Kitila, MMM bado yupo, labda aliweke wazi mwenyewe. Nilivyomwelewa mimi, ni kwamba anasema kuwaondoa CCM madarakani ndiyo focus ya CDM, na hilo ni kosa.
MMK fikra zake, maono,na imani yake huwa anafikiri kabisa kuwa ndio fikra za CDM,ndio malengo ya CDM ndio imani ya CDM.Wana CDM wanafanya wafanyayo wakiwa na fikra ,mipango tofauti n amikubwa zaidi.Its kinder fun.
Nadhani hapo namwelewa na pia nakubaliana naye.
Siku zote napata picha kwamba CDM hawana tatizo na sera za CCM , bali wana tatizo na watawala wa CCM. Kwa kiasi fulani hili wameliweka wazi, japo hawajakili kwa kiwango kinachotakiwa. Kama tatizo ni watawala wa CCM basi CDM watuambie hivyo ili wasije wakaingia madarakani kwa gia ya watawala wabovu wa CCM, na kisha baada ya kuwaondoa watawala wakataka kuondoa sera za CCM ambazo huenda ni nzuri tu.
Au je, CDM wanataka kuwaondoa CCM kwa sababu wanaona sera za serikali ya CCM ni mbaya? Kama ndivyo watuambie pia, ni zipi kati ya hizi sera wanaziona mbaya, na wanataka kuzibadili na kuweka sera za namna gani mbadala? Kwa mfano, japo muungano si suala la sera bali ni la kikatiba, CDM hata siku moja haijawa wazi kabisa kuhusu suala la muungano. Wanamung'unya maneno kuhusu msimamo wao thabiti juu ya muungano. Sera ya madini, CDM wamekazania ufisadi wa mikataba, na hawajasema lolote juu ya sera iliyopo. Hivyo hivyo na suala la nishati, na hata mfumo wa utawala wa nchi. Kwa nini CDM wanaogopa kusema kwa mfano, wakichukua nchi wataondoa nafasi za ukuu wa mkoa na wilaya au kuziacha hizo nafasi na kutoa sababu zao za msingi? Je ni kwa kiasi gani wanatumia mjadala wa Katiba wa sasa kuwaonyesha wananchi wanasimamia mambo gani?
Kwa mtu anayefuatia mikutano ya CDM, taarifa kwa umma, bungeni na kwinginepo atakuwa ameona/amesikia/amesoma wakitoa melezo yao kuhusu mgawanyo wa maeneo, baraza la mawaziri, madini na nishati, muungano,nafasi ya wakuu wa wilaya na mikoa, afya, elimu na kila kitu kurudia rudia tuu na kujichanganya na nia ovu tuu ndio inafanya watu kukomaa na vitu baseless.nani hajui kuwa CDM wanataka serikali 3, majimbo na si huu usanii kama wa dar
Pamoja na yote, nakiri kwamba CDM wanaelewa sana kwamba Tanzania ina wapiga kura (king makers) wa aina gani. Ni kweli wengi wa wapiga kura wa Tanzania wako katika ushabiki zaidi ya uelewevu wa sera na mwonekano wa mtu - na hii ndio sababu JK alishinda kwa kishindo 2005.
hijalishi hao watu ni wa aina gani chama bora kinapaswa kubalance yale mambo ya msingi ambayo yangeulizwa na watu wenye akili ili kuwasaidia hata wale watu wanaodhani pombe ya siku moja inatosha,huku wakijitahidi weka vionjo vichache kwa wale wafuatao shsbiki ili kuweza secure place ili kiwafanyie zaidi ya walichoomba wapiga kura.Tusipokuwa makini na hawa wasomi waliopotoka huku wakiwa na influence ktk kundi la waandishi makanjanja.Basi wata jenga demands za kijinga kwa wapiga kura na baadaye kuwa ndio criteria zao huku wakiacha mambo ya msingi kwa mataifa ktk kutatua matatizo ya ndani na pia kutuweka vyema ktk ushindani na usitawi mbele ya mataifa.
