Mkuu ufisadi hupo na ni sababu tosha ya kusema CCM iondoke kama reasoning ni hasira.
Lakini lazima tujiulize je ni nini hasa chanzo chake ukitoa viongozi wa juu ambao utumia mbinu za tender na kuiba kwa maandishi na kugawa rasilimali za taifa. Vile vile rushwa na wizi ni common practice in Tanzania kwenye nchi ambayo sasa inabajeti za matririon kwenye wizara nyingi lazima tujiulize hawa je watadhibitiwa vipi (maana sidhani wote wana hizini ya JK) kwenye kuiba (kama umefuatilia ripoti ya mwisho ya CAG, hela nyingi zinapotea mawizarani pia)
Surely a political party has to address the means to curb those evil deeds ambazo zina contribution kubwa kwenye kuleta poor services. Sasa CDM wanayazungumzia vipi au wana mbinu gani, au wataweka mbinu zipi na zitafanya kazi vipi.
Huo no mfano lakini kuna nyanza nyingi sana tunaweza ziweka na kuzihoji hili kufikia the potential ya taifa letu. So far the motto ni ufisadi na abusive of powers za CCM.
Je wakipewa hiyo dola how are they going to change things, methods and the policing of the resources including money taxes and their spending priorities, do they even know the loopholes that allows tax evasion in the country and how much do we loose on this evasion.
Maswali ni mengi and they need to be adressed kuliko kuwasifia tu kupitia hasira zetu, ingawa lazima wasifiwe kwa kazi waliofikia so far.
Siyo kweli kwamba wanasifiwa tu kupitia hasira zetu.Kiukweli wanakuwa critisized hadi nikaona kuwa ni ubinafsi na uonevu.
Chama kilichokaa madarakani kwa miaka 50,kisichowajali wananchi,kuendelea kukipa a benefit of doubt is also doubtfull to some of us!Utatufanya tujiulize kama una manufaa gani na unyama huo na ufisadi.
Mkuu chadema ni chama ambacho bado kinajengwa,na kitazidi kukomaa kama kitaungwa mkono na kuchukuwa madaraka ya nchi.
Sasa kina Mwanakijiji wanataka kikomae kikiwa bado ni chama cha upinzani,ukimwuliza akupe mfano halisi wa vyama vya aina hiyo,i doubt kama ataweza kufanya hivyo.
Kwenye kuhusu maoni ya katiba,kulikuja issue moja ya mwanajeshi aliyesema kuwa mafisadi watakaopatikana na hatia,basi wapigwe risasi!Halafu kuna watu humu wakadai eti mwanajeshi yule ni chadema!
Badala ya kukubaliana kwamba ni kweli kama tunataka kuutokomeza ufisadi,basi adhabu zake(ufisadi), ziwe kali kama tunavyosikia kuhusu kule uchina,tunarudi kwenye kunyoosheana vidole kuhusiana na itikadi ya vyama,kiasi cha kwamba kumekuwa kama ushabiki wa mpira wa miguu,kwa maana kwamba ukiwa ccm,basi kuupinga ufisadi,ni sawa na kukipinga chama chako,na watu wanaridhika na hayo,really?I don't think thats the way to go,nina imani kabisa kwamba kutokana na hapa tulipofikia(ushabiki),basi hatua ya muhimu kabla ya chochote kile ni kuiondoa ccm madarakani,wewe unadhani kwanini huwa kuna mapinduzi?
Tumeona jinsi wabunge wa upinzani walivyo na umakini hata bungeni licha ya upendeleo wa spika.Lakini bado wanazisimamia hoja zao kuliko hata hao ccm walioko madarakani more than 50 years!Why not give them a chance?
Nchi hii nani kasema imehodhiwa na baadhi ya watu?Ama nani kasema watu flani ndo wana haki ya kutawala wanavyotaka bila kuwajibishwa?
Halafu mtu huyo huyo anayesema ccm wapewe nafasi kwasababu chadema hawajajipanga ndo atakuja tena kuulalamikia uozo unaoendelea pale utakapojulikana?
Kiukweli nchi haiko kwenye right track na haijawahi kuwa kwenye right track,hilo tu linatosha kuwaondoa madarakani watawala right away whenever possible!
Kama unaamini(kama ninavyoamini), kwamba kuiondoa ccm itakuwa sawa na uhuru wetu wa pili,then jiulize kuhusu chama cha TANU,je kingewekewa vipimo kama hivi anavyoviweka Mwanakijiji kingeingia madarakani?
Kama unaamini pia kwamba revolution can be justifiable kuuondoa ufisadi,je unataka uambiwe baada ya mapinduzi nini kitafanyika?Is that a fair question?
Certainly that is impossible.Kitu kimoja cha msingi kabisa kinachowaunganisha wananchi ni kuutokomeza umasikini,ujinga na maradhi,na hayo hayatowezekana pasipo kuuondoa ufisadi kwanza.Hilo liko wazi kabisa wala huitaji kuwa a rocket scientist kuliona.
Hayo anayoyazungumzia Mwanakijiji siyo mambo yenye kustahili kukinyima chama cha chadema nafasi ya kuwatumikia wananchi.
Kwani shida ikwapi kama wasipo deliver si tunawaondoa?Sasa kusema tuiache status quo iliyotifikisha hapa tulipo kwenye umasikini uliokithiri siyo kuwa out of touch ni kitu gani?
Mafanikio ya nchi huyaangaliwi kwa kutizama kuhusu familia yako ama marafiki zako(kama wanavyofanya cronies wa ccm).
Hata kama wanakula na kulala vyema/kusaza na kufanya biashara zao vyema,bado hicho siyo kipimo cha kusema Tanzania wananchi wake wana unafuu ama tuna maendeleo.Tunapima kwa kuangalia wengi wa wananchi wanaishi maisha ya namna gani,na wengi wa wananchi wako vijijini.
Tuna raisi ambaye serikali yake inaingia mikataba ya hovyo ya rasilimali zetu huku akiendelea kuzunguka na kutembeza bakuli.Hakuna ile hali ya imani kwa wananchi kwamba tuna uongozi na tunapigadi hatua kama taifa,badala yake tuna rudi nyuma in terms of poverty amongst the people.
Hatuangalii maendeleo kwa uzinduzi sijui wa kivuko na mambo sijui ya mabasi ya kasi na train za Dar es Salam!nenda vijijini kuliko na wananchi walio wengi utizame maisha yao ndiyo utajuwa!
Its all about priorities,halafu kuna mtu anaitwa mwanakijiji ambaye kiukweli hayajui maisha ya kweli ya mwanakijiji wa Tanzania,anathubutu kusema ccm waendelee kutawala!
Na ndivyo hivyo ambavyo serikali ya ccm imekuwa ikifanya(kufukarisha wananchi wake),halafu eti mnakuja kusema hali hiyo iendelee kwasababu chadema hawajasema hili ama lile,sasa unataka tuite kitu gani hayo mambo?Ndiyo hayo yanayonishangaza sana tu mkuu wangu!