Hebu tupanue mjadala kidogo: Je, ni muhimu kuiondoa CCM madarakani na maovu yake sasa hivi au muhimu kwanza ni kuiondoa CCM madarakani na mengine yatafuata baadaye? Kama lengo ni kuiondoa CCM madarakani na sio lazima kuondoa na maovu yake mara moja, then MMM is right. Otherwise, he is missing the point.
Mimi msimamo wangu siku zote ni wazi kabisa: cha muhimu kwa sasa hivi ni kuiondoa CCM madarakani.
Kitila, MMM bado yupo, labda aliweke wazi mwenyewe. Nilivyomwelewa mimi, ni kwamba anasema kuwaondoa CCM madarakani ndiyo focus ya CDM, na hilo ni kosa.
Nadhani hapo namwelewa na pia nakubaliana naye.
Siku zote napata picha kwamba CDM hawana tatizo na sera za CCM , bali wana tatizo na watawala wa CCM. Kwa kiasi fulani hili wameliweka wazi, japo hawajakili kwa kiwango kinachotakiwa. Kama tatizo ni watawala wa CCM basi CDM watuambie hivyo ili wasije wakaingia madarakani kwa gia ya watawala wabovu wa CCM, na kisha baada ya kuwaondoa watawala wakataka kuondoa sera za CCM ambazo huenda ni nzuri tu.
Au je, CDM wanataka kuwaondoa CCM kwa sababu wanaona sera za serikali ya CCM ni mbaya? Kama ndivyo watuambie pia, ni zipi kati ya hizi sera wanaziona mbaya, na wanataka kuzibadili na kuweka sera za namna gani mbadala? Kwa mfano, japo muungano si suala la sera bali ni la kikatiba, CDM hata siku moja haijawa wazi kabisa kuhusu suala la muungano. Wanamung'unya maneno kuhusu msimamo wao thabiti juu ya muungano. Sera ya madini, CDM wamekazania ufisadi wa mikataba, na hawajasema lolote juu ya sera iliyopo. Hivyo hivyo na suala la nishati, na hata mfumo wa utawala wa nchi. Kwa nini CDM wanaogopa kusema kwa mfano, wakichukua nchi wataondoa nafasi za ukuu wa mkoa na wilaya au kuziacha hizo nafasi na kutoa sababu zao za msingi? Je ni kwa kiasi gani wanatumia mjadala wa Katiba wa sasa kuwaonyesha wananchi wanasimamia mambo gani?
Pamoja na yote, nakiri kwamba CDM wanaelewa sana kwamba Tanzania ina wapiga kura (king makers) wa aina gani. Ni kweli wengi wa wapiga kura wa Tanzania wako katika ushabiki zaidi ya uelewevu wa sera na mwonekano wa mtu - na hii ndio sababu JK alishinda kwa kishindo 2005.
Unfortunately, namwona pia MMM kuwa guilty wa ushabiki huu, kwani tupo tulioona tangu mwanzoni kwamba JK alikuwa kiongozi dhaifu kutokana na utendaji wake wa nyuma, na tulisikitika kuona ushabiki uliokuwa nyuma ya jina lake, na kujua kwamba watu watakuja kuujutia uamuzi wao wa kumuweka JK madarakani kwa sababu tu ya ushabiki waliokuwa nao juu yake (kuna posti niliweka kule Wanajamii juu ya hili). Nimeshangaa sana kuona ilimchukua MMM muda mrefu vile kugundua udhaifu wa JK kama kiongozi wa nchi. Sasa ikiwa mtu msomi kama MMM alikuwa kipofu wa hili, vipi yule mpiga kura wa mtaani!
Hivyo basi, kabla ya kuwasema sana CDM kwamba hawanadi sera katika mihadhara yao, ni lazima tujiulize swali la msingi kama tuna wapiga kura nchini ambao wanaelewa umuhimu wa sera katika mfumo wa vyama vingi vya siasa. Leo hii CDM wakianza kuhubiri sera, wapiga kura watawaelewa? Sikatai kwamba wapo Watanzania wapiga kura wachache wanaoelewa maana ya sera, na hili ni jambo ambalo CDM inapaswa kukumbuka na kutumia forum zinazokubalika kuliongelea. Ukweli ni kwamba kwa namna moja au nyingine CDM wamekuwa wakikwepa kukutana na kujadili issues na wasomi, watu wenye mpanuko wa kimawazo zaidi ya kuongea juu ya ufisadi na kuvua gamba!