Unfortunately, namwona pia MMM kuwa guilty wa ushabiki huu, kwani tupo tulioona tangu mwanzoni kwamba JK alikuwa kiongozi dhaifu kutokana na utendaji wake wa nyuma, na tulisikitika kuona ushabiki uliokuwa nyuma ya jina lake, na kujua kwamba watu watakuja kuujutia uamuzi wao wa kumuweka JK madarakani kwa sababu tu ya ushabiki waliokuwa nao juu yake (kuna posti niliweka kule Wanajamii juu ya hili). Nimeshangaa sana kuona ilimchukua MMM muda mrefu vile kugundua udhaifu wa JK kama kiongozi wa nchi. Sasa ikiwa mtu msomi kama MMM alikuwa kipofu wa hili, vipi yule mpiga kura wa mtaani!
teh teheeeeeeeeeeeeeeeeeh......niliwahi mwambia ajithaminishe kuanzia mwanzo wa thread hadi kwenye session tuliyokuwepo.Hakutaka jibu vyema badala yake akaweka kiburi ili kulinda "self esteem".Eti hakuwa ameitumia kujipima...nashukuru wengine wamempima.mimi nilimwambia naongea vitu ambavyo havi-work huku CDM mambo yao yakiwaendea vizuri.
Hivyo basi, kabla ya kuwasema sana CDM kwamba hawanadi sera katika mihadhara yao, ni lazima tujiulize swali la msingi kama tuna wapiga kura nchini ambao wanaelewa umuhimu wa sera katika mfumo wa vyama vingi vya siasa. Leo hii CDM wakianza kuhubiri sera, wapiga kura watawaelewa? Sikatai kwamba wapo Watanzania wapiga kura wachache wanaoelewa maana ya sera, na hili ni jambo ambalo CDM inapaswa kukumbuka na kutumia forum zinazokubalika kuliongelea. Ukweli ni kwamba kwa namna moja au nyingine CDM wamekuwa wakikwepa kukutana na kujadili issues na wasomi, watu wenye mpanuko wa kimawazo zaidi ya kuongea juu ya ufisadi na kuvua gamba!
Sidhani kama CDM wamewakwepa, ila nao wasomi wamekuwa wanakaa mkao wa kijanja sana.Kwa vile wamekuwa na theories kama za bar na mara nyingi mwenendo wa CDM na mafanikio yao yanawafanya wawe busy kuzirekebisha.CDM hawana haja ya kuhofia wasomi kwani bench lao linao wa kutosha, na hata wale wenye elimu ya kati wanakimbiza mbaya,wanameza vitu vigumu.Mnyika alisema Kikwete ni "..dhaifu...",Bila hofu wakati wasomi walikuwa wakipoteza muda kutafuta maelezo kuwa JK hana shida ila watendaji wake sijui na mafisadi.Waliokuwa na guts kukubalina na kusupport ni wachache,kisha wadandiaji walipoona kuwa upepo unaelekea upande wa Mnyika ndipo wakaingia.
MMK mwenyewe kakiri kuwa kaingia CDM alipoiona kuwa ine potential(something )ya kuchukua utawala wa nchi.Bongo hatuna wasomi wa kuweza toa wazo jipya(wa kutosha,kama wapo) kwani wengi wamejiwekea ipaka ya kifikra na wanaogopa igusa.Na kwa mahati mbaya wakigusa hukusa vibaya na kuwa ya kijinga.We need wasomi wenye tenacity ya CDM ,wana ujasiri na research kama hawa CDM ."The badgers".Hawamumunyi maneno hizi kauli ambazo si clear za MMK,mchambuzi, mkandara and the sort ni dhambi,ni za kinafiki na za kufuata upepo.Tazama wakibanwa wanavyokwepesha kaulizao,wakiambiwa wathibitishe wanaenda off topics mpaka waombwe sana thibitisha, mara nyingine wanadeka, wanatoa reference za mbali sana au zisizi clear.Sipendi vuguvugu kwani si reliable.Si muda mrefu MMK atakuja na mengine kuhusu CDM kama alivyokuja kwa JK kwa CCM.