I salute you Kichwa Mbovu.
Umesema kitu ambacho maofisa wakuu wa serikali na hata wenye dhamana ya usalama wamekuwa wanashindwa kuitofautisha kutoka katika ukweli na dhana ambayo haina malengo bali kuelemea upande mmoja.
Mauaji ya Dr Mafingo, Sheikh wa wilaya huko Mtwara nk yanayohusu waislam hutasikia kauli ya aina hiyo kutoka kwa IGP, Rais, Waziri hata maaskofu, ngoja sasa auawe mkiristo, utasikia alshababy, alqaida, nk. Hali hii si shwari kwa mustakabali wa nchi yetu katika kujenga umoja ambawo unaelekea kukosa mashiko pale waislam wanapolalamika kuhusu dhulma. Serikali na wakristo watapinga au kukaa kimya bila kujibu hoja badala yake wataomba serikali iifungie radio imani. Huu si uadilifu wa kiuchamungu. MuchamUngu atatetea haki hata kama ni chungu kwake au inapelekwa kwa adui yake.
Tazama jinsi magazeti yanavyotoa taarifa za matukio ya kiislam au waislam na yale ya kikirito na wakristo. Ukisoma habari ya waislam ujue imetoka bakwata hapo utaiona kwenye magazeti ya mwanachi, mtanzania, majira nipashe, nk. lakini itoke kwa wasiokuwa bakwata hata kama ni kubwa vipi -ukibaatka ni magazeti ya kiislam tu ndo yataandika. Upendeo hu wa wazi hauna tija kwa amani ya nchi
Tazama anapofariki kiongozi wa wakristo -ikulu na mawaziri wote wataamia huko, ngoja iwe ni kiongozi wa waislam na ambaye siye bakwata-hutomwona rais , waziri au yeyote kuhudhuria. Sheikh Bacho alikuwa ni kiongozi mkubwa wa waislam -kiongozi wa serikali hakuna aliyehudhuria maziko yake, hakuna gazeti la bara lililoripoti hata moja. Huu utaratibu unaamusha hasira na kufikiri zaidi ya kawaida kwa watendewa. Amani haijengwi hivyo. Tukiacha unafiki unaofanywa na seriali na viongozi wa makanisa ,amani itajengejeka tu, amani siyo zao la propaganda, ni zao la uadilifu tu.
Lakini pia dhulma ikiachwa ni kwa faida yetu sote, vinginevyo ni maafa kwetu sote, hivyo tuacha ushabiki wa kidini huku tukijificha chini ya mwavuli amani.