Wapendwa wana JF mwenzenu nimekwepa majaribu mara kadhaa kutoka kwa secretary wangu hua ananitega mara kwa mara, majuzi nilikuwa Iringa safari ya kikazi akanipigia simu saa tano za usiku baada ya kunisalimia akaniuliza vipi habari za Iringa?
Nilimjibu huku salama ila baridi ni kali sana ndipo alipo niambia kwanini hukuniambia tusafiri wote? nilibaki kimya huku nikisubiri aniambie tatizo la kunipigia simu usiku ule , akaishia kusema haya nilitaka kukusalimia tu ila usikose kuniletea zawadi.
Nilipo rudi akawa ananiangalia kwa macho ya kulembua kila anapo ingia ofisini. Kuna siku nimempa kazi ya kuchapa barua alipo maliza akaniletea laptop ili nii proof read ile barua akasimama nyuma ya kiti changu na kunigusisha nyonyo zake kwenye bega la kulia ,nilijikausha kama sioni kitu pamoja na kuwa mwili wangu ulipatwa na mfadhaiko.
Ilipo fika muda wa chai nilipo maliza kunywa chai nikanawa mikono akanifuta mikono kwa kutumia kitaulo kidogo wakati sio utaratibu ulio zoeleka.
Jana wakati ninatoka ofisini akasimama mlangoni kama vile anataka kunizuia nisitoke ,mimi nikasimama kusubiri anipishe akaniangalia usoni kwa sekunde kadhaa na baadaye akatoa bonge la tabasamu, nikaendelea kumuangalia akakimbia huku anacheka. jamani hii kama si mitego ni nini?
Dawa yake ni nini?