RUGE MUTAHABA (R.I.P) alisema kwamba;
"Tafuta nafasi, ukiipata onyesha uwezo wako, talanta yako, bidii yako. Utajiri na mafanikio yatakuja baada ya hapo".
Sijajua wewe upo mkoa gani, lakini hapa mjini Daslam, kuna watu walianza na gereji za spana mkononi, sasa hivi wana "brand" zao za gereji. Kunq ankoli mmoja wa Mwinyi, alitoka Polisi Ufundi Kurasini, akaanzisha gereji yake hapa mjini, ukiongelea mafundi wazuri wa Land Rover discovery kuanzia matoleo ya chini yale, mpaka hizi mpya. Watakwambia nenda gereji kwa Mwinyi.
Kuhusu utajiri: Kwa macho yangu naona anao. Importers na users wengi wa magari hayo wanamjua huyo bwana. Anashughulika na gari hizo tuu, amejibrand hivyo, kuanzia discovery matoleo yote, Range Rover matoleo yote, zipo chungu nzima gereji kwake.