI
 
Nafikiri waheshimiwa hawa hawawezi kukimbia ni watu ambao wanatakiwa kuwa na ngozi ngumu(Sita, 2009).

Je wakiwakimbia watu wa mtandaonni ambao wengine hawaonekani itakuwaje wakiwa kwenye majengo ya pale Dodoma ambako unamsema mtu huku akikuchungulia?
 
Hivi kweli FMES na Lunyungu wamepotelea wapi siku hizi? najua FMES akiibuka ataibuka na mambo mazito, pengine akatupa siri ya Tendwa kuwa na kigugumizi kuisajili CCJ!
 
Back
Top Bottom